Mnyika aongea na waandishi ngome kuu ya UKAWA, awajibu NEC

lowasa ni shidaaah...sisiemu wamechukia sana lowasa kuhamiaa UKAWA...lowasa anapendwaa..asante sana mbeyaa..asante mtwara..
 
Hahahahaha, mnaonesha ni vipi msivyoaminiana.

Ikiwa Mbowe kanunuliwa siwashangai kuwa waoga namna hiyo.

Lindeni msije na sababu kuwa mmeibiwa. Kama mlivyolinda kura Kalenga na Chalinze, mkakaa kimya.

#HapaKaziTu

namshangaa sana lowasa,sijui nini kawapaa watu wa kusini,huku ni baba lowasa....
 
Kama tulitoka bungeni ili kudai katiba ya wananchi, tulishindwaje kususia UCHAGUZI ili iundwe TUME HURU?
Wale kina CHIZI wako wapi waseme mbinu walizokuwa wakituibia kura?
 
Binafsi naona kama vile uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa na uwazia kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na haguzi zilizopita. Vijana tusibaki vituoni maana vurugu zikianza tutakuwa matatizoni. Nawaomba UKAWA waweke mawakala makini watakao simamia ukweli kuliko kuwahamasisha vijana kutoa sadaka ya maisha yao. Sote tunashauku na matokeo hivyo tutakuwa tunafutilia tukiwa nyumbani.
 
Mi we unavyonichefua yaani umekuja juuu kama moto wa kifuuu ukumbuke tulikesha pale Loyola kukufanikisha upate ubunge maskin mnyika ulikuwa hujui hats kuvaaa Sera ilikuwa ntaleta maji ubungo mpaka Leo maji hakuna zaidi umeenda bungeni kujifunza kuvaa suti ukatusahau tuliokesha wote pale Loyola uko kibamba usipte ntafurahi kweli kwa watu jeuri kama wewe


Wewe ndiye jeuri.

Mbunge kazi yake ni kushawishi chombo husika kwa ajili ya kutatua kero ya wananchi wake. Hivyo tatizo la maji maeneo ya jimbo la Ubungo yanajulikana. Si kwamba yeye ataenda kuchimba mfereji na kuweka mabomba, ingelikuwa ipo ndani ya uwezo wake sidhani kama angeshindwa. hapa tuilaumu Serikali na Wizara ya maji kwa kushindwa kutatua kero ya maji katika eneo hilo na ikiwa bomba linapita maeneo hayo.


=======================================================================================================
Bonyeza hapa, wenyewe CCM wanakiri: https://plus.google.com/109826525912620678114/posts/eBaNmeq13VQ


Eliya Mbonea
Limeshirikiwa hadharani - 20 Apr 2015

KINANA: MAJI SAFI BADO NI TATIZO
*CCM yakiri ugumu, yapanga kumaliza tatizo.

ARUSHA
TAKRIBANI Dola za Marekani Milioni 300 zinapelekwa Wizara ya Maji kila Mwaka, pamoja na kazi nyingine fedha hizo pia hutatua tatizo sugu la upatikanaji wa maji safi nchini.

Pamoja na Serikali kutenga fedha hizo nyingi bado upatikanaji wa maji vijijini, wilayani na mikoani umeendelea kuwa sawa na mfupa mgumu usiotaka kuvunjika.

Ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya 2010 -2015 ya Chama cha Mapinduzi (CCM), iliyoahidi kutatua tatizo la maji ili kuiwezesha jamii ipate maji maeneo ya vijijini na mijini ni kama imeonekana kukwama.

Hata hivyo ujio wa Ilani ya uchaguzi ya 2015-2020 eneo utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji safi nchini linatajwa kupewa msukumu wa ziada na Chama hicho tawala.

Katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amekutana na tatizo la ukosefu wa maji kwenye mikoa yote mitatu.

Katika mikoa hiyo alikutana na malalamiko ya wananchi kuhusu adha za kuyafuata maji mbali au usiku hasa kwa wanawake ambao baadhi hujikuta katika hatari ya kubakwa.

