Mnyika aongea na waandishi ngome kuu ya UKAWA, awajibu NEC

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
CQJIh23VEAAyXIt.jpg

Mnyika anafanya Press Conference kutokea Ngome ya UKAWA Kawe Jijini Dar muda huu.


Mnyika:Katika Magazeti Yenu Jana mlimnukuu M/kiti wa TUME akijibu tuhuma za UKAWA juu ya mazingira ya wizi wa Kura

Mnyika: Jaji Lubuva Jana amejibu kwa wepesi tuhuma za wizi wa kura

Mnyika: Lubuva anasema ukishapiga kura rudi Nyumbani. Nawaomba vijana na wapiga kura wengine waipuuze kauli ya Jaji Lubuva!

Mnyika: Jaji Lubuva amedai yupo tayari kuziba mianya ya wizi wa kura.Nitataja mianya hiyo ili Jaji Lubuva ajibu masuala haya!

Mnyika: Matokeo ya Rais kubandikwa kituoni sio jambo jipya. Ni suala la kisheria. Nawaomba watu wasome sheria ya Uchaguzi

Mnyika: Masanduku ya kura kupelekwa kituo cha majumuisho sio jambo Jipya.

Mnyika:Lubuva anasema matokeo yatascaniwa jimboni.Hili sio jambo jipya. Mwaka 2010 matokeo yaliyoscaniwa yalikuwa tofauti na karatasi halisi

Mnyika: Jaji Lubuva aseme hadharani, ni lini wataalamu wetu wa IT wakakague na kuhakiki mfumo wa kutuma matokeo ili kuepuka goli la mkono

Mnyika: mfumo wa kujumlisha kura mwaka 2010 ulikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea uchakachuaji wa kura!

Mnyika: Jaji Lubuva amesema uhakiki umefungwa, kuna jambo kubwa limejificha.Kama hakuna uhakiki daftari limeshakuwa la kudumu!

Mnyika: Mpaka tunavyozungumza hatujakabidhiwa daftari la kudumu la wapiga kura, Takwimu zinazotolewa idadi ya wapiga kura haziaminiki!

Mnyika: Tume iseme ni kwa nini mpaka sasa hawajatoa nakala za "soft copies" kwa vyama vya siasa ili wazihakiki?Hapa bao la mkono limejificha

Mnyika: UKAWA na vyama vingine Lazima viende kuhakiki Database ya Tume Makao makuu. Kwanini Lubuva hataki sisi tuende kuhakiki?

Mnyika: Jaji Lubuva anasema ipo kamati ya IT, muulizeni hiyo kamati ya IT ya vyama vya siasa inaundwa na nani?

Mnyika: Majeshi kuandikisha namba za askari, IGP alikiri jeshi kufanya hivyo kwa baadhi ya mikoa, kuna kitu kimejificha!

Mnyika:IGP alikiri suala hili limefanyika, msemaji wa TPDF alikanusha, kauli zao zilikinzana.Tume iseme ni kwanini majeshi yaliandika namba?

Mnyika: Suala la kuhamisha watumishi wa Tume, limeamia kwa wakurugenzi baada ya Rais, kuteua mkurugenzi Mpya!

Maswali: David Radio5: Wapiga kura wa Mara ya kwanza, na wasiojua utaratibu je wanabakia wapi baada ya kupiga kura?

Mnyika: Wapiga kura, wawe makini kuhakikisha wanapiga kura Siku ya tarehe 25 Oktoba!

Mnyika: Daftari la kudumu halitolewi kwa wakati ili kuruhusu goli la mkono!

Mnyika: wapiga kura wajielekeze kuangalia majina ndani ya daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo!

Mnyika: Orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo inaandaliwa na manispaa, na daftari analopewa wakala limeandaliwa na Tume

Mnyika: Tume itoe Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva amesema atalitoa daftari Siku 4 kabla ya Uchaguzi, hapa amejichanganya!

Mnyika:Hatua ya pili ni kutoa 'permanent voter register' hili ilipaswa kutolewa mapema

Mnyika: Kuna madaftari mawili, provisional voter register, hili tulitakiwa kupewa kabla ya uhakiki wa wapiga kura, hili hatujapewa!

