Big up mkuu, fisadi hawezi kua kiongozi wa nchi hii, kwanza katudhiaki sisi maskini ambao tunatafuta pesa kwa jasho letu yeye mwizi wa mali za taifa anakuja na vimaneno na uchukia umasikini sasa tuibe kama yeye
MISHAHARA YA MARAIS BARANI AFRIKA 2015
Wakati Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akiupunguza mshahara wake muda mfupi baada ya kuingia madarakani mwaka huu, marais wengine wa Afrika wameonekana kujilimbikizia mishahara mikubwa, tofauti na pato ‘kiduchu' la wananchi wao kwa mwaka.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa mtandao wa African Review, marais watano wanaoongoza kwa kuwa na mishahara mikubwa kwa mwaka ni Rais Paul Biya wa Cameroon anayelipwa Dola za Marekani 610,000, akifuatiwa na kiongozi wa Morocco, Mfalme Mohammed VI anayelipwa Dola 480,000 na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ni wa tatu akilipwa Dola 272,000.
Rais Jakaya Kikwete ni wa nne kwa malipo ya Dola 192,000 na wa tano ni Rais Abdel Aziz Bouteflika wa Algeria, anayelipwa Dola168,000.
Mtandao huo umebainisha pato la Mtanzania wa kawaida kwa mwaka kuwa ni Dola 1750 sawa na Sh3.5 milioni, linalozidiwa mara 114 na kiasi anacholipwa Rais kwa mwaka.
Madhumuni ya utafiti wa mtandao huo ilikuwa kuangalia kiasi wanacholipwa marais wa Afrika kwa mwaka na kile inachopata taifa husika kwa muda huo.
Pia walilenga kuangalia uhusiano wa viongozi hao na wananchi wa kawaida wanaowangoza.
Kwa mujibu wa mtandao huo, vyanzo vya taarifa za mishahara ya marais hao vilipatikana kutoka mitandao na wanahabari wa nchi husika.
Tofauti na maraisi wengine, Rais mpya wa Nigeria, Muhammadu Buhari, alitangaza punguzo la mshahara wa rais pamoja na wafanyakazi wengine wa Serikali mara alipoingia madarakani.
Rais mwingine aliyefanya hivyo ni Uhuru Kenyatta wa Kenya, ambaye pamoja na makamu wake walipunguza mishahara yao kwa asilimia 20 baada ya kuingia madarakani mwaka 2013.
Mwisho, hapa fisadi ni nani?