Ni msaada au wema gani ulimfanyia mtu ukakutokea puani ukajuta hutarudia?

Mosalah_

JF-Expert Member
Jul 10, 2018
314
720
Sitasahau kuna rafiki yangu nilipanda nae daladala akamuona mdada ana mtoto mchanga amesimama, wakati huo yeye alikua na siti amekaa, akamuomba kumsaidia mtoto yule dada yule dada akakubali.

Ila mimi nilimwambia Swahib kama umepanga kwa dhati kumsaidia huyu mdada we mpishe akae na mtoto wake, akasema oooh hamna sijui nini nini!

Haya wee mwisho wa siku aliachiwa mtoto kwenye daladala na yule dada akakimbia zake hatukujua alishukia wapi!

Jamaa alishapeleka barua kwa mdada mmoja aliekuwa shem wetu uchumba ukafa kisa huyo mtoto! Maana jamaa hakujua chakufanya zaidi ya kubaki na kale katoto mpaka leo kamekua sana na kanatuchangamsha sana kila nikiendaga kwa jamaa.

Inasikitisha na inachekesha maana jamaa alikuwa anataka kumtupa yule mtoto, na akasema kama mama yake amemuacha mimi ni nani!

Nikamuambia bro ukimtupa huyo mtoto wakwanza kukureport nitakuwa mimi ndugu yako wa damu kabisa! Kwenda polisi reception tukakutana na mdada ana nyodo balaa, nikamshauri tu ndugu yangu tumlee kijana akikua huenda akaja kututilia ubani siku tukifa tukapata angalau kukumbukwa.

Ila kiukweli nilikua namsaidia kuishauri huku namcheka sana, sisemi uongo. Ila dogo amekua sana siku hizi kanaongea kama kasuku, afya Ma-Sha-Allah na tumekapeleka nursery japo hakaelewi chochote kanaenda kufanya tu fujo na sisi baba zake kulipishwa vitu tu mitaani.

Basi bhana ndio hivyo anaitwa baba one, naitwa baba two. Shule hizo za chekechea mtoto kashajua one na two.

Ila we dada ulietukimbia na katoto hatukupi laana hata umetuletea baraka na kutufundisha majukumu, tumekua watu wazima now days Mungu akubariki sana. Na siku ukijitokeza uso wako eti kuja kumtaka huyu mtoto nadhani ndio hiyo siku utakuwa headgirl wa mortuary.

Note: Hii story siyo ya kwangu kuna sehemu nimeipata nikaipenda.
 
Kipindi nikiwa chuo kuna jamaa mmoja alinijia nikamkopesha hela ya matumizi baada ya kuishiwa boom lakini alikuwa mgumu sana kunirejeshea hadi nilipomkomalia kisawasawa. Tangu siku hiyo niliapa kutomkopesha mtu hela hata angekuwa na shida/njaa kiasi gani

 
Kipindi nikiwa chuo kuna jamaa mmoja alinijia nikamkopesha hela ya matumizi baada ya kuishiwa boom lakini alikuwa mgumu sana kunirejeshea hadi nilipomkomalia kisawasawa. Tangu siku hiyo niliapa kutomkopesha mtu hela hata angekuwa na shida/njaa kiasi gani

Pole mkuu, tena chuo bumu likikata inakuwa noma.
 
Ctasahau kuna rafiki yangu nilipanda nae daladala akamuona mdada ana mtoto mchanga amesimama wakati huo yeye alikua na siti amekaa

Akamuomba kumsaidia mtoto yule dada yule dada akakubali

Ila mimi nilimwambia Swahib kama umepanga kwa dhati kumsaidia huyu mdada we mpishe akae na mtoto wake

Akasema oooh Amna sijui nini nini

Haya wee mwisho wa cku aliachiwa mtoto kwenye daladala na yule dada akakimbia zake hatukujua alishukia wapi

Jamaa alishapeleka barua kwa mdada mmoja aliekua shem wetu uchumba ukafa kisa huyo mtoto maana jamaa hakujua chakufanya zaidi ya kubaki na kale Katoto mpaka leo kamekua sana na kanatuchangamsha sana kila nikiendaga kwa jamaa

Inasikitisha na inachekesha maana jamaa alikua anataka kumtupa yule mtoto

Na akasema kama mama yake amemuacha mimi ni nani

Nikamuambia bro ukimtupa huyo mtoto wakwanza kukureport nitakua mimi ndugu yako wa damu kabisa

Ilitokea kuenda polisi reception tukakutana na mdada ana nyodo balaaaa

Nikamshauri tu ndugu yangu tumlee kijana akikua huenda akaja kututilia ubani siku tukifa tukapata angalau kukumbukwa
Ila kiukweli nilikua namsaidia kuishauri huku namcheka sana sisemi uongo

Ila dogo amekua sana siku hizi kanaongea kama kasuku
Afya mashaAllah na tumekapeleka nursery
Japo hakaelewi chochote kanaenda kufanya tu fujo na sisi baba zake kulipishwa vitu tu mitaani


Basi bhana ndio Ivo anaitwa Baba one naitwa baba two

Shule hizo za chekechea mtoto kashajua one na two
Ila we dada ulietukimbia na Katoto hatukupi laana hata umetuletea baraka na kutufundisha majukumu tumekua watu wazima now days Mungu akubariki sana
Na siku ukijitokeza uso wako eti kuja kumtaka huyu mtoto nazani ndio hiyo siku utakua headgirl wa mortuary

Note: Hii story siyo ya kwangu kuna sehemu nimeipata nikaipenda.
Amkuwa na mawazo mngempeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatima tu.
 
Kipindi nikiwa chuo kuna jamaa mmoja alinijia nikamkopesha hela ya matumizi baada ya kuishiwa boom lakini alikuwa mgumu sana kunirejeshea hadi nilipomkomalia kisawasawa. Tangu siku hiyo niliapa kutomkopesha mtu hela hata angekuwa na shida/njaa kiasi gani

Kama ana njaa mpe chakula, ni mambo ya kupita tu.
 
Mbona ushuhuda mwingi ni wa maswala ya KUKOPESHA.. mnanipa stress kuna Jamaa wawili nimewakopesha Hela.... na Jamaa hao tangia niwakopeshe hata online siwaoni.. hata salam siku hizi hakuna.. ila uzur walisema mshahara huu watanipa. Ngoja nione
 
Kwenye swala la kukopesha ni kitu ambacho kimenifanya nijutie kukopesha watu kwakweli halafu sio mmoja yaani imefika Mahali Sasa hivi hadi nikukopeshe. Nimeku evaluate kisawasawa
Kukopesha mtu fedha ni habari nyingine hasa. Kwa kifupi usikopeshe maishani labda awe ni mtu unayemjua na kuelewana naye sana sana. Au uwe tayari kupata hasara kama hatalipa.
 
Back
Top Bottom