Lakini pamoja na changamoto hiyo kwa wananchi wa majimbo mengine, wananchi wa Kijiji cha Shimbumbu Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha wao wanalazimika kubadilishana na mawe ili wapate maji safi.

Akizungumzia tatizo la maji Kinana anakiri tatizo ukubwa wa tatizo hilo katika maeneo mengi nchini ambapo anasema CCM kitahakikisha kinaendelea kuikumbusha Serikali kukamilisha miradi ya maji sanjari na kupeleka fedha kwa wakati kwenye miradi ikiwamo ya maji.

Katika Majimbo ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro tatizo la maji limeendelea na kuonekana bado ni sugu kwani baadhi ya wananchi walijitokeza kumpokea kwa ndoo za maji huku wengine wakifunga barabara kwa lengo la kuomba wapewe taarifa maji yatawafikia lini.

Akizungumzia kwa kina tatizo la maji Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa Kituo cha Redio 5 wakati wa mahojiano maalumu anakiri wazi Ilani ya uchaguzi katika eneo hilo la maji imefanya vibaya.

Anasema katika eneo la maji wamefanya vibaya japokuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo miradi yake ya maji imefanya vizuri ukiwamo ule wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

“Hali ya upatikanaji maji bado ni tatizo kubwa sana, kama kuna tatizo tumeshindwa kwenye Ilani ya uchaguzi basi ni eneo la maji, kwa hili tunakiri kabisa,”anasema Nape.

Anasema pamoja na kukwama katika eneo la maji, bado yapo mazunguko na baadhi ya wafadhili yanayolenga kuwezesha upatikanaji wa fedha za kupunguza tatizo la maji.

Anasema Tanzania na India tayari zimezungumza namna ya kuwezesha maji ya Ziwa Victoria kutoka Kahama kwenda Tabora, Nzega na Igunga Singida na hadi Dodoma.

“Kwa kweli katika hili la kukwama kwenye eneo la maji lazima nikiri kwamba kuna watu walituangusha na hawa si wengine ni Benki ya Dunia,”anasema Nape.

Kuhusu miradi iliyosababisha washindwe kusambaza maji kwa wananchi anasema, Mwaka 2009 kabla ya uchaguzi Benki ya Dunia walileta mradi wa visima kwa vijiji 10 kwa kila wilaya nchini.

Anasema wakati wa ujio wa mradi huo waliuona kama sehemu ya mafanikio katika eneo la upatikanaji wa maji nchini.

Anasema tatizo walilokumbana nalo katika miradi hiyo ni kipindi uchaguzi mkuu ulipokaribia kwa WB walisitisha miradi wanayoifadhili kwa kisingizio cha uchaguzi.

“Hii ilitutesa lakini baada ya kumaliza uchaguzi wakatuambia tuendelee nao tena. Hata hivyo sehemu nyingi ya miradi hiyo waliiwekea masharti mabovu.

“Kwanza mpaka fedha zitolewe mtakuwa mmedhalilika vya kutosha. Lakini pia asilimia 90 wanataka ifanywe na watalaamu wao.

“Matokeo mabovu ya masharti ni mradi mmoja wa maji wilayani Kongwa mkoani Dodoma, hakuna kilichofanikiwa. Na fedha zimetumika hakuna maji. Miradi iliyotuangusha ni ya fedha zilitoka
Benki ya dunia japokuwa ipo iliyofanya vizuri,” anasema Nape.

Kuhusu mpango wa kuendelea na utatuzi wa changamoto hiyo ya maji anasema CCM imejipanga kuhakikisha tatizo hilo linaondoka.

Anasema tayari Chama hicho kimeanza kutengeneza Ilani yake ya uchaguzi mjini Dodoma ambapo moja ya maelekezo makubwa waliyopewa wajumbe wa Kamati hiyo ni kuhakikisha ufumbuzi wa tatizo la maji unapatikana.

