Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,415
- 12,627
Mimi ni Mkazi wa jimbo la Kibamba, nilimpigia kura yangu Mh Mnyika bila hata ya kuzisikia sera zake, ni moja ya wabunge vijana niliokuwa nina imani nao sana sana hasa kutokana na michango yake bungeni (Bunge lililopita), harakazi zake za kisiasa akishirikiana na wenzake kipindi hicho kabla Chadema haijamkaribisha Lowassa.
Kiukweli toka Bunge hili jipya lilivyoanza kumekuwa na tetesi mbali mbali juu mwenendo wa Mh Mnyika kisiasa, wengine wakisema hashirikiani na wenzake kwa sababu hajamkubali EL, anataka kujitoa kwenye chama etc etc, huku yeye akiwa kimya.
Sasa basi toka tumemchagua Mnyika, hajawahi hata siku moja kuja jimboni either kutoa shukran kwa kura alizopewa, au hata kuhudhuria vikao vya madiwani, kufanya mikutano ya kisiasa jimboni, kufanya mikutano na wananchi wakamweleza kero zao ili angalau hata akazisemee Bungeni.
Mnyika ni wakati sasa wa kubadilika kama kweli anataka maisha yake ya kisiasa yaendelee, au ampishe mtu mwingine anayetaka kuwawakilisha wananchi Bungeni.
Mnyika popote ulipo, fanya shughuli za chama lakini kumbuka wananchi waliokuchagua ukawawakilishe, haututendei haki, sitaki kujuta kwa kutompa Dr Fenella Mkangara (CCM), lakini ninaamini kwa mwenendo huu watu tutaanza kujiuliza mara mbili mbili juu ya kama tulipoteza kura au la!