Kutoka Efatha Church: Mambo muhimu ya kuzingatia mwaka huu 2024

PharaohMtakatifu

JF-Expert Member
Jul 3, 2023
659
1,074
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA MWAKA HUU 2024

Kuanzia leo Mungu hatakunyima vitamanikavyo, utakula kile kinachotamani moyo wako, hii inamaana kuwa hautakula kwa sababu ndio kilichopo, la! Bali utakula kile moyo wako unatamani.

Kuanzia leo ugonjwa wowote unaotokana na chakula au maji au matunda hautakuwa juu yako maana Bwana atakubariki. Unachokula na unachokunywa hakitasababisha magonjwa wala maumivu kwako. Mungu ataponya chakula unachokula,maji unayokunywa kwa Jina la Bwana.

Maadam umekubali kuijenga nyumba ya Bwana Mungu atakutafutia nyumba nzuri maana umemfanyia Bwana makao mazuri aweze kuheshimiwa katika dunia hii, hivyo Mungu anakwenda kulitukuza jina lako nawe utakuwa na makazi mazuri.

Kuanzia leo kwako ni makao salama, adui hataruhusiwa kuingia ndani ya nyumba yako, mchawi hata kuloga wewe wala kazi ya mikono yako na ibilisi hataigusa.

Shika haya ninenayo leo katika siku hii ya kwanza ya mwaka huu maana ndiyo yatakuwa yako katika mwaka huu.


Maswali niliyojiuliza na kuwaza .

Yaani unywe Double kick
Robot,Samson,Shimha ubaki salama?

Ule vyakula vya ovyo ovyo Bado ubaki salama?

Viongozi wenu wanawapoteza sana
FB_IMG_1704071682445.jpg
 
Back
Top Bottom