Mnyika kalisahau jimbo lake la Kibamba

Mnyika kalisahau jimbo lake la Kibamba

Acha uongo, kukopeshwa ni meya akishirikiana na DCB wala siyo mnyika, tena sio kibamba tu ni kinondoni yote,
Nafikiri mada ibadilike na tujadili jinsi ya kumtoa Myik... tufungue page na wadau wote wa kibamba ambao hawaridhiki na Mbunge wetu tujadiliane kwa kina jinsi ya kumtoa. Lazima ieleweke kwamba hatuna Mbunge hivyo hakuna maana ya kuendelea kuongozwa na kivuli. Mabifu yao yasitunyime haki ya kuwakilishwa. Kweli tutamkumbuka Dr. Fenella pengine nasie tungekuwa tunajidai kama wengine. Yaani inauma ukiona wabunge woote wanashiriki kwenye shughuli za maendeleo lakini leo hii Kibamba barabara zimeoza, maji hakuna, umeme Msumi B imekuwa ndoto, Afya vituo vinafungwa saa tatu asubuhi, vituo vya polisi mwisho saa kumi na mbili. Watu hawana amani saa kumi na mbili wafanya biashara saa kumi na mbili wameishafunga kisa usalama. Hili jimbo tukubali tusikubali tumelipoteza sasa mkakati uwe tunalirudishaje? Miaka kumi ni kama tumepotea. Wewe mwaka unakwisha Mbunge hatujui ana vipao mbele vyake ni nini? Je ametekeleza nini? Inauma sana sana. Huyu jamaa hafai hata kidogo.
 
Wewe unachomtuhumu Mnyika ni nini..mana mnadai hajawasemea bungeni mara hamna alichofanya jimboni mnapewa ukweli mnaweweseka au ndo degedege za ukubwani
Ukweli gani? Hv anaeweweseka ni nani kama sio nyie mnaojitahidi kutetea hata makosa? Hao wapinzani wao wasafi tu? Akili hamna nyie
 
Nafikiri mada ibadilike na tujadili jinsi ya kumtoa Myik... tufungue page na wadau wote wa kibamba ambao hawaridhiki na Mbunge wetu tujadiliane kwa kina jinsi ya kumtoa. Lazima ieleweke kwamba hatuna Mbunge hivyo hakuna maana ya kuendelea
kuongozwa na kivuli. Mabifu yao yasitunyime haki ya kuwakilishwa. Kweli tutamkumbuka Dr. Fenella pengine nasie tungekuwa tunajidai kama wengine. Yaani inauma ukiona
wabunge woote wanashiriki kwenye shughuli za maendeleo lakini leo hii Kibamba barabara zimeoza, maji hakuna, umeme Msumi B imekuwa ndoto, Afya vituo vinafungwa saa
tatu asubuhi, vituo vya polisi mwisho saa kumi na mbili. Watu hawana amani saa kumi na mbili wafanya biashara saa kumi na mbili wameishafunga kisa usalama. Hili jimbo
tukubali tusikubali tumelipoteza sasa mkakati uwe tunalirudishaje? Miaka kumi ni kama tumepotea. Wewe mwaka unakwisha Mbunge hatujui ana vipao mbele vyake ni nini? Je
ametekeleza nini? Inauma sana sana. Huyu jamaa hafai hata kidogo.
Endeleeni kujidanganya na mama yenu anaesuka twende kilioni..mwanaume ukiwa na husuda kwa mwanaume mwenzio ni tatizo
 
Aisee, kwahyo kwa kipindi ambacho bunge hakuna wale tu bata? Daah hizi akili zenu hizi
mkuu sijasema hivyo pili elewa kuna kazi nyingine za kamati zinaendelea na pili elewa majukumu yake kwa kusoma katika na pili mbunge ni mjumbe kwenye baraza la madiwani.
 
Sasa atakuwakilisha bungeni kivipi wakati hakai kwenye mikutano. Sugu nae anaenda kutukana watu bungeni na wengine wanatoa takwimu za uongo ili kupumbaza wananchi.
Na niliwahi kujiuliza swali hivi kama chadema ingeingia madarakani huyu Mh.Mnyika angepewa wizara gani ambayo ingemfaa na huyu Mdeye nae je?
 
mkuu sijasema hivyo pili elewa kuna kazi nyingine za kamati zinaendelea na pili elewa majukumu yake kwa kusoma katika na pili mbunge ni mjumbe kwenye baraza la madiwani.
Ndo mana mtoa mada akasema hata katika baraza la madiwani hawamuoni, mbona kina lema, msigwa prof j tunawaona kila siku?
 
