NG'WENEKELE
Member
- Mar 7, 2011
- 14
- 0
Juzi nikiwa natizama kipindi cha daladala kinachorushwa na itv kila siku saa moja jioni.kuna tetesi mh. J.mnyika umechukua ela kutoka kwa magari ya maji taka ili yaendelee kumwaga maji taka hayo katika mabwawa ya kiwanda cha urafiki yaliyopo mabibo.je tuhuma hizi zina ukweli?tujulishe wapiga kura wako wa mabibo.
, nasikia siku alipopewa ile cheki ya Tshs 90m alichanganyikiwa akaanza kutetemeka , kwani hakuamini kabisa kama angeweza kupata hela kama hizo
Kumbe hili ni jukwaa la umbeya?
Juzi nikiwa natizama kipindi cha daladala kinachorushwa na itv kila siku saa moja jioni.kuna tetesi mh. J.mnyika umechukua ela kutoka kwa magari ya maji taka ili yaendelee kumwaga maji taka hayo katika mabwawa ya kiwanda cha urafiki yaliyopo mabibo.je tuhuma hizi zina ukweli?tujulishe wapiga kura wako wa mabibo.
mbunge hana mamlaka ya kutoa kibali cha gari la maji taka limwage wape,hipo kazi ya halmashauri....NG'WENEKELE kama huna cha kuandika unaweza kusoma walichoandika wenzako itakusaidia pia..sio kuandika utumbo tu ili na wewe uonekane uwa unapost humu...kaendelee na kazi ya kuvua gamba huko
Nakubaliana na wewe mkuu. Mbunge hana uhusiano wowote na utoaji wa idhini ya kutumia eneo au kukataza. Wenye idhini ya kufanya hivyo ni Wakurugenzi wa manispaa au jiji. Unapotuhumu mtu inabidi ijifahamishe kwanza na taratibu za uendeshaji wa serikali yetu ya Wadanganyika.sidhani kama mbunge aweza kuidhinisha eneo la kutupa taka!!!
Na kama alipewa hiyo rushwa basi mtoa rushwa si mfanyabiashara maana hajui namna ya kutumia fedha yake!!! IF SO THEN, HE GAVE THE WRONG PERSON!
Huu ni mchezo mliotumwa na chama chenu cha magamba mje JF kujaribu kuleta propaganda zenu za siasa za maji taka. Bahati mbaya mnazileta kwa watu ambao siyo mazezeta kama mlivyo huko kwenu na hivyo hoja zenu hazipata mashiko kirahisi kama siyo ninyi kupoteza muda wenu kirahisi na kwa gharama nafuu ya kupewa T-Shirt na kofia za njano.Sasa mbona umekuja juu? tulia watu waandike uone jinsi kijana wenu alivyo nae fisadi, niliisha wahi kusema humu ndani hakuna mtu msafi CDM hata mmoja, yataanza kujionyesha kwa mmoja baada ya mwingine, haya ya mnyika hayo sasa
Kijana ameingia kwa kasi sana kukamata mshiko, nasikia siku alipopewa ile cheki ya Tshs 90m alichanganyikiwa akaanza kutetemeka , kwani hakuamini kabisa kama angeweza kupata hela kama hizo
Hizi ni habari za ndani kabisa na za uhakika, na tena huyu dogo kwenye akaunti yake ameingiziwa Tshs 280m kwenye benki fulani, muulizeni amepewa na nani ? asije kuwa anatumiwa na mapacha 3
watu kama geniusmavi china mnanyongwaSasa mbona umekuja juu? tulia watu waandike uone jinsi kijana wenu alivyo nae fisadi, niliisha wahi kusema humu ndani hakuna mtu msafi CDM hata mmoja, yataanza kujionyesha kwa mmoja baada ya mwingine, haya ya mnyika hayo sasa
Jamani wana JF!
Ndio maana JF inaonekana ni CDM kwa kupinga kila kinachoibuliwa against CDM na kuunga mkono kila kinachohusu ccm, mngeambiwa J. Makamba kapewa hela na makampuni ya madini kusafirisha udongo wenye dhahabu nje ya nchi naamini mngeendelea kudodosa na kusaka ukweli na sio kumjibia kuwa hiyo ina mhusu waziri wa madini kama mnavyomjibia Mnyika sasahivi. Ingawa habari hiyo ni tetesi lakini source imetajwa kipindi cha daldala ingawa ushahidi zaidi katika hilo unahitajika na pia sio lazima kila tuhuma ijibiwe lakini ukimya pia unaleta hisia za kuwepo kwa viji chembechembe vya ukweli lakini pia watu huchokoza ili wapate kitu flani ndani yake. Tuvumiliane jamani tunapotofautiana.