Mnyika apanda daladala!

Mnyika apanda daladala!

Mnyika panda mwana punda kama Bwana Yesu alipoingia Yerusalem kwa shangwe siku ile ya mitende na Last supper
 
Huyo anazuga tu,hana lolote! Hapo mnashangaa nini,kaamua mwenyewe! Angeuza kabisa gari lake na aache kuchukua posho.Wanasiasa wa bongo ni mafisi tu,njaa inawasumbua!hawa wanafaa kupigwa mawe popote wapitapo,bungeni vita ya kijinga,vita ya matumbo yao na hawana lolote zaidi ya kujitafutia umaarufu.Eti ndani ya daladala, pambafu!

Naona anafanya vizuri sababu haoni sababu ya kwenda na private car wakati maswahiba wake wote wako kwenye daladala. Mnajua ubunge sio kuwa mbali na watu wako. Hii kwa mnyika ni kama bajeti pia sababu asiporudi bungeni akiba yake ataitumia kwa amani kuliko kuanza kutumia matumizi makubwa kwasasa wakati akili ina mambo mengi ya kufanya
 
Mnyika amekuwa akionesha tabia kadhaa ambazo kimsingi inawapasa viongozi wote waige kwa kuwa ni tabia za kiungozi. Kwanza Mnyika amekuwa hana tabia za kujitenga na jamii na kujifanya yeye ni mtu wa daraja nyingine kama wanavyopenda kufanya viongozi wengine. Amekuwa akichanganyika na kushirikiana na wananchi wa level zote bila kujali hali zao kimaisha na kijamii.Tofauti ya Mnyika na wanajamii wengine si nyengine bali ni hoja zake anazojenga akiwa katikati ya wanajamii wengine ;Hili ndilo jambo pekee linaloweza kumfanya mtu akagundua kuwa huyu ni kiongozi.


Katika uchaguzi wa 2010, Ijapokuwa mimi sikuwa mwana CHADEMA, ila nilivutiwa sana na staili aliyokuwa anatumia Mnyika katika kampeni zake.Mnyika alikuwa anawaomba wanajamii wamchangie ili aweze kushinda na sio yeye aliyekuwa akitoa hela kwa jamii ili achaguliwe (rushwa).Huu ulikuwa ni utaratibu mwengine ambao kila kiongozi angepaswa kuufuata. Nasema hivyo kwa sababu, ikiwa mtu ni mgonjwa, yeye ndio anatakiwa amsaidie daktari nauli ili afike nyumbani kwake aweze kumtibu na sio daktari ampe hela mgonjwa ili mgonjwa akubali kutibiwa.Ukimwona daktari anampa mgonjwa hela ili eti mgonjwa akubali kutibiwa na daktari huyo; basi ujue daktari huyo pengine ana shida na damu ya mtu.Kwa kuwa kiongozi ni kwa ajili ya kutatua matatizo ya watu; watu ndio hutakiwa wawezeshe zoezi la kupatikana kiongozi huyo na si kinyume chake.Mnyika alipatikana kwa njia hiyo.Kwa hiyo tabia ya Mnyika ya sasa (tabia ya kiuongozi) ni kitu kilichokuwa kinatarajiwa.Binafsi nataraji Mnyika atakuwa ni mbunge na kiongozi wa kuigwa Tanzania kulingana na mazingira na njia zilizompa uongozi.
 
Huyo anazuga tu,hana lolote! Hapo mnashangaa nini,kaamua mwenyewe! Angeuza kabisa gari lake na aache kuchukua posho.Wanasiasa wa bongo ni mafisi tu,njaa inawasumbua!hawa wanafaa kupigwa mawe popote wapitapo,bungeni vita ya kijinga,vita ya matumbo yao na hawana lolote zaidi ya kujitafutia umaarufu.Eti ndani ya daladala, pambafu!

images


Hata huyu anaigiza...si ndiyo!? Au undhani huyu hapati posho...acha kuropoka ndugu!!
 
Hata kama Mnyika amepanda siku moja hilo daladala bado ni mfano wa kuigwa coz

1. Amesave mafuta/pesa ambayo atayatumia kwa manufaa mengine

2. Amepunguza foleni kwa kuacha gari lake home

3. Amepunguza uchafuzi wa mazingira unaotokana na moshi wa magari

HONGERA MNYIKA MFANO WA KUIGWA.......................
 
Mkuu huoni kama wanasiasa walioshika hatamu ya nchi ndio wanapaswa kupata hizo adhabu ulizoziainisha?
Maana wao ndio walio na dhamana na hatma ya taifa kwa kuwa kama ni jembe basi wao wameshika mpini na.wengineo huku tumeshika makali.

Huyo anazuga tu,hana lolote! Hapo mnashangaa nini,kaamua mwenyewe! Angeuza kabisa gari lake na aache kuchukua posho.Wanasiasa wa bongo ni mafisi tu,njaa inawasumbua!hawa wanafaa kupigwa mawe popote wapitapo,bungeni vita ya kijinga,vita ya matumbo yao na hawana lolote zaidi ya kujitafutia umaarufu.Eti ndani ya daladala, pambafu!
 
Kuna mmoja alioneshwa kapanda MTUMBWI mkasema anaigiza,, huyu kapanda dala dala mnamtetea......DOUBLE STANDARDS!!!! hamna lolote.
 
..dogo namkubali sana,nilikutana nae kariakoo msimbazi anachapa lapa bila wasiwasi...
 
Vitz mafuta 20,000 .....Daladala 500....uamuzi sahihi kwani David Cameron mbona hamsemi anataka sifa au sababu ....acheni wivu wa kike
 
What is so special? Mimi sioni cha ajabu kwa mtu upanda daladala. Au Mnyika hakuwahi kupanda daladala maishani mwake?
 
nyerere.jpg


Huyu hapa Mzee wangu niliyependezwa naye sana. Leo hii anaibuka mchumia tumbo mmoja na kutuambia tuongezewe gharama za mafuta kwa 50shillings ili tupate visima ilhali serikali ina magari ya kifahari yenye thamani ya visima 50 kila moja na kazi yake ni kupeleka watoto wao shule.

Ipo siku hii nchi, nyie subirini.
 
.ni moja kati ya njia ya kuongeza umaarufu...
 
Back
Top Bottom