INAUZWA USHUHUDA: Jinsi Fridge linavyofanya napiga show kali kwa Bed

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
3,945
7,945
Habari ya leo ndugu waTanzania na wote msomao mada hii. Hope you are good with your life.

Leo napenda niwape ushuhuda wa maisha yangu jinsi fridge lilivyo badilisha maisha yangu na kuongeza ufanisi wangu wa kupiga show kunako majambo.

Mimi nimepanga geto, sina mke, ila katika kuhakikisha napunguza matumizi ya home na kupata msosi wenye ladha nzuri huwa napika msosi mwenyewe, sasa changamoto nilizokutana nazo kipindi sina fridge zilikuwa nyingi sana mfano

Kutokula mlo kamili, hapa hii inatokana na uvivu wa kupika, just imagine nimetoka misele saa 3 usiku nianze kupika nyama, kisha nipike mboga majani etc, hapa kulikuwa na uvivu sana mara nyingi ningeweza kula wali + na nyama tu au kama nimechoka ningenunua soda kisha nile na wali mkavu

Kulazimika kula sana chakula kwa kuhofia kuharibika, mfano binafsi sio mpenz wa kula nyama, hivyo naweza nunua nyama nusu kg halafu ikanibi kuila yote ndani ya milo miwili tu, (hii ni hasara kiafya na kifedha pia)

Kutokula matunda, hii ilikuwa inatokea mara nyingi yani ile kufika geto na kukumbuka kuwa sijanunua matunda ilikuwa kawaida kabisa, sometimes namaliza siku 5 bila mboga majani wala matunda 💔 (hii ilipelekea kiwango cha show kushuka kwa kiasi fulani )

Kula vyakula vyenye viungo vichache, mm sipend kwenda gengeni kila siku, so mara nyingi huwa nanunua kwa jumla eg fungu la hoho, fungu la karoti etc, sasa changamoto ni kuwa ukinunua leo kesho yameshaharibika kabisa 💔 unajikuta unafika geto unatupa tu vyakula (unakula mboga ina kitunguu na nyanya tu) hii ilishusha uwezo wangu pia

Sasa bana Mungu si Feisal Salum au Saido Ntibanzokiza wala Mpwayungu Village, Nikafanikiwa kupata fridge langu zuri kabisa toka KENSHOP kwa bei nzuri kabisa tena na ofa kibao kama vile Pasi bure, Stand bure, usafiri bure pamoja na Jagi la kuchemshia maji (Just imagine), hili lilibadili kabisa maisha yangu ya kula na pia kusababisha nikawa natumia pesa ndogo zaidi kwenye msosi na Kikubwa zaidi naona kiwango changu cha kitandani kinazidi kuwa kikubwa hadi nafurahia, kwa sababu ya kuweza kula mlo kamili na matunda kila siku tena vizuri kabisa, mfano wa badiliko yaliyoletwa na fridge kwangu ni kama yafuatayo
Picsart_23-06-08_21-06-50-596.jpg

Bei za fridge toka KENSHOP, Hakika zipo chini

Matunda nanunua ya jumla, natengeneza juice naweka kwa fridge, kila asubuhi kabla ya kusepa lazima nipate glass moja ya juice ya tikiti yenye tangawizi na asali kwa mbali, (hii ipo kwa fridge, natengeneza mara moja kwa week naweka kwa fridge)

Kila jioni kabla ya kulala nakunywa juice ya mchanganyiko wa karanga, ndizi asali na maziwa, hii naitengeneza mara moja kwa week kisha naweka kwa fridge simple tu jioni napata moja

Ulaji wa mboga majani umekuwa bora sana, nanunua mboga majani mafungu mawili, napika kisha naiweka kwa fridge, hii nakuja nakula kila muda wa mlo (huwa siipash hii ili kutopunguza viinilishe)

Nakula samaki fresh, hapa simple tu kama kwenye nyama na vitu ka hivo, nanunua kg moja ya samaki, kisha inachemshwa simple tu na kisha kuwekwa kwa fridge, m nikuunga tu kila nikirudi, samaki wanasaidia sana kuongeza nguvu za kiume

Fridge limeniondolea uvivu wa kupika, yan saizi mm nikifika geto, nyanya ni nyingi nilishaunga nikaziweka kwa fridge, viungo vyote vipo easy kwa fridge, nyama nakuta ishachemshwa ni kuungwa tu bila mambo ya kuchemsha wala nini, naweza sema fridge limepunguza nusu ya muda niliokuwa natumia kuandaa msosi, hivyo kuongeza ufanisi wangu kazini kwa kuwa linanipa muda zaidi wa kupumzika

Matokeo ya yote hayo wakuu naona ubora na uwezo wangu kitandani unazidi kuwa mkubwa, saizi nina uwezo mkubwa sana wa kuunga bao 2, kisha napumzika dakika 10 naunga la tatu, haya ni maajabu kabisa kwangu, itoshe kusema fridge limenisaidia sana.

Nawashauri na vijana wengine ambao mnasumbuka kula mlo kamili na hivyo kufanya viwango vyenu kuwa chini, muwacheki KENSHOP mpate fridge ili muweze kula mlo kamili na kisha muweze kuongeza viwango vyenu vya bed na pia kusave sana pesa ya matumizi.

Mpaka wakati mwingine tena,
Wenu Beberu J
 
Kilichobaki sasa mkuu ni kunicheki ili upate fridge lako moja
 
Hakuna mwanaume asiye na nguvu za kiumee mkuu ...

Lipia tangazo la frige
Mkuu sasa uniungishe ili nipate pesa ya kulipia tangazo kabisa,

Btw kama taifa tujitahidi kula vizuri, matunda na mboga za majani
 
Back
Top Bottom