Hata Malamba mawili hajawahi kufika baada ya uchaguzi. mimi nasema kwa niaba ya Wana Malamba mawili. badilika Mh. Mnyika bado tunakuhitaji. njoo ongea na wananchi wako waliokuchagua. kwani mikutano ya mbunge aliyeshinda ktk jimbo si yanakubalika? au ubize wa chama umekuzidia. jitahidi maana zamani jimbo la Ubungo lilikuwa kubwa sana na ukatuambia inakuwia vigumu kufanya mikutano sehemu zote, tukakuamini, sasa jimbo limegawanyika na kuwa 2 in maana umerahisishiwa kidogo. Jitahidi Mh. Unatuangusha😎😎
 
Nasikia hilo jimbo kila ikifika saa kumi na mbili kasoro asubuhi; wagawa mwanga wanaondoka nao mpaka hapo jioni ya kumi na moja hivi.
Kazi inakuwa ni kwa wachoma magilili, wachana mbao, wauza nyama, samaki, vinywaji baridi, wafyatua matofali nk kupata kipato chao cha siku maana mwanga hamna!
Nani awaliliye hao masikini wa mkuu wa kaya anaotaka kuimarisha maisha yao. Nani ampigiye kelele yule Profesa aliyeahidi kuwashughulikia mameneja wake wasojishughulisha kuongeza mapato ya shirika na wateja wapya; ya kwamba yupo mmoja kati yao yeye yupo busy kuondoka na mwanga badala ya kuongeza ili mapato yaongezeke.
 
Mkuu mimi siyo mshabiki wa chama chochote, ila ninaamini Mnyika muda bado anao wa kufanya mabadiliko.

BTW, siyo kazi ya Mbunge kuleta maji, kutengeneza barabara, kuleta umeme; kazi yake ni kuiambia serikali ifanye majukumu yake.

Mnyika hajafanya hayo, sidhani kama Mkangara atafanya hayo, CCM no!


Mkuu umejenga hoja yako kwenye dhana dhaifu.

Hakuna aliyemdai Mnyika alete maji, barabara nk nk jimboni Kibamba kwa bidii au kwa pesa zake mwenyewe. Lakini kama mbunge ana jukumu la Utetezi "Advocacy" na Ushawishi "Influence" ama moja kwa moja akiwa bungeni au nje ya bunge katika majukumu yake ya kila siku. MNYIKA HAFANYI HIVO HATA KIDOGO!!

Sasa anafanya kazi gani hasa? Kwa nini alipwe pesa ya walipa kodi??? Tafadhali tuhabarishe.

Pili unaposema CCM No, ni sawa. Tungetamani kupata kiongozi toka chama mbadala. LakIni tayari tunaye na ndo hio type ya Mnyika. Au wewe unataka yupi maana tuliye naye ndo huyo Mnyika. Sasa si bora kujaribu na CCM kuliko kuendelea na failed guy bro??

Kumbuka majirani zetu wanatamani wangepata uongozi tulionao sisi hapa Tanzania ambao ndo hao (CCM) usio wataka with a big No.

Choose between an EVIL(MNYIKA-CHADEMA) and LESSER EVIL (MKANGARA-CCM)!
 
Mkuu umejenga hoja yako kwenye dhana dhaifu.

Hakuna aliyemdai Mnyika alete maji, barabara nk nk jimboni Kibamba kwa bidii au kwa pesa zake mwenyewe. Lakini kama mbunge ana jukumu la Utetezi "Advocacy" na Ushawishi "Influence" ama moja kwa moja akiwa bungeni au nje ya bunge katika majukumu yake ya kila siku. MNYIKA HAFANYI HIVO HATA KIDOGO!!

Sasa anafanya kazi gani hasa? Kwa nini alipwe pesa ya walipa kodi??? Tafadhali tuhabarishe.

Pili unaposema CCM No, ni sawa. Tungetamani kupata kiongozi toka chama mbadala. LakIni tayari tunaye na ndo hio type ya Mnyika. Au wewe unataka yupi maana tuliye naye ndo huyo Mnyika. Sasa si bora kujaribu na CCM kuliko kuendelea na failed guy bro??

Kumbuka majirani zetu wanatamani wangepata uongozi tulionao sisi hapa Tanzania ambao ndo hao (CCM) usio wataka with a big No.

Choose between an EVIL(MNYIKA-CHADEMA) and LESSER EVIL (MKANGARA-CCM)!

Mkuu ki-ukweli nimependa sana ulivyojenga hii hoja, sana.

Mimi kusema CCM no ni kwa sababu kuu zifuatazo:-

1. Jimbo la Ubungo limewahi kuwa Chini ya CCM, haya matatizo hayakupungua, na Mnyika karithi jimbo la Ubungo likiwa na kero hizi hizi.

2. Serikali kuu iko chini ya CCM, nina uhakika serikali inayajua maeneo yote ya nchi na hali halisi ya miundo mbinu yake, maji, umeme, huduma za kiafya nk, sioni kama inafanyika jitihada zozote za kuyatatua haya kutoka serikali kuu.

3. Kwa miaka zaidi ya 50, chini ya utawala wa CCM maisha yameendelea kuwa magumu, tena sana! Sasa kuendelea kuwakumbatia ni kukumbatia umaskini, hawabadiliki.
 
Back
Top Bottom