“Ilani ya uchaguzi inaendelea kutengenezwa Dodoma wajumbe wanaendelea na vikao, moja ya maelekezo waliyopewa ni kuhakikisha tatizo la maji linatatuliwa na kwisha kabisa,” anasema Nape.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Mwanga Professa Jumanne Maghembe akizungumzia upatikanaji wa maji nchini, anakiri kuwa bado ni tatizo kubwa.

Waziri Maghembe anasema Mwaka 2013 Serikali ilianza utekelezaji wa tatizo la maji kwa nguvu zaidi ikiwa na asilimia 40 huku lengo lake likiwa ni kufikia asilimia 75.

“Hadi kufikia mwakani lengo letu ni kufikia asilimia 90. Kwa upande wa mpango wa Taifa wa Mwaka 2025 ni kufikia asilimia 99.9 na adhani kwa wakati huo tutakuwa tumemaliza sehemu kubwa ya tatizo la maji nchini,” anasema Prof Maghembe

Anasema pamoja na kuwapo kwa mpango wa Taifa wa 2025 bado malengo yanawaelekeza hadi ifikapo Mwaka 2017 asilimia 90 watakuwa na maji safi na hivyo watabakia watu wachache maeneo ya vijiji.

“Kwa hiyo CCM inaposema hili ni jambo gumu na linasumbua ni kweli hii ni kutokana na sababu mbili kwanza watu wanasumbuka sana na tatizo la maji. Lakini jambo la pili ni kwamba miradi hii ya maji ni ghali sana.

“Angalia mfano bajeti yetu Wizara ya Maji kwa mwaka ni takribani Dola za Marekani Milioni 300 kwa hiyo kwa fedha hizi bado huwezi kusema ni fedha kidogo, hizi ni fedha nyingi.

“Lakini tatizo ni kubwa sana, ila kwa mipango tuliyonayo hadi kufikia mwakani tutakuwa tumelifanyia kazi kwa asilimia 74 kwa upande wa vijijini na upande wa mijini itakuwa asilimia 95. Ni jambo gumu lakini tumelivulia viatu tunalifanyia kazi kwa nguvu sana,” anasema Prof. Maghembe.

Pamoja na majimbo yote yaliyotembelewa na Kinana katika ziara yake kuwa na tatizo la maji kwa kiasi kikubwa, Mbunge Same Magharibi Dk. David Mathayo David anaiomba Serikali kupeleka fedha za maendeleo kwa wakati.

“Ninaiomba Serikali inapopanga bajeti na kupitisha fedha kwenda serikali za mitaa au Serikali Kuu izitoe kwa wakati ili zifanye shughuli za maendeleo kwa wakati.

“Kama fedha zinazopangwa kwenye bajeti ya miradi ya maendeleo ikiwamo miradi ya maji ambalo ndio limekuwa tatizo sugu hazitatolewa kabisa maana yake bajeti iliyotengwa na serikali haina maana kwa wananchi.

“Tunakuomba Katibu Mkuu utusaidie kusukuma hili katika wizara na ofisi zinazohusika ili fedha zifike Halmashauri kwa wakati na miradi ikiwamo ya maji iweze kutekelezwa,”anasema Mbunge Mathayo na kufafanua:

“Hivi sasa tumebakiza miezi mwili kuingia kwenye bajeti nyingine, kuna maeneo mengine fedha zilizoletwa ni asilimia 12 hadi 40 ya
fedha walizopangiwa,”anasema.

Mwisho. 
 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imebanwa mbavu ikitakiwa kutoa hadharani Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mujibu wa uandikishaji wa wapigakura ulivyofanyika nchi nzima.

Sambamba na kibano hicho mbele ya waandishi wa habari jana, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilirudia msimamo wake wa kuyatangaza matokeo ya urais kabla ya Tume hiyo kwa kuwa kura zinahesabiwa vituoni na matokeo kubandikwa kabla ya kuwasilishwa kituo kikuu cha tume kwa ajili ya majumuisho.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika alisema kwamba chama hicho ambacho safari hii kinashirikiana na vyama vingine vitatu chini ya muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kimeshaamua kutozembea kwa namna yoyote ile kuhusu matokeo ya uchaguzi mwaka huu.

