MMU baadhi yetu tupunguze ulalamikaji

MMU baadhi yetu tupunguze ulalamikaji

ragin

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
7,391
Reaction score
9,385
Habari za usiku wapenzi na wadau wote wa MMU,

Kiukweli tu humu kuna miibuko ni ya mda sana juu ya kuilalamikia jinsia flani hasa KE mtu kaombwa 10000 tu atakuja kuanzisha uzi kuwa wanawake kwa mizinga bhana mbaya zaidi unajumuisha ni wote.

Mtu ameona mdada kajipodoa sana na mawigi juu moja kwa moja ataanzisha uzi kuwa wanawake mda mwingi ni wa kwenye kioo.

Mtu amesalitiwa na mpenziwe atakuja huku kulalamika wanawake sio waaminifu ni malaya mbaya zaidi anawajumuisha ni wote.

Mtu kamvua pichu mke wa mtu kwa tamaa za mwili alafu atapost wake za watu hasa walio ndoani hujirahisisha tena bure napo mbaya zaidi anajumuisha na mengineyo mengi juu ya kumlaumu hasa mwanamke niwaulize tu mnapo kuja kupost humu malalamiko wengine hadi wanatusi jinsia ya kike mbaya zaidi huwa wanajumuisha kana kwamba ni wote ndio wapo hivo.

Je hamjawahi kufikiria kuwa hata mama/ dada/shangazi /mamdogo zenu nao wanawekwa kwenye makundi hayo mabaya mnayoyapost humu kwa kugenerelize? Punguzeni kuikashifu jinsia ya KE mkumbuke hiyo ndiyo inayowazaaa hiyohiyo ndiyo inayo wafanya muitwe baba wa Tafa la sasa na kesho.
 
Matatizo hayafanani...kama 10,000 kwako ndogo, ni kubwa Kwa wenzio!!
 
Binadamu pia tumetofautiana uvumilivu...we unaweza kuona ni tatizo dogo Ila mwingine ndo yamemfika haswaa!!
 
Binadamu pia tumetofautiana uvumilivu...we unaweza kuona ni tatizo dogo Ila mwingine ndo yamemfika haswaa!!
Wapo wenye matatizo na analeta mada inayoeleweka. Juzi hapa mtu kapost analalamika demu kamuomba vocha ya buku. Seriously?
Kwanini asimwambie huko huko kuwa sina? Kaja kugeneralise wanawake tumezidi.
 
Wapo wenye matatizo na analeta mada inayoeleweka. Juzi hapa mtu kapost analalamika demu kamuomba vocha ya buku. Seriously?
Kwanini asimwambie huko huko kuwa sina? Kaja kugeneralise wanawake tumezidi.
Usimlaumu dadaangu, huenda ndio the best thing he can post....hili ni jukwaa lenye watu aina zote!!!
 
Utoto umeharibu heshima na hadhi ya MMU
yaani sijui limekuwa jukwaa la watoto au veep post hazina mantiki ila za ulalamikaji tu

ukichunguza mtoa mada eti utasikia yupo chuo au form six au kitaan pia yaani ni tabu
 
Wapo wenye matatizo na analeta mada inayoeleweka. Juzi hapa mtu kapost analalamika demu kamuomba vocha ya buku. Seriously?
Kwanini asimwambie huko huko kuwa sina? Kaja kugeneralise wanawake tumezidi.
hapo ndo sielewagi kbsa

yaani mwanaume ukilalamika dunia nzima ijue umeombwa vocha ya buku hiyo ni aibu na fedhea ni bora umalize kimyakimya.
 
Usimlaumu dadaangu, huenda ndio the best thing he can post....hili ni jukwaa lenye watu aina zote!!!
Na huyo aliyeomba vocha akanyimwa aje kuanzisha mada jamaa kamnyima vocha ya buku. Ha haaa jamani kazi ipo. Anyway ni maamuzi ya mtu
 
Na huyo aliyeomba vocha akanyimwa aje kuanzisha mada jamaa kamnyima vocha ya buku. Ha haaa jamani kazi ipo. Anyway ni maamuzi ya mtu
Hahaaa!! Ndio..at the end of the day ni maamuzi ya mtu!
 
Binadamu pia tumetofautiana uvumilivu...we unaweza kuona ni tatizo dogo Ila mwingine ndo yamemfika haswaa!!
ila mkui uvimilivu ukikushinda

wapi penye nafuu kuwaambia watu usiowaona wala kuwajua au kumwambia mhusika au marafiki waliokuzunguka ambao mnaonana ana kwa ana daily?
 
Back
Top Bottom