Elections 2010 Mnajimu yahaya hussein na ccm kunani?

Mabel

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,273
677
Heshima kwenu wakuu

Jana usiku nilikuwa nikiangalia Chanel Ten, ndipo akaingia Sheikh Yahaya hussein na mambo yake, kwa kifupi mzee huyu alikuwa akimfagili JK kwa ushindi wake, alidiliki kumuita JK "Super President" kwa sababu zifuatazo;-
  1. JK alifanyiwa "midahalo" na maraisi watatu waliomtangulia kuwa anafaa, na hakuna raisi mwingine aliyefanyiwa hayo.
  2. JK ni chaguo la Mungu, akitumia vitabu vitakatifu kudhihilisha hili, kwenye Bible alitumia kitabu cha Isaya (siikumbuki aya)
  3. Baada ya JK kuchukua nchi, Bush alikuja Tanzania akakaa siku nne (ambapo ni tukio la kihistoria) na kutupatia vyandarua pia dola 800million zilitokana na safari yake kuja hapa
  4. JK alimaliza mgogoro wa kenya
Mzee huyu alikwenda mbali zaidi na kumsifia mke wa JK Bi Salima akisema hakuna raha kama yeye (Kwa tafsiri ya huyu mzee, mwanamke ni raha thus why alimwita Bi Salima "raha", alimfananisha na bikira Mariamu aliyetukuka kuliko wanawake wote. Aidha alisema haya juu yake.
  1. Alikwenda nyumbani kwake(Salima) siku moja kumwamkia akakuta watoto wake wakifundishwa Quran nyumbani chini yake, hii ikamfanya kuona hakuna kama yeye
  2. Pia walimwita kwenye mashindano ya kusoma Quran, Bi Salima alifanya vizuri sana
Mwisho huyu mzee aliwatakia watanzania wote sikukuu njema ya Iddi (hapo kesho) akisema sikukuu ya mwaka huu imekuja wakati mwafaka watanzania "wakisherekea" ushindi wa CCM na JK

Sasa mimi najiuliza, huyu mzee ni nani ndani ya CCM na selikali ? akumbuke alisema uchaguzi usingekuwepo mwaka huu na kudai mgombea mmoja atakufa, hayajatokea yote haya, au yeye na Tambwe wako kitengo kimoja ndani ya CCM?
 
aliniboa sana pale alipolazimisha wale watoto eti waseme"Tunataka Kikwete atuongoze"haya semeni mtoto mmoja akaakaa kimnya akamuuliza wewe mbn husemi mtoto bado kimnyaaaaaaaaaaaaaa,alafu mmmh sura yake kama imeshaanza kuchoka maana jana bana angekuwa ni mwanamke anaetumia mkorogo tungesema umedunda.
 
Hapa umenikumbusha, yule mtoto mmoja alikuwa kashika tama halafu tena kanuna
 
Antmbw. Hana lipya .... ingekua mtabiri kweli angekua anajificha oh mara hakuna uchaguzi, atkufa huyu, mara sijui ivi, nja inamsumbua
 
Achaneni na huyu Mzee,
Sijui ni nani huwa anampa jukwaa la kueneza mauzauza yake.
Huyu angetakiwa kunyimwa jukwaa la kuongelea maana anachosema hakisaidii taifa, akae nyumbani kwake aongee na watoto/wajukuu wake.
 
Uchawi uchawi uchawi uchawi nchi ikongozwa na walozi haifiki kokote kimaendeleo. Waarabu walikuwa wakitegemea uchawi kufanya mambo yao wakagundua hauwasaidii lolote..wameachana nao sisi bado tunang'ang'ania mabo yasiyo na kichwa wala miguu! Aibu
:A S angry:
 
Hii ni changamoto kwa mchungaji yule wa Moshi aliyesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu utashangaza wengi kwani Mungu kamwambia yeyote atakaetegemea nguvu za uchawi hatashinda uongozi, na ikitokea akashinda basi mchungaji kadai yupo tayari kupigiwa mawe. Sasa Jk siyo siri anautegemea sana uganga wa Yahya na wote wawili yaani Jk na Yahya wanajivunia matokeo ya ufundi wao hadharani bila hata kificho. Sasa ni zamu ya yule mchungaji kujitokeza hadharani ili tumpe zawadi yake ya mawe aliyoomba, au ajitokeze kuomba msamaha kwa wa Tz kuwa hakuzungumza na Mungu ama atujulishe kuna county attack gani na mda uwe specific vinginevyo hatutamuelewa na hata kama asipojitokeza tutamtafuta ili tumpe stahiki yake (mawe)!!
 