"Mabere Marando alishasema kuwa mwaka huu tutatangaza wenyewe matokeo kabla ya Tume kwa kuyajumlisha kutoka katika vituo vya kupigia kura nchi nzima, msimamo wetu bado ni hai tutatangaza wenyewe hata kama watasema ni uchochezi," amesema.
Marando ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na wakili maarufu wa Mahakama Kuu nchini, alitoa kauli hiyo iliyonukuliwa na gazeti la MAWIO, wakati akielezea maandalizi ya UKAWA katika kudhibiti uchakachuaji wa matokeo.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, hakuna haki ya kuhoji matokeo ya urais wakati wa uchaguzi mkuu. Haki hii imekuwa moja ya madai ya vyama vya upinzani nchini kwa muda mrefu.

Mnyika ambaye alikuwa mbunge wa Ubungo, safari hii akigombea jimbo jipya la Kibamba lililochomolewa ndani ya Ubungo, alitoa uzoefu wa jimboni kwake ambako mwaka 2010, alitangaza matokeo ya kura zake kabla ya Tume baada ya kuona mpango wa kumuibia ushindi wake.

"Kutangaza matokeo kabla ya tume ndio jambo lililonisaidia kutoporwa ushindi wangu 2010. Kile kilichotuokoa Loyola (eneo la kutangazia matokeo ya Ubungo) ni sisi kutangaza matokeo kwa wananchi na kuishinikiza tume iyatangaze pia," alisema.
Msimamo huo unasisitizwa na CHADEMA wakati tayari Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva ameshasema watatangaza matokeo ya urais ndani ya siku tatu (saa 72) na utaratibu utakuwa kura kuhesabiwa kituoni, matokeo yake kubandikwa kituoni na nakala itaskaniwa na kupelekwa kituo kikuu cha Tume.

"Hakutakuwa na wizi wa kura katika uchaguzi wa mwaka huu. Hao wenye wasiwasi kwamba kura zao zitaibiwa kama wanajua mianya ya wizi wa kura waje walete taarifa na tume itatumia mamlaka yake kuzima mianya yote, si kwa zege tu bali hata kwa kutumia nondo," alisema Jaji Lubuva.

Jaji Lubuva amekuwa akisema kwamba safari hii kumewekwa utaratibu wa kiteknolojia usiotia shaka wa kuzidhibiti kura dhidi ya uwezekano wa kuchakachuliwa na kwamba wamedhamiria kutangaza matokeo vituoni hata ya urais ili kuondoa hofu na kuwawezesha wananchi kurudi kwenye shughuli za ujenzi wa taifa.

Mnyika katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika eneo la Ngome ambako ndiko makao makuu ya UKAWA kwa ajili ya uchaguzi, alisema wakati umefika Tume itoe orodha ya wapigakura na kujiandaa kuondoa hitilafu zitakazobainika.

"NEC imetangaza jana wapiga kura wote ni milioni 23.7 lakini maelezo yao wanadai idadi kamili itafahamika kadri muda na uhakiki unavyoendelea. Huu ni mkanganyiko, tunatoa wito watoe rasmi orodha ya wapiga kura kwa vyama vya siasa," alisema.

Alisema panahitajika kuundwa tume shirikishi inayohusisha vyama vyote ambayo itakagua orodha ya wapiga kura na kuona kama kuna utata wowote ili utatuliwe.

Mnyika alieleza kuwa uandikishaji kwa mfumo mpya wa kielektroniki (BVR) na hata uhakiki wa majina umetawaliwa na utata na "inaonekana tayari tume inalo daftari lake ambalo vyama kama wadau wa kwanza wa uchaguzi huo hawana mpaka sasa."

