Mnyika ashinda kesi dhidi yake; Hawa Nghumbi atakiwa kulipa gharama za kesi!

Mbona maendeleo ya updates yamepotea? kazi zimesimama tunasubiri akili na mawazo yetu yako huko kwa sasa mkuu.
 
Kumtoa Mnyika Ubungo kwa hila ni kumkaribisha Dr.Slaa a.k.a dokta wa ukweli kumwaga sumu Ubungo. Magamba watapoteza zaidi ya kuvuna katika hili. Kwanza tutashuhudia vita ya nani agombee kwa tiketi ya gambaz halafu baadaye tutaona CDM itarudi mjengoni.

Mliopo korti rum, twambieni nini chaendelea
Hivi kama Mnyika akishindwa nani atakuwa amemtoa kwenye ubunge?
 
Pamoja na haraka zetu za kataka kupata update na Matokeo tumpe nafasi muhabarishi wetu kwani Kazi anayoifanya ni Ngumu ikizingatia wamepiga marufuku vyombo vya habari kutoa live update yeye anatumia cmu na lazima acheki situation ili aweze Kitupa information
 
Hali ya mambo ni nzuri watu hawana munkari kama ilivyotarajiwa hasa wale wa Chadema ndio wengi na wanaonyesha wana matumaini ya Ushindi,

Hukumui haijaanza kusomwa tunaelezwa itaanza mida ya saa 3 hivi,

Polisi kwa mida hii sio wengi sana kwa hesabu hawafiki 50. Kwa ujumla hali ni ya amani kabisa!

Tutawajuza hatua kwa hatua moja kwa moja toka ukumbini!

Updates:

- Basi aina ya coaster lililobeba mashabiki wa chadema ndio linaingia huku likishangiliwa na watu kwa alama ya vidole viwili alimaarufu Amani na Upendo!

- Naaaaam vijana wakazi (FFU) ndio wanaingia kwenye eneo la tukio wakiwa wamevalia kikazi yani kama Baghdad lakini wapo kwa usalama tu hakuna dalili ya vurugu yoyote hali ni yaamani tu!

- Kuna mabishano ya hapa na pale kati ya wananchi na wahudumu wa mahakama, watu wanalalamika kuwa mbona mda unakwenda na hawaruhusiwi kuingia mahakamani! Lakini wamefanikiwa kuwasihii na wananchi wametuliza munkali

- Tunaendelea kusubiri mda ufike tuanze kufuatilia kesi hii!

- Naaaaam tumeshaingia ukumbini tayari kuanza usikilizaji wa kesi hii uendelee! Tumeambiwa tuzime simu lakini MIMI sitazima mwanzo mwisho!

- Tunasubiri jaji aingie na jopo la mawakili wa pande zote wapo tayari!

UPDATES:
Kuna kichekesho kimejitokeza hapa, yani wakati wakuingia ukumbini kuna mbinu iliyotumika na mashabiki wa CDM kuwabana mlangoni wale wa Magamba na wakashindwa kupata siti kilichofuata ni afande kuwatoa nje, wakati wakitolewa nje kuna kuna mwanachadema mashuhuri akaingia ukumbini afande akataka kumuunganisha na wanachadema kutoka nje, unaambiwa ukumbi umelipuka na kusema huyo siti ipoo!

Naaaaaaaaaaam Mh Mnyika ndio anaingia ukumbini anashangiliwa kwa makofi na Pipooooooozi Pawaaaaaaaaaaaaaa!

Updates:
Wakili wa Mnyika ndugu Mbogolo ndio anaingia anasalimiana na mnyika waapiga picha wanaendelea kupiga picha!
Sasa kilichobaki ni kumsubiri jaji tu aingie ukumbini!

Updates:
Jambo la kufurahisha ktk kesi hii nikuwa Mh Mnyika na Hawa Ng'umbi wamekaa pamoja na wanapiga stori kweli, hata alipotokea afisa usalama akataka kuwatenganisha mnyika amemwambia haina tatizo watu pipoooooooooooz!

UPDATES:

M/Kiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe aka Sauti ya Zege ndio anaingia anashangiliwa ile mbaya pipooooooozi


UPDATES: Mpaka dakika hii saa nne kamili bado Jaji haja ingia ukumbini, tunaendelea kumsubiri!

UPDATES:
Naaaam jaji ameingia na hukumu inaanza rasmi,

Jaji anaomba radhi kuwa ataisoma hukumu kwa lugha ya kitumwa! Twendeleeee!

Updates:
Jaji anaendelea na mapitio ya mwenendo wa kesi nzima tangu ilipoanza na mpaka ilipo, kimsingi ameanzia kwenye historia ya kampeni,uchaguzi, uhesabuji kura na utangazwaji wa mshindi, sasa anaingia kwenye malalamiko makuu ya mlalamikaji,

Vuteni subira naripoti kwa kificho maana tumeambiwa tuzime simu na kamera zote za wanahabari!

mwenzangu asante enelea kutwambia ila take care na hako kasim hahahaha
 
Ukitaka kufuatilia vizuri we usiangaike na hizi comment za wengine wanaotoka nje ya mada kabisa maana anayeripoti habari hii ni mmoja tu itakuwa jambo la muhimu kama tutakuwa tunamfuatilia yeye kwenye updates zake na si kuanzisha porojo zisizo na maana.
 
Yaani nnilipo hapa nikiguswa tu nalipuka kama petrol vile na kadri muda unavyokwenda hasira zinazidi!mkuu update unatuacha huku preshaaaaaaaa!
 
Mbona maendeleo ya updates yamepotea? kazi zimesimama tunasubiri akili na mawazo yetu yako huko kwa sasa mkuu.
Mkuu hukumu inasomwa kwa kizungu hivyo jamaa inabidi atafasiri kwenda kiswahili huku akiwa mafichoni hapo mahakamani. Tumpe nafasi hawezi kuwa kasi kama vile ingekuwa inasomwa kiswahili na yeye hakujificha.
 
Wakuu tukumbushane basi, hoja za walalamikaji zilikuwa ngapi..?

Kuna hatari Yericko ameamuriwa kuzima simu.
Kama yuko hai atupe update hoja baada ya hoja.
 
Hivi hii CCM inavyoacha mambo nyeti kama haya na yanayomgusa mtu wa hali ya chini ya ripotiwe kwakiswahili wamejitahidi vipi kuwapa hao watu wa chini uwezo wa kuielewa hii lugha?
 
Tuheshimu maamuzi yoyote ya mahakama tuheshimu uhuru wa mahakama.
Samahani wadau nilipost hapa nikimjibu Ritz kuheshimu maamuzi ya mahakama, nikadokeza kuwa kesi ya Mhe Lema inaanza kusikilizwa 1st June 2012 lakini kwa ukweli hizo sio habari za kweli!!! Nilisikiliza habairi hizi kwenye radio moja sikumbuki ni ipi hapa Arusha ikitaja hizo tarehe, nikapost bila kuchunguza!! Naomba samahani kwa usumbufu uliowapata wadau waliosoma habari hizi, kiukweli ni kwamba tarehe maalum ya kusikiliza hiyo kesi haija pangwa. Nawaomba radhi hasa Ritz!!!

 
Anajificha nini kwani ni jamaa wa magamba? basi kama ni wa magamba lazima ajifiche kwani naamini hataweza kutafasiri neno hadi neno!
 
Back
Top Bottom