Kuwavua Ubunge Halima Mdee na wenzake bila kumshtaki Dkt. Mahera na Mnyika kwa kuhujumu Uchumi itakuwa ni kuwaonea bure

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,870
Kuna kila dalili kwamba wabunge wa viti maalumu wa Chadema wote 19 wataondolewa bungeni kwa sababu waliingia kinyume na matakwa ya katiba ya JMT

Tundu Lissu aliongea, Spika Tulia aliongea na sasa Rais Samia ameongea na hata Watanzania waishio Marekani wameongea.

Sote tunajua Covid-19 hawajajipeleka wenyewe bungeni bali walialikwa na Dr Mahera kisha wakaapishwa na Spika Ndugai.

Lakini hata Katibu mkuu wa Chadema hakuchukua hatua zozote za kisheria kama ni kweli saini yake ilighushiwa pale Tume ya Uchaguzi

Natoa angalizo, kabla ya kuwatimua akina Halima Mdee na wenzake ni haki tena ni wajibu Mahera na Mnyika wakachunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

Ramadan kareem!
 
UVCCM mkivibiwa mnakuwa wapuuzi kweli, Bonaphace Jacob alitaka kumfungulia kesi Makonda kwa kufoji alisikilizwa na nani? angali Nondo pia alitaka tu kujua utajiri wa Makonda kamishina wa tume tena Jaji akakataa, kwa ule utawala wa shetani ungemfungulia kesi nani ambaye ameletwa na dola?
 
Kwahiyo Bonny ndio Chadema?

Wewe Bawacha bure kabisa!
 
Sote tunajua Covid-19 hawajajipeleka wenyewe bungeni bali walialikwa na Dr Mahera kisha wakaapishwa na Spika Ndugai.

Lakini hata Katibu mkuu wa Chadema hakuchukua hatua zozote za kisheria kama ni kweli saini yake ilighushiwa pale Tume ya Uchaguzi

Natoa angalizo, kabla ya kuwatimua akina Halima Mdee na wenzake ni haki tena ni wajibu Mahera na Mnyika wakachunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki.
Mtamuonea KM Mnyika bure.. kama kuna saini yake ilighushiwa waulizwe Mahera na Ndugai waliokutwa nayo. Anayekutwa na ngozi ndo mwizi!

Wahusika wa huo utapeli na ufisadi wa fedha za walipa kodi maskini kugharimia wabunge feki wa C19, ni Mahera na Ndugai Kwa idhini ya jiwe🙄
 
Mtamuonea KM Mnyika bure.. kama kuna saini yake ilighushiwa waulizwe Mahera na Ndugai.

Wahusika wa huo utapeli na ufisadi wa fedha za walipa kodi maskini kugharimia wabunge feki wa C19, ni Mahera na Ndugai Kwa idhini ya jiwe🙄
Ndugai anahusikaje hapo?
 
Back
Top Bottom