Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,415
- 12,627
- Thread starter
- #121
Nafikiri mada ibadilike na tujadili jinsi ya kumtoa Myik... tufungue page na wadau wote wa kibamba ambao hawaridhiki na Mbunge wetu tujadiliane kwa kina jinsi ya kumtoa. Lazima ieleweke kwamba hatuna Mbunge hivyo hakuna maana ya kuendelea kuongozwa na kivuli. Mabifu yao yasitunyime haki ya kuwakilishwa. Kweli tutamkumbuka Dr. Fenella pengine nasie tungekuwa tunajidai kama wengine. Yaani inauma ukiona wabunge woote wanashiriki kwenye shughuli za maendeleo lakini leo hii Kibamba barabara zimeoza, maji hakuna, umeme Msumi B imekuwa ndoto, Afya vituo vinafungwa saa tatu asubuhi, vituo vya polisi mwisho saa kumi na mbili. Watu hawana amani saa kumi na mbili wafanya biashara saa kumi na mbili wameishafunga kisa usalama. Hili jimbo tukubali tusikubali tumelipoteza sasa mkakati uwe tunalirudishaje? Miaka kumi ni kama tumepotea. Wewe mwaka unakwisha Mbunge hatujui ana vipao mbele vyake ni nini? Je ametekeleza nini? Inauma sana sana. Huyu jamaa hafai hata kidogo.
Mkuu katiba hairuhusu hiko kitu, hata hivyo nadhani Mnyika bado ana nafasi ya kubadilika na kufanya vizuri.
Sidhani kama kweli Mama Mkangara angeweza kufanya lolote na kuleta mabadiliko, ukoo wa CCM ni ukoo wa CCM tu. Wao ndo waliotufikisha hapa na hawana mbinu za kututoa hapa na kutupandisha.