Heshima kwenu wakuu
Jana usiku nilikuwa nikiangalia Chanel Ten, ndipo akaingia Sheikh Yahaya hussein na mambo yake, kwa kifupi mzee huyu alikuwa akimfagili JK kwa ushindi wake, alidiliki kumuita JK "Super President" kwa sababu zifuatazo;-
Sasa mimi najiuliza, huyu mzee ni nani ndani ya CCM na selikali ? akumbuke alisema uchaguzi usingekuwepo mwaka huu na kudai mgombea mmoja atakufa, hayajatokea yote haya, au yeye na Tambwe wako kitengo kimoja ndani ya CCM?

- JK alifanyiwa "midahalo" na maraisi watatu waliomtangulia kuwa anafaa, na hakuna raisi mwingine aliyefanyiwa hayo.
- JK ni chaguo la Mungu, akitumia vitabu vitakatifu kudhihilisha hili, kwenye Bible alitumia kitabu cha Isaya (siikumbuki aya)
- Baada ya JK kuchukua nchi, Bush alikuja Tanzania akakaa siku nne (ambapo ni tukio la kihistoria) na kutupatia vyandarua pia dola 800million zilitokana na safari yake kuja hapa
- JK alimaliza mgogoro wa kenya
- Alikwenda nyumbani kwake(Salima) siku moja kumwamkia akakuta watoto wake wakifundishwa Quran nyumbani chini yake, hii ikamfanya kuona hakuna kama yeye
- Pia walimwita kwenye mashindano ya kusoma Quran, Bi Salima alifanya vizuri sana