Mnyika ashinda kesi dhidi yake; Hawa Nghumbi atakiwa kulipa gharama za kesi!

CCM Imeshachukiwa hata Kama wana kizuri but jamii imeshagoma .. Jamii inataka mabadiliko no matter how it will cost them. Hata Kama mabadiliko hayata kuwa chanya but yawe manadiliko tu.. And that is.. CCM Knows this . Lakini .. Lakini....
 
Tafadhali wakuu, tusipotoshe maudhui ya hii thread. Kama unaona mtu anaingiza mambo ambayo ni nje ya hii mada ni vema ukampotezea.
 
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amemuudhi Jaji Upendo Msuya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kiasi cha kumtaka Wakili wake amuonyeshe kile jaji huyo alichosema ni sawa na kudharau mahakama.

Jaji Msuya alieleza kuudhiwa na mbunge huyo jinsi alivyokuwa akijibu maswali mbalimbali ya Wakili wa mlalamikaji, Issa Maige, wakati akijitetea katika kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi.

Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombe wa ubunge wa jimbo kupitia CCM, Hawa Ng’humbi.

Jana, Mnyika alipanda kizimbani kujitetea huku akikana madai yote na kudai kuwa, hata kasoro zinazolalamikiwa hazikuathiri matokeo, lakini alipobanwa kwa maswali na Wakili Maige alifika mahali akamuudhi Jaji Msuya anayesikiliza kesi hiyo.

Mambo yanayodaiwa kumuudhi Jaji Msuya ni jinsi Mnyika alivyokuwa akijibu maswali hayo, wakati mwingine alikuwa akijibu kinyume na swali na wakati mwingine kutoa maelezo marefu ambayo yalikuwa hayahitajiki.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Msuya alilazimika kuingilia kati mara kwa mara akimtaka Mnyika ajibu swali kwa kadri alivyokuwa akiulizwa, badala ya kutoa maelezo ambayo hayakuwa yakihitaji. Hata hivyo, Mnyika aliendelea kupiga chenga.

Hali hiyo ilimuudhi Jaji Msuya na Wakili wake, Edson Mbogoro alisimama na kumnong’oneza Mnyika mambo kadhaa.“Nafikiri wakili ni vyema pia umemwelewesha kuwa majibu mengine anavyojibu si sawa, na hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni dharau kwa mahakama maana nimeshamuonya na kumuonya lakini bado tu,” alisema Jaji Msuya.

Baada ya onyo hilo, Mnyika alionekana kutulia na kujibu maswali kadhaa ya Wakili Maige kwa utulivu na kwa kadri swali lilivyokuwa likiulizwa.

Katika hatua nyingine, Mnyika alipingana na aliyekuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Gaudence Kadiarara, kuhusu madai ya matumizi ya kompyuta zake (Mnyika) kuhesabia kura.

Majibu ya swali hilo ni miongoni mwa majibu yaliyoonesha kumuudhi Jaji Msuya kwa jinsi Mnyika alivyokuwa akijibu.
Wakili Maige: Kwa hiyo DW1 ni muongo?

Mnyika: Nimesema maelezo yake siyo ya kweli
Wakili Maige: Sawa, siyo sahihi kwa hiyo ni muongo, kweli au si kweli?
Mnyika: Nimesema maelezo yake siyo ya kweli.

Katika kujibu maswali ya Wakili Maige, Mnyika likiri kuwapo kwa dosari katika matokeo yaliyorekodiwa katika fomu ya matokeo ya jumla na kwamba, kwa jinsi yalivyorekodiwa siyo sahahi wala halali.

Pia, alikubali kuwa kama angeyabaini mapema asingesaini mpaka yangerekebishwa huku akikiri pia kuwa katika hali hiyo mwenye mamlaka ya kurekebisha dosari hizo kwa sasa ni Mahakama.

Mnyima pia alikiri tofauti ya kura zaidi ya 14,000 inayoonekana katika fomu hiyo yeye binafsi hawezi kuielezea.

Lakini katika awali katika ushahidi wake wakati akongozwa na wakili wake, Mbogoro Mnyika alidai kuwa dosari hizo haziathiri matokeo hayo na kwamba, hata kama ikithibitika kuwa tofauti ya kura hizo ni za Ng’humbi, bado hawezi kushinda.

Kwa nini umeweka hili bandiko?
 
Hivi hii CCM inavyoacha mambo nyeti kama haya na yanayomgusa mtu wa hali ya chini ya ripotiwe kwakiswahili wamejitahidi vipi kuwapa hao watu wa chini uwezo wa kuielewa hii lugha?

hapo sasa me mwenyewe sielew nilioj pale juu mtu akanijibu et kwan jaj alisoma sheria kwa kiswahili haya bana tuwaachie wanasheria
 
Wale wote ambao huwa mnaofanya live coverage ya tukio lolote naomba mjifunze kwa Yericko Nyerere. Hivi ndivyo tungependa updates ziwe zinaenda. Asante sana mkuu kwa kutupatia updates, tuko pamoja.
 
Kutumia simu Mahakamani ni kosa linaloweza kumpeleka mshtakiwa ndani kwa up to six months,sasa usije kukuta bwana Yericko amenaswa na sasa hivi anasubiri wenzake wakwee basi la kijani kuelekea Segerea,MBONA KIMYA namna hii!!!!
 
Ya Arusha mjini yakitokea hapa nitakuwa na furaha sana.
Hamna chochote huyu kijana alichokifanya ubungo
 
Ngoja ni mwambie mfanyakazi wangu aende store anichukulie lile faili lenye matusi nianze kuyamwaga hapa. mmmmmmmmhhhhhh nimekumbuka ngoja nitengeneze Id nyingine kwasababu matokeo yake ni Ban
 
Back
Top Bottom