Antmbw. Hana lipya .... ingekua mtabiri kweli angekua anajificha oh mara hakuna uchaguzi, atkufa huyu, mara sijui ivi, nja inamsumbua

Ebana...eeeeeehhhh!!!! utakula BAN wewe..... ila me nakuunga mkono maana huyu jamaa kwanza nikimuona tu, achilia mbali utabiri wake, nasikia kifuchefuche......
 
Hii ni changamoto kwa mchungaji yule wa Moshi aliyesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu utashangaza wengi kwani Mungu kamwambia yeyote atakaetegemea nguvu za uchawi hatashinda uongozi, na ikitokea akashinda basi mchungaji kadai yupo tayari kupigiwa mawe. Sasa Jk siyo siri anautegemea sana uganga wa Yahya na wote wawili yaani Jk na Yahya wanajivunia matokeo ya ufundi wao hadharani bila hata kificho. Sasa ni zamu ya yule mchungaji kujitokeza hadharani ili tumpe zawadi yake ya mawe aliyoomba, au ajitokeze kuomba msamaha kwa wa Tz kuwa hakuzungumza na Mungu ama atujulishe kuna county attack gani na mda uwe specific vinginevyo hatutamuelewa na hata kama asipojitokeza tutamtafuta ili tumpe stahiki yake (mawe)!!
Huyu mzee kamaliza kambi yake (sijui bagamoyo au wapi) ya kumsaidia JK kupata ushindi kwa nguvu za giza karudi kwa kasi
 
katika tembea tembea niliwahi kutembelea zanzibar na kukutana na maongezi kuwa huyu mnajimu aliwahi kufungwa zanzibar kwa kosa la kuingilia kinyume na maumbile.najua wa zenj nao ni wana jamii tunaomba ukweli kuhusu hili.
 
Ndo wale wale tu wa CCM, yupo chini ya CCM huyo, na ndio maaana alijifanya kutabiri kifo kwa maraisi tena akasema watakao mpinga JK, hakukuwa na lolote zaidi ya kuwatishia watu na kuwatia woga wa kugombania nafasi... na vile vile kuwafanya wananchi wajiandae kisaikolojia kumpigia kikwete.. Hivi hamna habari, huyu ni shushu wa CCM, anajifanya mtabiri kumbe anasaidia serikali...
 
Katika nchi zilizoendelea, wataalam katika fani mbalimbali za kitaaluma husakwa na, kama tegemeo la taifa, kukabidiwa jukumu la kuwa MSAURI wa Rais hata kama mtu huyu hana dini sawa na mheshimiwa, rangi, ukabila, ama itikadi za kichama. Nchi hizi hufanya vizuri sana kiuchumi na maeneo mengine muhimu kwa jamii.

Hapa nyumbani, nimebaini tu baada ya kupitia maoni yenu hapo juu kwa kumbe wengi hamfahamu Sheikh Yahaya Hussein na mguso wake katika ikulu yetu ya sasa. Huyu ndugu ndiye tegemeo kutuangazia uchumi wetu wa nchi itakavyokua siku za uso. Na kweli mfumuko wa bei nchini mwetu kila kukicha huruka sana moto wa msitu wa Amazoni kule Brazil; hili benchi la ufundi na viona-mbali binafsi linatafuna taifa bila hata kutoa risiti ya malipo. Kwa kiti chake hicho hicho hachelewi kutoa ushawishi wa ajabu kutaka kupenyeza ndani ya katiba yetu mawazo sumu ya ki-udini bila kuhojiwa na mtu.

Baba huyu anasadikika kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuona mambo kabla yetu sisi ambayo mara nyingi huchele sana kutokea wakati mwingine usitokee kabisa. Huyu ndiye Mzee Yahaya Hussein, mzee wa lango la Jiji Magomeni Mikumi. The World is like that men!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom