Katika nchi zilizoendelea, wataalam katika fani mbalimbali za kitaaluma husakwa na, kama tegemeo la taifa, kukabidiwa jukumu la kuwa MSAURI wa Rais hata kama mtu huyu hana dini sawa na mheshimiwa, rangi, ukabila, ama itikadi za kichama. Nchi hizi hufanya vizuri sana kiuchumi na maeneo mengine muhimu kwa jamii.
Hapa nyumbani, nimebaini tu baada ya kupitia maoni yenu hapo juu kwa kumbe wengi hamfahamu Sheikh Yahaya Hussein na mguso wake katika ikulu yetu ya sasa. Huyu ndugu ndiye tegemeo kutuangazia uchumi wetu wa nchi itakavyokua siku za uso. Na kweli mfumuko wa bei nchini mwetu kila kukicha huruka sana moto wa msitu wa Amazoni kule Brazil; hili benchi la ufundi na viona-mbali binafsi linatafuna taifa bila hata kutoa risiti ya malipo. Kwa kiti chake hicho hicho hachelewi kutoa ushawishi wa ajabu kutaka kupenyeza ndani ya katiba yetu mawazo sumu ya ki-udini bila kuhojiwa na mtu.
Baba huyu anasadikika kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuona mambo kabla yetu sisi ambayo mara nyingi huchele sana kutokea wakati mwingine usitokee kabisa. Huyu ndiye Mzee Yahaya Hussein, mzee wa lango la Jiji Magomeni Mikumi. The World is like that men!!