Mnyika ashinda kesi dhidi yake; Hawa Nghumbi atakiwa kulipa gharama za kesi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika ashinda kesi dhidi yake; Hawa Nghumbi atakiwa kulipa gharama za kesi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, May 24, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Hali ya mambo ni nzuri watu hawana munkari kama ilivyotarajiwa hasa wale wa Chadema ndio wengi na wanaonyesha wana matumaini ya Ushindi,

  Hukumui haijaanza kusomwa tunaelezwa itaanza mida ya saa 3 hivi,

  Polisi kwa mida hii sio wengi sana kwa hesabu hawafiki 50. Kwa ujumla hali ni ya amani kabisa!

  Tutawajuza hatua kwa hatua moja kwa moja toka ukumbini!

  Updates:

  - Basi aina ya coaster lililobeba mashabiki wa chadema ndio linaingia huku likishangiliwa na watu kwa alama ya vidole viwili alimaarufu Amani na Upendo!

  - Naaaaam vijana wakazi (FFU) ndio wanaingia kwenye eneo la tukio wakiwa wamevalia kikazi yani kama Baghdad lakini wapo kwa usalama tu hakuna dalili ya vurugu yoyote hali ni yaamani tu!

  - Kuna mabishano ya hapa na pale kati ya wananchi na wahudumu wa mahakama, watu wanalalamika kuwa mbona mda unakwenda na hawaruhusiwi kuingia mahakamani! Lakini wamefanikiwa kuwasihii na wananchi wametuliza munkali

  - Tunaendelea kusubiri mda ufike tuanze kufuatilia kesi hii!

  - Naaaaam tumeshaingia ukumbini tayari kuanza usikilizaji wa kesi hii uendelee! Tumeambiwa tuzime simu lakini MIMI sitazima mwanzo mwisho!

  - Tunasubiri jaji aingie na jopo la mawakili wa pande zote wapo tayari!

  UPDATES:
  Kuna kichekesho kimejitokeza hapa, yani wakati wakuingia ukumbini kuna mbinu iliyotumika na mashabiki wa CDM kuwabana mlangoni wale wa Magamba na wakashindwa kupata siti kilichofuata ni afande kuwatoa nje, wakati wakitolewa nje kuna mwanachadema mashuhuri akaingia ukumbini na afande akataka kumuunganisha na wana ccm kutoka nje, unaambiwa ukumbi umelipuka na kusema huyo siti ipoo!

  Naaaaaaaaaaam Mh Mnyika ndio anaingia ukumbini anashangiliwa kwa makofi na Pipooooooozi Pawaaaaaaaaaaaaaa!

  Updates:
  Wakili wa Mnyika ndugu Mbogolo ndio anaingia anasalimiana na mnyika waapiga picha wanaendelea kupiga picha!
  Sasa kilichobaki ni kumsubiri jaji tu aingie ukumbini!

  Updates:
  Jambo la kufurahisha ktk kesi hii nikuwa Mh Mnyika na Hawa Ng'umbi wamekaa pamoja na wanapiga stori kweli, hata alipotokea afisa usalama akataka kuwatenganisha mnyika amemwambia haina tatizo watu pipoooooooooooz!

  UPDATES:

  M/Kiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe aka Sauti ya Zege ndio anaingia anashangiliwa ile mbaya pipooooooozi


  UPDATES:
  Mpaka dakika hii saa nne kamili bado Jaji haja ingia ukumbini, tunaendelea kumsubiri!

  UPDATES:
  Naaaam jaji ameingia na hukumu inaanza rasmi,

  Jaji anaomba radhi kuwa ataisoma hukumu kwa lugha ya kitumwa! Twendeleeee!

  Updates:
  Jaji anaendelea na mapitio ya mwenendo wa kesi nzima tangu ilipoanza na mpaka ilipo, kimsingi ameanzia kwenye historia ya kampeni,uchaguzi, uhesabuji kura na utangazwaji wa mshindi, sasa anaingia kwenye malalamiko makuu ya mlalamikaji,

  Vuteni subira naripoti kwa kificho maana tumeambiwa tuzime simu na kamera zote za wanahabari!

  Mtanisamehe nitaripoti yale muhimu tu, longolongo za jiji sitaziripoti mda wa kutafsiri lugha ya kitumwa sina!
  Jaji mwenyewe inamsumbua kusoma ana nasanasa tu wakati anaisoma kwenye karatasia utadhani kaambiwa aisome kichwani!

  Bado anaendela kusoma mwenendo wa kesi! Hajaingia kwenye vifungu halisi vinavyosubiriwa!

  UPDATES:
  Naam Hoja ya kwanza ndio inaelekea ukingoni kuna dalili za jaji kuitupa nje! Pamoja sanaaaa!

  HOJA zenyewe ni hizi:
  1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
  2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
  3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
  4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
  5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)


  - Hoja ya kwanza imetupwaaaaaaa!

  - Hoja pili inaendelea na kunadalili za kutupwa nje kwani jaji tayari keshasema hazikutumiwa ila lilikuwa kama ombi tu baada ya kuona za tume zipo slow! Bado anaendelea kufafanua juu ya hoja hiyo!

