Mnaotumia soda ya coke mnaona ipo sawa?

BROKE BOYS

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
13,218
39,047
Mimi sio mtumiaji wa soda ila jana nilinunua soda coca lakini nilivyoinywa niliona utofauti mkubwa sana hasa kwenye ladha na pia soda haina gas.

Leo tena nimeinywa sehem nyingine naona ladha ileile coca imebadilika sio kama ilivyokuwa zamani kiukweli soda imenishinda ina ladha mbaya sana. Hii sio coca nayoijua mimi imekua ya hovyo mpaka nikahisi labda ime expiry, kucheki date naona ipo sawa.

Kuna mabadiliko makubwa sana kwenye hii soda sijajua kwenye fanta na aina zingine. Cocacola wamechange formula yao au ni mimi tu sababu sijainywa muda mrefu??. Maana nasikia mpaka kichefuchefu soda inaladha ya ajabu.

Mnaoitumia hii soda naombeni majibu juu ya hii soda.
IMG_0701.jpg
 
Vinywaji baridi vingi siku hizi ni sumu maalumu ziliyoandaliwa kimkakati kuua taratibu watu weusi. Watu weusi hatutakiwi duniani.

"We buy poisons with our own money"--- it is poisons for sale.
 
Coke takeaway na hizi chupa za glass ladha Ni tofauti kabisa.

Hivyo hivyo Pepsi takeaway na glass ladha zake ni tofauti.

Kwahiyo ni kweli ladha imebadilika siyo kama ya zamani ila kama ni mnywaji wa kila siku huwezi kugundua
 
Na watu weupe nawao wanatumia lakini labda hapa duniani hatutakiwi watu wote mkuu sio weuc tu na weupe pia


Weweee, nani kakuambia mtu mweupe huwa anatumia vitu kama hivyo??!!, Wao wanajali sana viwango (standards) kabla bidhaa haijaingia sokoni na hasa bidhaa yenyewe ikiwa inahusiana moja kwa moja na afya za watu, huwezi kukuta vitu kama hizi Energy drinks zisizokuwa na viwango huko Ulaya, kabla vinywaji havijaingia sokoni hufanyiwa uchunguzi mkali sana ndipo ziingizwe sokoni kitu ambacho huku kwetu ni vigumu sana kufanyika kwasababu ya utaalamu wetu mdogo, Rushwa nk.

Mimi huu ni mwaka wa 6 sijanywa kinyaji chochote cha machupa na Soda.
 
Sio mtumiaji wa soda na hapohapo ulipokunywa ukaona radha ipo tofauti, sasa huo utofauti umeujuaje ikiwa sio mtumiaji? Nijibu hili swali tafadhali
 
Sio mtumiaji wa soda na hapohapo ulipokunywa ukaona radha ipo tofauti, sasa huo utofauti umeujuaje ikiwa sio mtumiaji? Nijibu hili swali tafadhali

Mtu akikwambia mimi sio mtumiaji wa daladala anamaanisha hajawai panda kabisa???.
 
Back
Top Bottom