Aliua uchumi kwa kuondoa pesa kwenye private sector Ili yote ibakie serikalini bila kujua inaua
uchumi matokeo yake serikali ikawa Ina pesa ilihali wananchi Wana ukata.
Alileta mgawanyo wa kisiasa bila sababu kwa kupambana na wapinzani as if ni dhambi kuwa na mawazo tofauti.
Hakushughulika na mafisadi ambao walikua ndani ya mfumo... Aliwanyoosha wale mafisadi ambao hawakuwa kwenye network yake. Mfano mafisadi aliowalinda ni DEO Mwanyika huyu JPM alisema amesababisha hasara ya matrillion kupitia Makinikia ila hakumfunga Bali alimpa ubunge, same case kwa Nchambi licha ya ujangili alimuachia kiulaini kwa fine uchwara
Pia alitugawa kwa ukabila maana alikua na chuki za wazi kwa wakaskazini kisa tu upepo wa Lowassa.
Kingine alitugawa kwa uchama, kule kwetu walimkataa kabisa JPM 2015 Jamaa alivyokuja ziara mbunge wetu akaomba Maji aisee alitukanwa sababu tu tulichagua Chadema. Sasa inakuaje akusanye Kodi zote alafu maendeleo eti mpaka mchague CCM.
Hapo Bado sijaongelea alivyoharibu mifumo ya BOT kisa tu kukomoa benki binafsi. Kwa kupandishwa reserve ratio na kuondoa pesa za wizara kwenye benki binafsi bila kujua Aliua credit creation.