Mnaoagiza Magari Japan kuweni makini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnaoagiza Magari Japan kuweni makini!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KakaKiiza, Mar 20, 2011.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Kutokana na Radioactive zilizopatikana Taiwan kwenye maharage!!Yaliyoagizwa kutoka Japan Nidhahiri hivyo mionzi ya nyukilia itakuwa imesambaa sehemu nyingi za japan!Hivyo hata katika magari inaweza kuwemo ningeomba wanaoagiza magari wakwasiliana na idara ya mionzi ili kabla yakutumika hapa Tanzania yakaguliwe kwanza kama yana mionzi ya nyukilia!
   
 2. K

  King kingo JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante kwa taarifa Mkuu
  Hivi hapa Bongo kuna idara ya mionzi na kama ipo inaweza kukagua na kujua kama baidhaa hii ina mionzi au la???? naomba kujulishwa tafadhali...
   
 3. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hoja nzuri, naomba kufaham hiyo mionzi huisha baada ya muda gani? Au ikifika imefika? Maana nakumbuka kuna taarifa ilitolewa kuwa kuna mionzi ilikuwa imefika katika maeneo ya bahari around 10 km ila wakasema stregth yake inapungua. Je, kwenye magari inakuwaje? Inang'ang'ania kwenye viti au sehem gani? Na inamaana haitaisha na vivyohivyo yale maeneo waliokuwa wanaishi raia hawatarudi tena?
   
 4. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Imagine yame magari yalio kua yana sombwa na maji, yakisha kuwa repaired yote yata letwa Africa huku tusio jali viwango na afya za watumizi.
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Shirka la Mionzi au Tanzania Commission of Radiation lipo Arusha maeneo ya Sakina.
  Ni zaidi ya miaka 17 tangu nifike hapo wakati viwanja vikiwa bado vinauzwa maeneo ya sakina kuzunguka shirika hilo.

  Wale wapendao kitu ili mradi ni imported naona wanapata somo.

  Fikiria kuhusu kurecycle chuma na plastic ambayo ni Radio active kisha kutengeneza Microwaves , majkofu,bicycles Toys na vyombo vingine vya majumbani.
  Fikiria kwamba raw materiala yenye radio active kibao kupelekwa China Indonesia Malaysia n kwingineko kutengeneza utitili wa kila kitu.

  Hapo ndipo kila mtu ikiwa ni pamoja na wajinga wanao dhani Technolojia si haki yetu waonapo umuhimu wa kujitegemea kuteknolojia.

  Ujamaa si lazima na si jambo muhimu lakini kujitegemea ni jambo la lazima na muhimu kwa taifa lolote duniani.

  Nchi za Third World zinalishwa sumu nyingi sana hasa zile za Heavy Metal kama Lead kupitia vyakula vinavyoingizwa kutoka nchi zenye viwanda na zisizo wajali walaji.

  Kipimo chetu cha maendeleo kama Third World ni Ulukuki wa kuhodhi bidhaa agahali kutoka nje ya nchi zetu hasa zile zitokazo First world.

  Umasikini mkubwa kuliko wote Duniani ni kudharau kilicho chako na zaidi ni kujidharau wewe mwenyewe na wajomba zako.

  In Shor radiation hukaa katika kitu kilicho athirika fo Thousand of years, japo the first hundred or so years ndiyo time ya madhara makubwa. Kule FUKUSHIMA Japan wanatumia Plutonium katika kufua umeme wao hebu ona Half life ya Plutonium katika Jedwali.


  RADIONUCLIDE HALF-LIFE

  Radon-222 4 days
  Iodine-131 8 days
  Krypton-85 10 years
  Tritium (Hydrogen-3) 12 years
  Strontium-90 29 years
  Cesium-137 30 years
  Americium-241 433 years
  Radium-226 1,622 years

  Plutonium-239 24,000 years

   
 6. L

  Lwikunulo Senior Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Jun 1, 2007
  Messages: 114
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  ....., my Almighty GOD!, I am speechless!:redfaces:
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Ikumbukwe kuwa hata hayo magari ambayo yamekuwa yakiagizwa kabla ya Tsunami hatajui kabla ya kuletwa huku yalipatwa na mikasa gani.
   
 8. L

  LAT JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  gonga hapa TANZANIA ATOMIC ENERGY COMMISSION (TAEC)
   
 9. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,487
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  m-bongo unadhani anaweza kuathirika na hiyo mionzi? itawadhuru hao wenyewe huku mchakamchaka wa maisha tu ni zaidi ya mionzi ya nyuklia
   
Loading...