Tume imetangaza kwamba uchaguzi huu utakuwa na vituo 72,000 natayari vifaa vya uchaguzi vimewasili nchini, zikiwemo karatasi za mfano huku Jaji Lubuva akisema karatasi halisi zitaletwa nchini wiki moja kabla ya Oktoba 25 na kudhibitiwa na Tume yenyewe kwa ajili ya usalama.

Chanzo Mpekuzi blog
 
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kinapenda kuwapa taarifa wananchi wote kuwa kitakuwa kikireport matokeo ya URAIS yatakayobandikwa kila kituo nchi nzima! mtandao wa chama unaoratibiwa na kurugenzi ya uchaguzi ya chama umebainisha azima hiyo baada ya kuwapo mtandao unaotatibiwa na intelligensia ya chama.kazi iliyopo wananchi ni kuhakikisha mnashuhudia matokeo yakibandikwa kila kituo kaa mita 200 hiyo ni sheria na hakuna wa kubatilisha!

TV mbalimbali ziko kwenye mazungumzo na CHADEMA kwa ajili ya zoezi hilo muhimu kwa taifa letu.Tume isije ikatoa matokeo tofauti na yale yaliyobandikwa kituoni!

OFISI YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI-CHADEMA MAKAO MAKUU.
 
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kinapenda kuwapa taarifa wananchi wote kuwa kitakuwa kikireport matokeo ya URAIS yatakayobandikwa kila kituo nchi nzima! mtandao wa chama unaoratibiwa na kurugenzi ya uchaguzi ya chama umebainisha azima hiyo baada ya kuwapo mtandao unaotatibiwa na intelligensia ya chama.kazi iliyopo wananchi ni kuhakikisha mnashuhudia matokeo yakibandikwa kila kituo.kaa mita 200 hiyo ni sheria na hakuna wa kubatilisha! TV mbalimbali ziko kwenye mazungumzo na CHADEMA kwa ajili ya zoezi hilo muhimu kwa taifa letu.Tume isije ikatoa matokeo tofauti na yale yaliyobandikwa kituoni!
OFISI YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI-CHADEMA MAKAO MAKUU.

acheni kuwahadaa wana nchi. Hili ni taifa letu wote msijifanye mpo juu ya sheria. In short mchezo mnaucheza ni mchezo wa hatari hakikisheni pindi mtakuwa mnachimba makaburi ya watanzania muwe mnachimba na makaburi yawatu wote wanaratibu upuuzi huu. Chadema ina iteljensia mlishindwa hata ku screen Lowasa? Nasema nikijiamini tamaa iliuwa fisi na chadema sitoshanga kuona tamaa yenu ikilitumbukiza taifa kwenye machafuko. Ccm walinde kura mita 200, chadema wafanye hvyo kila chama kikusanye watu nini kitatokea? Nilazima Mbowe na tm yako mjuwe kabla watanzania hawajadhurika kwa ujinga wenu wa tamaa nyie muwe wakwanza kudhurika na Mungu asiwasamehe kwa dhambi kubwa hii mwataka kuifanya.
 
Safiiiiii.... excellent...!!!

✌✌✌✌👏👏👏👏
 
Hamchelewi kuiga maana magufuli naye kakimbia mdahalo

Haujajua kitu kimoja, ccm hawana ubavu wa kwenda kwenye midahalo walichokua wanataka kukifanya ni kumuingiza mkenge Lowasa aende then wao dakika ya mwisho wachomoe kama walivyochomoa hivi hivyo katika mdahalo ccm wasingekuwepo
 
Ha ha ha ha Pumbavu ninyi chadema hizi taarifa mngetoa siku moja kabla ya Uchaguzi, huku:D:D Lumumba mnatuua na Presha

Mdogo wangu J.makamba-ko karibu anazeeka kwakuwaza mbinu mpya daily, yule mwingine Mwigulu amesahau hata kunyoa ndevu saizi anafanana na Okwonkwo .

