Mnaokataa Chato isiwe mkoa, kuna swali moja kwenu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Je, hawa Watu (wakimaanisha nyie wana JamiiForums) wanaokataa Chato isiwe Mkoa mbona Katavi (sasa Mkoa) Kijiografia ni Mdogo kuliko Chato na haina Miundombinu mizuri (hasa barabara) kama Chato lakini umekuwa Mkoa na wala hamkulalamika na kusema lolote ila kwa Chato Macho yamewatoka kama Bundi na Mishipa ya Shingo imewashupaal kama Nondo za Madirishani?

Haya sasa kama mnawaweza wajibuni.
 
Two wrongs,do not make it light,

Songwe, haikutakiwa kuwa mkoa, ingebaki Mbeya tu, Katavi ingefutwa, Manyara ingefutwa, Pwani Ingefutwa, Dar ingebaki na wilaya zake tatu tu, Ubungo, Kigamboni zingefutwa,

Hizi hoja kwamba unasogeza huduma kwa wananchi? Kwani umbali unaongezeka? Lazima tuwe na kikomo Cha idadi ya mikoa, wilaya, kata, bila hivyo kwa miaka 100 ijayo,tutakuwa na mikoa 70!
 
Tatizo sio Chato tatizo unalijua kabisa rohoni mwako Mkuu..watu hawana shida na Chato tatizo lipo kwenye Legacy ile ya Mwendazake.

Binafsi hata Chato iwe mkoa itokee tena Wilaya ndani ya Chato iwe tena Jiji sina tatizo kabisa.

Wacha kila mtu afaidi mema ya Nchi ili mradi tu taratibu zifuatwe.

Waambie waharakishe ule uwanja uliojenga kwa Pesa nyingi unaanza kuota Nyasi na hata Miezi sita haijafika.
Wapeleke hata Bomba D ipaki tu kule iruke ruke mara kadhaa.
 
Two wrongs,do not make it light,

Songwe, haikutakiwa kuwa mkoa, ingebaki Mbeya tu, Katavi ingefutwa, Manyara ingefutwa, Pwani Ingefutwa, Dar ingebaki na wilaya zake tatu tu, Ubungo, Kigamboni zingefutwa,

Hizi hoja kwamba unasogeza huduma kwa wananchi? Kwani umbali unaongezeka? Lazima tuwe na kikomo Cha idadi ya mikoa, wilaya, kata, bila hivyo kwa miaka 100 ijayo,tutakuwa na mikoa 70!
Rekebisha upesi hicho Kiingereza chako kibovu katika mstari wako wa Kwanza kabla 'Wordsmiths' wengi hawajagundua.

Jamani kana Kiingereza kwetu ni Changamoto tutumie tu Kiswahili chetu hiki kwani bado tu tutaonekana ni Wasomi sawa?
 
Ilikua ni kosa kubwa sana tulifanya kama taifa kuruhusu mtu kama magufuli kuwa rais.
Nitakuwa wa mwisho Kuamini hili kwani pamoja na Hayati Rais Dkt. Magufuli kuwa na Mapungufu yake ambayo hata akina Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete nao walikuwa nayo ila kwa Kiasi chake nae ametufanyia Mema na Maendeleo fulani Watanzania. Tupunguze Chuki Kwake na tuacheni Unafiki pia.
 
Two wrongs,do not make it light,

Songwe, haikutakiwa kuwa mkoa, ingebaki Mbeya tu, Katavi ingefutwa, Manyara ingefutwa, Pwani Ingefutwa, Dar ingebaki na wilaya zake tatu tu, Ubungo, Kigamboni zingefutwa,

Hizi hoja kwamba unasogeza huduma kwa wananchi? Kwani umbali unaongezeka? Lazima tuwe na kikomo Cha idadi ya mikoa, wilaya, kata, bila hivyo kwa miaka 100 ijayo,tutakuwa na mikoa 70!
Mikoa inaongezwa ili kuwapatia ulaji watoto na ndugu wa watawala, wenzetu sasa wanaongelea umoja sisi tunaongelea kutengana.
 
Je, hawa Watu (wakimaanisha nyie wana JamiiForums) wanaokataa Chato isiwe Mkoa mbona Katavi (sasa Mkoa) Kijiografia ni Mdogo kuliko Chato na haina Miundombinu mizuri (hasa barabara) kama Cbato lakini umekuwa Mkoa na wala hamkulalamika na kusema lolote ila kwa Chato Macho yamewatoka kama Bundi na Mishipa ya Shingo imewashupaal kama Nondo za Madirishani?

Haya sasa kama mnawaweza wajibuni.
Umemsikiliza mnazi wa Chato akiongea BBC Swahili kupambania mkoa na wewe umebeba vilevile alivyosema na kutengeneza 'hoja' pasipo kufanya utafiti huku bando unalo.

Mkoa wa Katavi una Ukubwa wa kilometa za mraba 45,843 huku Mkoa wa Geita ambao unapendekezwa kumegwa ili Chato iwe mkoa una ukubwa wa kilometa za mraba 20,054. Sasa hapo tu hiyo kijiografia uliyoizungumza inakataa, mkoa wa Katavi ni mkubwa kuliko Geita, Geita ikikatwa hata nusu basi Chato itakuwa na ukubwa wa kilometa za mraba elfu 10.
Prof. Tibaijuka aliwapa pendekezo badilisheni jina la mkoa wa Geita uitwe Chato na makao makuu ya mkoa yawe Chato itakuwa poa kuliko kung'ang'aniza kupata mkoa mpya.
 
Ndiyo maana kuna ulazima wa kupata katiba mpya, siyo mtu anajiamulia tu kufanya jambo fulani na kesho tukiamka tunakuta jambo limetendeka!
FB_IMG_1622533894528.jpg
 
Two wrongs,do not make it light,

Songwe, haikutakiwa kuwa mkoa, ingebaki Mbeya tu, Katavi ingefutwa, Manyara ingefutwa, Pwani Ingefutwa, Dar ingebaki na wilaya zake tatu tu, Ubungo, Kigamboni zingefutwa,

Hizi hoja kwamba unasogeza huduma kwa wananchi? Kwani umbali unaongezeka? Lazima tuwe na kikomo Cha idadi ya mikoa, wilaya, kata, bila hivyo kwa miaka 100 ijayo,tutakuwa na mikoa 70!
kwa manyara umepotea mkuu huko kwingine mi sipafahamu ila manyara na arusha ni sahihi ni pakubwa mno
 
Shule zetu hizi nazo ni majnga matupu; we jamaa si una degree ya SAUT? So kama kuna kosa tumewahi kulifanya then tuendelee kulifanya kwasababu huko nyuma tuliwahi kukosea!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom