Mnyika: Uamuzi wa mahakama umetengeneza athari na madhara kwenye mfumo wa utoaji haki katika taifa letu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,650
218,105
FCOCGi9XsAEiEPv

Picha: John Mnyika akizungumza na Vyombo vya Habari
Leo tarehe 21/10/2021 Chama cha Demokrasia na Maendeleo kitazungumza na Waandishi wa Habari wa Kimataifa na wa ndani kwenye ofisi za chama hicho nje ya Jiji la DSM, huko Kinondoni, kuanzia saa 6 kamili mchana.

Wote mnakaribishwa.

Muhimu: Tufuate mwongozo wa WHO wa kujikinga na corona.
===
Mkutano umeanza ambapo Katibu Mkuu wa CHADEMA J.J. Mnyika anatarajia kuzungumza kuhusu maamuzi yaliyotolewa na mahakama kuhusu Uamuzi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi katika shauri dogo linalimuhusu Mbowe pamoja na wenzake watatu.

John Mnyika ameanza kuzingumza na Wanahabari
Mnyika:
Uamuzi uliofanyika jana umekwenda kutengeneza athari, taathira na madhara kwenye mfumo wa haki katika taifa letu kwa sababu maamuzi ya Mahakama Kuu hata kama yemetolewa na Jaji mmoja yana ushawishi kwa Majaji wengine wa mahakama kuu pamoja na kuwa hayawalazimishi lakini pia yanaziongoza mahakama nyingine za chini.

Mnyika: Hukumu ya jana imekwenda kutoa mwanya na muongozo usiokuwa halali kwa misingi ya haki na misingi ya kisheria ambao:

Mnyika: Mosi, unatoa mwanya kwa polisi kwa kisingizio cha kutokukamilika kwa upelelezi ama kisingizio cha kumsafirisha mtuhumiwa au kisingizio kuna mtu mwingine wanamtafuta kama sehemu ya upelelezi kuwashikilia Watuhumiwa kinyume cha haki, kinyume cha Sheria zaidi ya masaa manne bila kuwaandikisha maelezo.

Mnyika: Kwahiyo matokeo yake hayatakuwa kwa Mwenyekiti Mbowe nchi nzima huko sasa. Hukumu ya jana imetolewa na mtu ambaye amepandishwa hadhi ya kuwa Jaji Kiongozi, na Jaji kiongozi kwa katiba sio tu msaidizi wa Jaji Mkuu bali ni Mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania. Jukumu la kuipinga Hukumu hii linapaswa kuwa la kila Mtanzaia na kila mpenda haki popote pale.

Mnyika: Msingi wa pili mbovu na mbaya wa kisheria kinyume na misingi ya haki uliowekwa na huku ya jana ni kwamba Polisi wamepewa mwanya wa kufanya mateso kwa Watuhumiwa kinyume na Police General Orders (PGO) kinyume cha Sheria, Kinyume cha haki kwa haki hizo kupokonywa kwa kivuli cha masuala ya kiufundi.

Mnyika: Kutokana na maamuzi ya upande mmoja wa kusikiliza na kuheshimu hoja za upande mmoja, hoja ambazo hazikuwa halali bila Mahakama kuchukua jukumu lake la kusimama mstari wa kati wa kusikiliza na kuchambua hoja za pande zote na kufanya uamuzi wa haki.

Mnyika: Kwa hukumu ile athari yake ni kwamba polisi ambao wakati wa kusikilizwa kwa shauri dogo walianza kupewa somo kuhusu kuheshimu PGO'S katika ukamataji, usafirishaji na upelelezi sasa wamefunguliwa mlango ya kuendelea kukiuka sheria na kukiuka haki.

Mnyika: Kwa jambo hili la pili vilevile, wajibu wa kuipinga hukumu hii ni jukumu la kila mpenda haki ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu. Kwahiyo nilitaka niseme hayo kuweka msingi wa mazungumzo.

Mnyika: Tatu, ni imani yetu kwamba yale yaliyofanyika jana na uamuzi uliofanywa na Jaji Kiongozi ni matokeo ya kwamba hukumu dhidi ya Mwenyekiti Mbowe ilishatolewa nje ya mahakama hata kabla ya kuendelea kusikilizwa kwa hili shauri dogo.

Mnyika: Kwahiyo, Mbowe alikwisha hukumuwa kabla ya kusikilizwa na wenye mamlaka na kwa sababu wenye mamlaka mamehukumu kabla ya kusikiliza mahakama inaingiliwa. Mhakama tunayoiheshimu kama chombo cha juu cha haki na kwa sababu katiba yangu ya sasa haina misingi thabiti ya kulinda uhuru wa mahakama, inakuwa rahisi mahakama kuingiliwa hatimaye kushindwa kutenda haki na kutenda haki huku haki ikionekana kutendeka.

Mnyika: Leo tarehe 21/10/2021 ni siku ya Haki za Binadamu Afrika, nawatakia Watanzania na Wafrika wote heri katika siku ya Haki za Binadamu Afrika.