  - Shtaka la 4 la laptop binafsi limetupwa mbali. Bado moja na la mwisho la Idadi kubwa ya watu kituo cha kuhesabia kura

  UPDATES

  Hoja zote tano zilizo wasilishwa mbele ya mahakama zimetupwa na jaji amemtangaza Ndugu Mnyika kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo, na kumtaka mlalamikaji hawa Ng'umbi kulipa gharama zote za kesi hii!

  Tumeshindaaaaaaaaaaaaaaa samahani kwafuraha nimeshindwa kuwajuza mwishoooooo!
  Pipooooooooozi Powaaaaaaaaaaaaa!
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nashukuru upo eneo la tukio na umeanzisha uzi, uendelee kutujuza sisis tulio mashenzini ambao kwetu JF ni kila kitu.
   
 3. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Thanks sana kaka endelea kutupa matokeo nn kinaendelea hapo!
   
 4. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Asante kwa updates mkuu. Endelea kutujuza tunafuatilia hapahapa mkekani.
   
 5. s

  sanjo JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Tunasubiri updates za kila wakati mkuu.
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Haahaa ondoa shaka mkuu pamoja sana!
   
 7. K

  KWELI TUPU Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini hukumu imehamishiwa mahakama nyingine? hepu turushie hilo kinagaubaga!
   
 8. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ni mahakama gani mkuu ndo niko njiani
   
 9. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kwa sababu CCM walitaka kuvuruga hukumu.
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Mahakama kuu Tz nyuma ya BOT na Wizara ya Mambo ya Kigeni
   
 11. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  UPENDO HILLARY MSUYA (Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania)  *Jaji No. 40 (J.40) kulingana na nafasi ya uteuzi wake (Seniority) kwa Majaji Mahakama Kuu ya Tanzania waliopo sasa (bila kumjumuisha Jaji Kiongozi FAKIHI ABDALLAH RHENO JUNDU)

  *KANDA/Kituo cha Kazi: DAR ES SALAAM (Kama ilivyohakikiwa tarehe ya April 5, 2012. Kituo hiki cha kazi na pia namba ya Jaji huyu ki-mpangalio kwa uteuzi wake, vyaweza kubadilika pasipo sisi kuwa na taarifa. Tafadhali fanya uhakiki binafsi. Hatutawajibika kwa kutohakiki kwako huko katika jambo hilo na mengineo yaliyoandikwa humu)

  *Maamuzi ya Mh. Jaji UPENDO MSUYA yanapatikana katika Mahakama Kuu ya Tanzania; Mahakama ya Rufaa ya Tanzania (hasa yanapokatiwa Rufaa hapo); machapisho ya Sheria, maktaba za wanasheria na pia katika blog ya Case Lawyer
   
 12. G

  Gegwaz Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naam,endelea kutujuza kaka!!
   
 13. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Tunakutegemea Kamanda na hata hivyo usisahau picha angalau!

  Kila la Kheri Chama makini kwa wanainchi wake!
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kaka yericko tupo pamoja,unakumbuka jina hili lakini? CHINDWEWE
   
 15. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbona naona kama uzi huu umepotea na baadhi ya post hazionekani!!!!
   
 16. m

  maswitule JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,385
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa nchi hii chochote chaweza kutokea hata kile ambacho macho ya binadamu hayawezi tegemea eti. Tunasubiri updates toka kwenu mlioko karibu.
   
 17. NDAMANDOO

  NDAMANDOO JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 250
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  tupe ma-News! kwa sasa nini kinaendelea?
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,389
  Likes Received: 19,674
  Trophy Points: 280
  usizime simu ila iweke silence kwani itakapoita ndio utawaju magamba ni kina nani
   
 19. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Walishiriki dhambi ya kumzuia nakumpoka ushindi mwaka 2005 mungu akampa uvumilivu na subira. Akajenga sana hamasa kubwa kwa vijana kupenda siasa na kujitoa kugombea nafasi kubwa kama Ubunge, Vijana wakaanza kufikiria mageuzi na mapinduzi ya mifumo ndani na nje ya chama tawala. Mwaka 2010 wananchi kwa wingi wa ajabu na kwa kishindo wakampa ridhaa ya kuwatumikia na kuwa msemaji wao. Wanajaribu tena kumpoka ushindi kwa mamlaka zao walizo zitengeneza wao na wanadai ni Huru na Haki ila maamuzi wanayaingiliwa na kuwahadaa majaji. Mungu yu mwema atasimama na wengi atasimama na wenye haki ndani na nje ya Mahakama

  Leo furaha ya Ushindi na mageuzi ya Kura itapatikana, Leo furaha ya Ushindi na mageuzi yaweza kuporwa ila hakika wakifanya hivyo watakuwa wanajenga hamasa na ushawishi mkubwa zaidi kwa watu kuunga mkono mageuzi.
   
 20. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duuuuuh umempa angalizo zuri kweli.
   
Loading...