Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,880
- 2,758
asubuhi tu nimesikia habari moja redioni. dada kaolewa tatizo likawa kupata mtoto. mwisho wa siku ikajulikana mwanamke ndiye mweye tatizo. bahati nzuri mwanaume alikuwa mwelewa, akamchukulia poa. mwanamke akawa hana amani, akamwita mdogo wake toka bush na kumwomba azae na shemejiye then amwachie mtoto. binti alikataa sana ila mwisho wa siku alikubali. jamaa nae alikataa sana mwisho wa siku alikubali. mara mimba mara mtoto. jamaa akafurahi sana hadi kamnunulia shemeji gari. ikawa siku za shemeji kuondoka zimefika, ila jamaa akatia ngumu shem asiondoke. keshampenda shem kwa gharama yoyote ile hata kama ni kuua. anataka waishi wote pale au mke (dada mtu) mgumba aondoke. wazazi hawajui kinachoendelea. jamaa nae anadai anataka kuishi na aliyemzalia mtoto, na anataka kuongeza wengine. shem nae hakupenda kuharibu ndoa ya dada anataka kuondoka ila jamaa ndo keshapenda. nilijua ni muvi za kinaijeria tu kumbe haya mambo yapo. sasa yakitokea ufumbuzi unakuwaje