Mnyika: Rai yangu kwa wana UKAWA, wasikate tamaa kufuatia matamko ya mawaziri mbalimbali

Mnyika:Juu ya matumizi ya vyombo vya Serikali kujihusishanaUchaguzi, linaongozwa naraisi,Bunge limevunjwa ila baraza la mawaziri linaendelea

Mnyika: Iundwe kamati ya pamoja ya vyama vya siasa ya IT ikakague Daftari na kuliboresha ili kuzuia goli la mkono!

Mnyika: Swali la1: Tulianza kusema haya mambo mapema, waliamua kufumba masikio na macho!

Maswali:Fred kutoka Mtanzania: Kisheria mnatakiwa mpate soft copy ya Daftari baada ya Muda gani?

Maswali: Francis kutoka ATN: suala la uhakiki wa BVR hamuoni Siku zimebaki chache na kwanini msingeliibua suala hili mapema?

Mnyika: Tume iliwahi kukiri kuwa haiko huru mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, WaTZ wasikubali faster faster hii.

Mnyika: Wanapeleka huu mchakato faster faster, rai yangu tusisubiri tarehe 25 Oktoba, tuanze sasa kudhibiti goli la mkono!

Mnyika: Ndani ya nchi tunao watazamaji wasisubiri mpaka Uchaguzi uishe, waende Tume kutazama mfumo huu wa ujumlishaji wa kura

Mnyika: Nawaomba 'Waangalizi wa Uchaguzi' watoe ripoti zao mapema juu ya haya masuala!

Mnyika: Tume ya Uchaguzi sio Mali ya watu binafsi, ni tume ya Taifa letu.

Mnyika: Kijana ukishaona matokeo yamebandikwa, piga picha matokeo hayo na uyatume kwenye WhatsApp!

Mnyika: Kama kuna MTU ataniita mchochezi kwa kusema 'first time voters' wakae mita 200 kusubiria matokeo basi atangulie mahakamani,

Mnyika: First time voters, kukaa ndani ni kosa kisheria, kukaa nje si kosa kisheria, kisheria wanakaa mita 200!

Maswali: David Radio5: UKAWA mtafanya nini endapo tume haitafanya mnayosisitiza wafanye?

Mnyika: Nasisitiza BVR ni Bomu la kufungwa bao la mkono, yote tuliyosema yazingatiwe na wahusika!

Maswali: Prosper - The Guardian: Mnataka wataalamu wa IT wakakague daftari pekee, vipi kuhusu ukaguzi wa idadi ya kura zilizopigwa?

Mnyika: Kama Tume haitasikiliza haya tunayosema wanajitengenezea mazingira ya kupelekwa ICC!

Mnyika: Local monitors wa Uchaguzi wapo wachache, wanasubiria matokeo majimboni, kila mpiga kura lazim awe monitor!

Mnyika: Nje ya kituo cha kupiga kura sisi wapenda Amani, tutawalinda mawakala wetu, wasirubiniwe kupokea hongo ndani ya vituo vya Uchaguzi!

Mnyika: Marando alisema atatangaza matokeo, sasa kwa sababu anaumwa yupo hospitali Mimi Mnyika nitayatangaza.
 

Mnyika: Marando alisema atatangaza matokeo, sasa kwa sababu anaumwa yupo hospitali Mimi Mnyika nitayatangaza.

Maskini Mnyika kichwa kimeshapata moto tayari baada ya kujua uwezekano wake kurudi bungeni mdogo.Eti atatangaza matokeo yeye!!!! Yaani yeye awe mgombea ubunge,mpiga kura,na mtangaza matokeo mwenyewe!! Segregation of duties ziko wapi? Vyama haviwezi kugombea uchaguzi vyenyewe,vihesabu kura vyenyewe na kutangaza matokeo vyenyewe hakuna kitu kama hicho duniani.Marando namsamehe kwa kuwa anaumwa inawezekana alitoa tamko akiwa tayari anaumwa.Mnyika yeye naona maradhi ya kichwa yamemuanza ndio maana anaropoka tu baada ya kumpokea fisadi Lowasa.
 
kachanganyikiwa fisadi huyu wameuza chama sasa wanabwabwaja tu.

