BUSARA ZANGU
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 779
- 1,267
Pia mkuu naona kama umeonesha kwamba kuihusisha serikali za mitaa ni hiari kama unapoamua kumuhusisha Jirani ama rafiki. Lakini huoni serikali ya mitaa ina uzito zaidi ya hao uliowataja?
Huyo ni mchumia tumbo.Amekuvuta umevutika.Mwambie akuandikie na barua ya dhamana utoke mahabusu au gerezani.Look here,Afisa Mtendaji ni Mlinzi wa amani. Anaweza kisimamia hayo mambo. Huyo yupo kibiashara zaidi. Kalagabaho!Aisee, umenifumbua akili, ubarikiwe
Huyo mleta uzi roho inamuuma akiona mwenyekiti anapewa 10%!Andiko lake limelalia hapo. Hana lingine.Viongozi wa mitaa hawana mshahara hayo ndiyo Malipo Yao ya halali na siyo rushwa.
Huyo ni mchumia tumbo.Amekuvuta umevutika.Mwambie akuandikie na barua ya dhamana utoke mahabusu au gerezani.Look here,Afisa Mtendaji ni Mlinzi wa amani. Anaweza kisimamia hayo mambo.Huyo yupo kibiashara zaidi.Kalagabaho!
Umeandika kwa uelewa mkubwa sana.Atakayesoma maoni yako atamaizi ukweli.Tena ukweli mtupu.Mtu ambaye hafahamu uhalali wala historia ya sehemu eti ndiyo asimamie mauziano.Haiwezekani!Kila mtu acheze karibu na sufuria lake la ubwabwa.Ingawa kunaweza kuwa na ukweli kwenye bandiko lako lakini mimi napata uwalakini huenda mnajitafutia soko tu nyie wsnasheria maana kwa muda mrefu na niseme wengi wetu tumekuwa tukiuziana hasa viwanja kwa kupitia serikali za mitaa pasi na shaka na zaidi ya yote wale ndio wanaofahamu eneo husika na mmiliki wake kuliko kuja tu na wakili asiyejua ABC ya eneo husika
Ndio maana serikali pia inawapa uwezo serikali mfano ya kijiji kutoa Maeneo kwa muwekezaji kwa kiwango fulani kwa kuitambua utendaji kazi wake
Ushauri wako labda ungekuwa baada ya watu kuuziana kwa mtindo huo pendwa basi nyaraka zipelekwe kwa hao mawakili kwa ajili ya maboresho
Kuna kesi ipo inasema bank au taasiu ya fedha yenye leseni kutoka bank kuu ndo wanaweza kukopesha kwa riba.Nyongeza nyingine kuna watu wanakopeshana kwa riba na wanaandikishana kwa mwenyekiti. Hapo pia hakuna mkataba
Ukweli ni kwamba tuna siasa sana kwenye maamuzi yetu. Alichosema wakili ni kitu cha kuwa makini sana. Hatujui kesho yetu ni bora kuwa upande sahihi.Basi wengi wameliwa na ikija msako wa pekua pekua ya mikataba yakihalali basi wengi watakuwa hawana nyumba kihalali
Maana imekuwa mazoea kufanya mikataba hii ya kuuziana viwanja , mashamba kwenye serekali za mitaa hadi sasa imekuwa kama ndio sheria .
Lakini nauliza mbona hao wanasheria wenyewe hawakulizungumzia hili mapema ,
Maana kwa hali ilipofikia sasa ni mbali sana kwani kila mtu anajua mikataba inafanyika serekali za mitaa tu kama njia ya kwanza kuuziana na kununua,
Sasa mfano mtu ndio unataka kununua kiwanja au nyumba alafu uje na hii article mitaani humo nadhani kwanza watakushangaa sana
Uko sawa. Nilimuuliza sasa kwa wenyemikataba ya wenyeviti wanaweza kupeleka kwa mawakili ilikuisatify akachuna mpaka leo.....Ukweli ni kwamba tuna siasa sana kwenye maamuzi yetu. Alichosema wakili ni kitu cha kuwa makini sana. Hatujui kesho yetu ni bora kuwa upande sahihi.
Ngoja nitalifanyia research mkuu...nioneUko sawa. Nilimuuliza sasa kwa wenyemikataba ya wenyeviti wanaweza kupeleka kwa mawakili ilikuisatify akachuna mpaka leo.....
Katikati hapo ameandika serikali ya mtaa husaidia kumtambua muuzaji na pia kama kiwanja kina mgogoro au laah. Kwahiyo ni muhimu na hela yeyote itolewayo lazima ipate risiti halali vinginevyo ni takrima au rushwa.Na je kuifahamisha serekali za mitaa kuhusu kuuziana nilazima?