Mnaotafuta ajira kuweni makini na matapeli

Mnaotafuta ajira kuweni makini na matapeli

Habari wadau,

kumeibuka utapeli unaowalenga wahitimu wa vyuo, hasa ukizingatia kipindi hiki kila mtu anatafuta ajira na zimekuwa ngumu kwelikweli, hivyo matapeli hawa wamekuja na njia ya kutangazia watu kuna nafasi za kazi mahali fulani na kutoa mawasiliano yao.

Ukishawatafuta wanakuomba pesa kwa ajili ya fomu na na vitu vingine vya ajabu ajabu, kuna mtu ameombwa atume pesa ya fomu ya fire extinguisher, teh teh teh.

Kuweni makini na mtu anayeitwa ERNEST, ndivyo anavyojitambulisha na anatangaza nafasi za kazi Migodini hasa GGM, huyu ni tapeli anaanza kwa kuomba hela ya medical checkup form, na pesa zake ni zile ambazo huwezi enda polisi, 5000, 6500 akienda sana 10000.

anatumia email ya yahoo kuweni maikini.

Nawasilisha.
Kwa pesa anazoomba si ajabu kajenga kabisa
 
Toka lini medical check up za GGM zikalipiwa? Huu ni utapeli wa waziwazi kabsa... Na wanafanya hivi kwa walio mbali na maeneo yanaouzunguka mgodi... Hakuna gharama za medical check kwenye migodi yote Tanzania!!
 
Buzwagi hawakua na x-ray machine, kipindi naajiriwa ilibidi niende kulipia Hospitali ya Kahama, na kuna form pia nilijaziwa kule nimeisahau jina. GGM na Bully wako vizuri kila kitu unapata humo ndani.
 
Kabsa mkuu, sema kama huna ufahamu na hauna watu wa karbu wanaofanya kazi GGM au Bully basi lazima upigwe tu...
 
Hahahah pole my loves, yani ungepigwa 1M sijui ingekuwaje 🤩🤩🤩
Weee 1M ,nahisi ningepagawa ila kwa huu ubahili sidhani kama mtu anaweza nipiga 1m kabisa, hiyo 4500 yenyewe nilisita kutuma hadi nilipoambiwa acha ubahili utakuja kosa kazi bure pesa yenyewe ndogo,ndiyo nikatuma😀😀
 
Back
Top Bottom