Baada ya kupiga kura tutaenda nyumbani kujiandaa kurudivkwebye mkesha wa matokeo kituoni! Muda ni kuaanzia saa 12 jioni maana najua upigaji kura mwaka huu hautaishia saa 10 kwa sababu ya wingi wa watu!

Vijana wote siku hiyo ni kuamka saa 10 asubuhi ili tuwahi kurudi kupunzika tayari kwa mkesha wa matokeo!
 
Mnyika yuko sahihi tunataka uchaguzi wa haki ili mtu akishindwa ashindwe kwa ghaki sio kuleta ujanjaujanja tu
Kipindi hiki ndio watumishi wa tume wahamishwe kipindi chote mbona hawakuhamishwa LUBUVA asitake kuibeba ccm aache watu wacheze mpira na wa kushinda ashinde kwa haki na vivyohivyo kwa atakae shindwa tume iwe huru huu ujanja wa kihuni atuutaki
 
RUCCI

Nasi Tunaomba Pia Kwa MCHANGANUO Huu Huu Mnyika Nae Pia ATUAMBIE Jinsi MCHAKATO Mzima Na MGAWANYO Wa Pesa WALIZOHONGWA Na Lowassa Na KUMUUZIA Chama Cha CHADEMA Kwa Kuanzia Mbowe, Lissu Na Yeye MNYIKA Mwenyewe Na Kama Endapo ATASHINDWA Kutoa Huo UFAFANUZI Na Sisi TUTAUTOA Hapa ILI Watanzania Waweze Kujua Kati Ya NEC Na Mnyika Na UKAWA Yake Akina Nani Ndiyo WANAFIKI Na WAONGO Wa KUTUKUKA.
 
Last edited by a moderator:
baada ya kupiga kura tutaenda nyumbani kujiandaa kurudivkwebye mkesha wa matokeo kituoni! Muda ni kuaanzia saa 12 jioni maana najua upigaji kura mwaka huu hautaishia saa 10 kwa sababu ya wingi wa watu!

Vijana wote siku hiyo ni kuamka saa 10 asubuhi ili tuwahi kurudi kupunzika tayari kwa mkesha wa matokeo!

ukosawa kabisa mkuu hongera xana wote tutakuwepo
 
Kichwa cha habari chahusika.Marando anaumwa nini,anaulinzi mkubwa kiasi gani alipo?Ikumbukwe kwamba Kamanda huyu amekuwa akiahidi kutangaza matokeo ya urais kila yatakapomfikia kutoka vyanzo vyake mbalimbali.Ahadi hiyo siyo jambo dogo na haijawai kutokea.Ukizingatia kuwa kuna chama kimeandaa goli la mkono,Je Marando aumwa kawaida tu?
 
Mi Nashangaa Mnyika Anakuja Kusema Wakati Huu Eti "tume Walikiri Kuwa Haipo Huru" Wao walichukuwa Hatua Gani Wakati Wao Ndo Wanawajibu Wa Kuunda Sheria Itakayofanya Hii Tume Iwe Huru?Haya Ndo Mambo Ambayo Siku Zote Upinzani Wakifika Kusaini Sheria Kabla Ya Kuingia Ulingoni Hawaliangalii,hawalisemi Wala Hawalikemei Mpaka Matokeo Yakitoka Ndo Unaanza Kuwasikia Oh Tumeibiwa,uchaguzi Haukuwa Huru Na Haki,mlikuwa Wapi Wakati Wa Makubaliano?
 
Kichwa cha habari chahusika.Marando anaumwa nini,anaulinzi mkubwa kiasi gani alipo?Ikumbukwe kwamba Kamanda huyu amekuwa akiahidi kutangaza matokeo ya urais kila yatakapomfikia kutoka vyanzo vyake mbalimbali.Ahadi hiyo siyo jambo dogo na haijawai kutokea.Ukizingatia kuwa kuna chama kimeandaa goli la mkono,Je Marando aumwa kawaida tu?

Mission Accomplished.
 
Mbona atapona na kushiriki uchaguzi bila shaka yeyote,msiwe na wasiwasi kwani tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu kwa ushindi ambao haujapatatokea hapa east africa.
 
Back
Top Bottom