Mnyika: Naviomba Vyombo vya Habari siku ya leo,siku ya haki,utawala wa awamu ya sita Rais alipoapishwa kuna wakati alizungumza kuhusu haki na uhuru wa Vyombo vya Habari Hapa ninapozungumza mkiwa wawazi mnaweza kueleza kwa uwazi kwamba uhuru na haki zenu zimeanza kuingiliwa.

Mnyika: Natoa wito kwenu Vyombo vya Habari bila kujali vitisho, vishawishi vya fedha na matangazo ni vyema mkaurusha mkutano huu na Waandishi wa Habari moja kwa moja na wale watakaoenda kurusha baada ya hapa na wale watakaoandika baada ya hapa mkaandike kwa uhuru na haki.

Mnyika: Uvunjaji wa haki ukihamia mahakamani ni hatari sana kwa mustakhabali wa watu na nchi. Hili tukio la uamuzi uliofanywa jana na Jaji siani kwa kila anayetafakari kuhusiana na haki za binadamu na haki za watuni vema akasikiliza na akaitafakari katika muktadha mpana wa haki.

Mnyika: Mara ya mwisho nilizungumza nanyi kuhusu kesi ya Mwenyekiti tarehe 31/07/2021 wakati ule niliwaambia kauli ambayo niliwaambia kufunguliwa kesi ya mashtaka ya kubambikiza ya Ugaidi dhidi Mbowe ni shambulio dhidi ya uhuru, haki na dhidi ya demokrasia.

Mnyika: Nikawaasa kesi hii isichuliwe ni ya Mbowe pekee yake, isichukuliwe kama ni shambulio dhidi ya Chadema pekee yake kwa sababu madhara yake kwa nchi na wananchi yatakuwa makubwa kuliko shambulio dhidi ya Mbowe na Chadema, madhara yatakuwa kwenye uhuru, haki na demokrasia
 
Jambo baya ukishindwa kulitatua kwa mikono basi angalau likemee kwa Maneno ya mdomo wako. Kama haiwezekani kulisemea basi onesha kulisusia usifungamane nalo.

Haya ni Mafundisho kutika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Mohammad (s.a.w) Akiunasihi Ummat Muhammad
 
Chadema fanya mchakato mpate kaimu mwenyekiti as makamu wa mwenyekiti yupo nje ya nchi ili muwe na vikao vya kuendesha chama na kufanya maamuzi. Vinginevyo nasikitika kusema hiki chama kinakwenda kufa
 
Shida ya Mbowe ni uenyekiti, aachie uenyekiti Chama kiongozwe na mtu mwenye maono. Tushachoka na huyu bibi kidude na lichama lake, kumkabili ukiwa jera ni vigumu. We need a smart active head!

(Sasa kwa makuku yalonyeshewa kama mitanzania tutaishia kuandamana mioyoni)
 
Shida ya Mbowe ni uenyekiti, aachie uenyekiti Chama kiongozwe na mtu mwenye maono. Tushachoka na huyu bibi kidude na lichama lake, kumkabili ukiwa jera ni vigumu. We need a smart active head!

(Sasa kwa makuku yalonyeshewa kama mitanzania tutaishia kuandamana mioyoni)
Uenyekiti wa Mbowe unazuia kitu gani ?
 
Kila aliyeitamkia kifo Chadema alikufa yeye
Tatizo CHADEMA kila anayewashauri mnamuoma hana akili mimi nawambia CHADEMA inahitaji reforms watu wengi saizi CCM walishaichoka pia kuna kundi kubwa la watu lilikuwa linamshabikia Magufuli sio CCM,ili muweze kulichukua kundi hilo fanyeni mabadiliko madogo yatakayowafanya wananchi kuwaona nyinyi ni kimbilio!

Lakini mmegeuka kuwa wanaharakati na kuwakabidhi chama akina na Pambalu watu wanaoongea kwa jaziba huku wametokwa na mishipa ya shingo wakitukana kila mtu, mfano sisemi Magufuli ni mtu mwema alikuwa na Makosa yake,ila sasa ameshakufa hatuko maye tena lakini nyinyi mmebaki kutukana tu kuhusu yeye mwisho wa siku ....... matokeo nini?

Mnaamini huyo Magufuli alikuwa hana watu wanaompenda vipi hao watu mtawashawishi vipi kuja kwenu huku wanaona mna maneno mengi ya kukera? Mawashauri achaneni ma mambo yasiyo ya msingi Magufuli aliwanyanyasa kila mtu anajua ila achaneni naye aliyepo mbele yenu ni CCM ili muweze kushinda uchaguzi mjipange wananchi wakiwakubali hata kwa katiba hii CCM wataachia tu maana hakuna marefu yasiyo na ncha,Hata CCM hii hakuna mtu anahangaika nayo na wananchi wako tayari ka mabadiliko wanawasubiri nyinyi na vyama vingine!
 
Vyombo vya habari vya kimataifa vitakuwapo? Cdm ikikohoa dunia inasimama ikipiga chafya dunia inarejea kwenye mzunguko wake tena
 
Back
Top Bottom