Cool down baby, mbona unaandika blah blah?! ivoo ndio nini? Next time unaongea na mimi, anza na shikamoo.
Wewe unafahamu tuna serikali makini, hapa kazi tu...mbunge ana haja gani ya kufuatilia na hali serikali ni makini? Tangu lini serikali ya awamu ya 5 ikafanya mambo kwa 'mujibu wa bunge?' Ina maana hujui kuwa kuna barabara zinajengwa nje ya bajeti?
Well, usije ukadhani 2015 ndio nimepiga kura mara ya kwanza kama wewe, niko humu duniani kwa miongo kadhaa. Nafikiri wakati napiga kura kwa mara yangu ya kwanza, mama yako alikuwa bado kigori, kwa hiyo ukisikia nimekwambia kitu juu ya wanasiasa, tafakari kwanza, niko nao siku nyingi.
You are such an innocent girl, maisha haya ya fitina na unafiki bado huyajui. Mbunge, hata apige kelele kiasi gani bungeni kelele zake hazijengi barabara. Sisi tuliozaliwa huku mjini, tunapochagua mbunge huwa tunaadhimia overall responsibility ya mwakilishi kwa taifa na sio jimbo. Mbunge wa Ubungo mathalan, hatumtarajii kusimama aongee kuhusu madawati...tunataraji kumsikia yanapojadiliwa mambo makubwa ya uchumi wa hii nchi. Nafikiri unaweza kuona jinsi ambavyo ilikuwa ngumu VAT ya miamala ya simu kujadilika vyema na kupatiwa tafsiri bungeni, badala yake taasisi mbili za serikali (BoT na TRA) zikaja kulumbana nje. Hii yote ni kwa sababu, wabunge wa mjini hawakuwepo, waliobaki ni wale ambao wametumwa na nyie watu wa kijijini kuomba zahanati ili kwamba wadogo zako wasizaliwe tena onyuma yo mti wakapata akili za mfano wako.
Impact ya Mnyika kufunga plasta sio Kibamba kukosa barabara na maji. Impact ya Mnyika & CO kufunga plasta ni kwa hoja muhimu na nzito kukosa wa kuzijadili matokeo yake zinakuja kujadiliwa nje. Waliobaki ndani waliishia kuwajadili waliotoka na kuomba vitu muhimu kwa jamii zao, ikiwamo UWANJA WA KUMBUKUMBU YA PUSH UP...asalaaam aleikhum Bi Mdogo!