Nini kujenga madaraja? Kwani kuna Rais hakuwahi kujenga?
Ujuwe kuanzia Nyerere 1961-85 nini kilifanyika. Angalia barabara za kuanzia Dar- Tunduma, TAZARA na uanzishaji mashirika ya umma zaidi ya 400 huku kuna umoja wa kitaifa na elimu bure. Nenda kamuangalie AH Mwinyi 1985-1995 uone alifanya nini kwenye kuleta soko huria, barabara za njia 2 Dar es Salaam na barabara za Arusha Segera
Halafu njoo kwa BW Mkapa uone Baba wa uchumi na miundombinu namna alivyoteremsha deni la taifa. Yeye ndiye aliyehakikisha barabara ya Kahama-Nzega- Singida-Dodoma inakamilika ili Watanzania wa Kagera wasipite Uganda na Kenya wanapokwenda makwao
Mwishowe njoo kwa JKikwete uone alivyomailizia kuunganisha mikoa yote kwa barabara za lami kasoro Tabora - Mbeya.
Hawa watangulizi walifanya mengi kuliko hayo ila hawakuwa watu wa masifa kwa sababu walijuwa ndiyo kazi yao. Lakini huyo mshamba wa Chato alibakia kujitangaza kuwa eti yeye ndiyo kafanya makubwa.
Mungu hapendi Mijitu inayojitukuza, ndiyo maana dikteta lilikufa 2021