Believe me wanaweza kata umeme tangu jumamos mchana mpk alhamis. Ila nimeandaa jenerator na mafuta watu wote nitatoa tv nje waangalie 24hrs
 
acheni kuwahadaa wana nchi. Hili ni taifa letu wote msijifanye mpo juu ya sheria. In short mchezo mnaucheza ni mchezo wa hatari hakikisheni pindi mtakuwa mnachimba makaburi ya watanzania muwe mnachimba na makaburi yawatu wote wanaratibu upuuzi huu. Chadema ina iteljensia mlishindwa hata ku screen Lowasa? Nasema nikijiamini tamaa iliuwa fisi na chadema sitoshanga kuona tamaa yenu ikilitumbukiza taifa kwenye machafuko. Ccm walinde kura mita 200, chadema wafanye hvyo kila chama kikusanye watu nini kitatokea? Nilazima Mbowe na tm yako mjuwe kabla watanzania hawajadhurika kwa ujinga wenu wa tamaa nyie muwe wakwanza kudhurika na Mungu asiwasamehe kwa dhambi kubwa hii mwataka kuifanya.

Don't panic. This time around, no bao la mkono. ccm mpaka mnatia huruma. Niiimuona kijana mmoja akibembeleza kuweka bendera za kijani katika kituo cha taxi. Alipokubaliwa, alifurahi utafikiri kapata bingo.
 
acheni kuwahadaa wana nchi. Hili ni taifa letu wote msijifanye mpo juu ya sheria. In short mchezo mnaucheza ni mchezo wa hatari hakikisheni pindi mtakuwa mnachimba makaburi ya watanzania muwe mnachimba na makaburi yawatu wote wanaratibu upuuzi huu. Chadema ina iteljensia mlishindwa hata ku screen Lowasa? Nasema nikijiamini tamaa iliuwa fisi na chadema sitoshanga kuona tamaa yenu ikilitumbukiza taifa kwenye machafuko. Ccm walinde kura mita 200, chadema wafanye hvyo kila chama kikusanye watu nini kitatokea? Nilazima Mbowe na tm yako mjuwe kabla watanzania hawajadhurika kwa ujinga wenu wa tamaa nyie muwe wakwanza kudhurika na Mungu asiwasamehe kwa dhambi kubwa hii mwataka kuifanya.
chadema haiwalindi ccm, na ccm haiwalindi chadema, bali wapiga kura wanakaa 200m kutoka eneo la kuhesabu kura ili kuzuia watu kutoka nje ya chumba cha kuhesabia kura kujaribu au kuingia ama kuingilia utaratibu ndani ya chumba cha kuhesabia kura.

Azma ya utekelezaji wa kanuni hii inakiumiza chama cha mapinduzi kutokana na hitoria yake kwenye chaguzi zilizopita mfano mmoja ni jimbo la segerea.

kumbuka kuwa hii ni haki ya mpiga kura sio ya chama cha siasa.
 
acheni kuwahadaa wana nchi. Hili ni taifa letu wote msijifanye mpo juu ya sheria. In short mchezo mnaucheza ni mchezo wa hatari hakikisheni pindi mtakuwa mnachimba makaburi ya watanzania muwe mnachimba na makaburi yawatu wote wanaratibu upuuzi huu. Chadema ina iteljensia mlishindwa hata ku screen Lowasa? Nasema nikijiamini tamaa iliuwa fisi na chadema sitoshanga kuona tamaa yenu ikilitumbukiza taifa kwenye machafuko. Ccm walinde kura mita 200, chadema wafanye hvyo kila chama kikusanye watu nini kitatokea? Nilazima Mbowe na tm yako mjuwe kabla watanzania hawajadhurika kwa ujinga wenu wa tamaa nyie muwe wakwanza kudhurika na Mungu asiwasamehe kwa dhambi kubwa hii mwataka kuifanya.

Mbona unatoa povu, wanalinda kura ni Ukawa, CCM zao ziko salama. Wao wakisha piga kura watarudi nyumbani, halafu tume itawapelekea matokeo nyumbani au watangaziwa kwenye vyombo vya habari.

Sasa vurugu itatoka wapi ? haiwezekani Ukawa wavurugane wao kwa wao.
 
Back
Top Bottom