Mimi kwa kweli sijaiona faida ya muungano huo unaoliliwa sana. Zanzibar hasa ndio wenye faida nao zaidi lakini ndio wa kwanza kulalamikia. Kila kijiji in equivalence to Bara kina mbunge, nyadhifa nyingi katika muungano huo wazanzibar wanabebwa sana sababu za kisiasa tu ati kuimarisha muungano. Hapa Bara wazanzibar wamejitwalia ardhi kedekede na vitegauchumi lukuki vinamilikiwa na wao na hatuwasemi tunajua ni wenzetu, lakini nenda Zanzibar kama utaruhusiwa hata kuweka kibadna cha miti kuuza nyanya!!!! Bado mimi naamini usalama wetu Tanganyika ni pale tutakapoachana na Zanzibar tusipigiwe makelele hayo nao wazanzibar wote warudi kwao watuachie bara yetu, hapo ndo watajua kwamba wanafanya makosa kula na kipofu kwa kumpigapiga mikono yake kwenye sahani. Tunavumilia kuwaenzi kina Nyerere tu, Mtikila yuko sahihi saa zote na viongozi wa serikali wanakubaliana naye isipokuwa ni waoga kuchukuwa maamuzi magumu. Zanzibar haitadumu nje ya muungano, wanabwabwaja sana kwa sababu wanalindwa chini ya muungano.