Mnyika: Ndugai alitumwa na akajiandaa

Mnyika: Ndugai alitumwa na akajiandaa

WISE BOY

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2011
Posts
782
Reaction score
244
Mh Mnyika ktk kipindi cha "tuongee asubuhi" ndani ya startv ameeleza kuwa naibu spika mh ndugai aliagizwa na NEC kihakikisha matakwa ya ccm yanapita ktk katiba, hvyo alichokua anafanya bungeni juzi ni kutekeleza maagizo.

Pia kasema askari walioingia kuleta fujo bungeni waliandaliwa kabisa na wengine hata si askari wa pale bungeni na ana ushahidi akitakiwa kuutoa maana anawafahamu kwa sura na majina (akimaanisha ilipangwa mapema liwalo na liwe lkn matakwa ya wapangaji yatimie.

Amezungumza mengi machache ya hayo ni kuonyesha jinsi gani Zanzibar hawajashirikishwa (na yeyote anaesema wameshirikishwa na mwongo), upinzani walichokuwa wanakifanya ni "filibustering".

Pia akamalizia kwa kusema hatua inayofuata ni kurudi kwa wananchi wao ndio waamue muafaka wa katiba mpya "nguvu ya umma"
 
Ndugai ni kama Robot tu,kuna mambo mengine mtu hawezi kukubali kujiaibisha eti kisa katumwa na bwana wake,kama pale ndugai amejivua nguo kabisa,ni mtu asiye na ubongo tu ndiye angeweza kufanya upuuzi kama ule.
 
Hiyo ndio ccm kwa nguvu hamtoweza kuitoa...ila kwa kutumia akili mtaweza, wapinzani undeni chama kimoja ili kuingoa ccm kinyume na hapo mtaishia kuburuzwa kila siku mimi yangu macho
 
Hata kama umetumwa cyo vile bhana ndugai kachemsha mnoo upande wake ndugai kadai hakuna kanuni za bunge zinazomtaja kub jamaa kapanic wakati huo huo hakuna kanuni za bunge zinazomtaja naibu speake jamaa ndugai anajificha kwenye jiko la mkaa
 
Hiyo ndio ccm kwa nguvu hamtoweza kuitoa...ila kwa kutumia akili mtaweza, wapinzani undeni chama kimoja ili kuingoa ccm kinyume na hapo mtaishia kuburuzwa kila siku mimi yangu macho

Mkuu waunde CHAMA KIMOJA kwa Katiba ipi?
 
the only option unganeni
gawaneni majimbo ya uchaguzi, pigeni kampeni kwa pamoja
nina uhakika wabunge wa Upinzani mtakuwa wengi zaidi na mtakingoa chama cha mafisadi.
Chadema hadi saa wana uhakika wa kuzoa kila jimbo watakalomsimamisha mgombea wao
undeni mseto wenu wapinzani. simple
 
Ile picha hata mtoto mdogo anaweza kugundua kwamba ndugai alidhamilia kufanya aliyoyafanya....!
 
Mi sijui nisemeje?sio CHADEMA wala CCM,wote hawana nidham,hakuna anaye msikiliza mwenzie,kila chama kinatafuta kujifaharisha sio kwa faida ya wana nchi.Nadhani kama sikuile ya mgogoro uliangalia bunge uliwasikia Lukuvi na Lissu,mi nilipata jibu siku hiyo na kuvidharau vyama vyote viwili.
 
Siku nyingine CDM waoneshe weledi ikiwa wanajua kuwa kuna mambo yamepangwa ili yaende basi wawe makini kukwepa mitego na sio kuingia mtegoni kisha kuja kusema kuwa waliishajua kuhusu huo mtego au mpango. wapaze sauti kabla ya kunaswa na mtego.
 
the only option unganeni
gawaneni majimbo ya uchaguzi, pigeni kampeni kwa pamoja
nina uhakika wabunge wa Upinzani mtakuwa wengi zaidi na mtakingoa chama cha mafisadi.
Chadema hadi saa wana uhakika wa kuzoa kila jimbo watakalomsimamisha mgombea wao
undeni mseto wenu wapinzani. simple

ni kweli kabisa km 2010 kulikuwa hakuna sababu ya mtatilo kugombea ubungo angegombea tmk
 
Hiyo ndio ccm kwa nguvu hamtoweza kuitoa...ila kwa kutumia akili mtaweza, wapinzani undeni chama kimoja ili kuingoa ccm kinyume na hapo mtaishia kuburuzwa kila siku mimi yangu macho


Kwa kuunda chama kimoja haiwezekani mkuu bali wawe kitu kimoja waachiane na waratibu majimbo wanapoona upepo ukoje katika kila jimbo husika hapo CCM haponi asilani kwani nii vigumu mno kuiba kura za jimbo,,ngangari wanasimamia kura zao kingangari, makamanda nao vilevile, hatoki mtu hapo lazima kinuke..

MWENZETU SUGU KESHAANZA KULA TIZI LA KULINDA KURA ZAKE AKIWA MJENGONI

SAFI SANA MBUNGE WANGU TUNAKUSUBIRIA MBEYA KAMA SHUJAA

"KIDUME KWELI HAKITISHIWI NYAU"
 
Mnyika naona sasa na yeye anaelekea kukosa ya kuzungumza, "kutumwa" nayo ndio hoja ya kuita press na kuwaeleza, hili neno ni utamaduni wetu na umeshazoeleka, jambo likifanyika utasikia "umetumwa nini" huo ni utamaduni wa kimazoea , na si hoja ya kujengeka, engetuambia kama ni sahihi alichofanya sugu pia..
 
Tumeanza na mungu tutamaliza na mungu 2015
 
Back
Top Bottom