Wakuu,
Nazitambua juhudi za wafuasi wa babu na mashabiki wake katika kujaribu kumtetea ionekane ni jambo la kawaida sana kwa Dr. W. Slaa kuwa na kadi ya CCM mpaka leo! Juhudi za kutumia social media na magazeti mengine hasa gazeti la M4C(TanzaniaDaima) kujaribu kumtetea Slaa na wakati huo kunikejeli na kunitukana japo kuwa kwa matusi ambayo lazima nikiri si mapya, yalishawahi kutumiwa dhidi yangu au watu wengine duniani. Hapa nitajibu hoja moja baada ya nyingine( wenye matusi mapya wanakaribishwa wakijisikia kunitukana tena).
1. Katika matamshi yangu hakuna mahali nilipohusisha kuwa na kadi na uanachama wa mtu.....hivyo wanaojaribu kubwabwaja kuwa sijui Katiba ya CCM wanakurupuka kwasababu ndogo sana..kukairishwa lazima kumtukana Nape hata bila kupima kwa makini hoja....nilichosema Dr. Slaa na baadhi ya vigogo wa CDM wana kadi za CCM na baadhi yao wanazilipia mpaka leo. Sijazungumzia uanachama wao...najua kuwa kwa katiba ya CCM ukisha kuwa mwanachama wa chama kingine uanachama wako CCM unakufa hapohapo.
2.Ni kweli kuwa hakuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya kuwa na kadi ya CCM kwa babu na maendeleo ya wananchi masikini, lakini babu anatafuta kuwa kiongozi wa nchi ANAPASWA KUISHI YALE ANAYOYASEMA NA KUWA MWAMINIFU KWA NAFSI YAKE MWENYEWE. Ni Dr. huyu ambaye huhamasisha wananchi wengine warudishe kadi za CCM anapofanya mikutano ya hadhara wakati yeye kabaki nayo bila kuanza yeye kuongoza kwa kuonyesha njia kwa kuirudisha yake kwanza...USIPOKUWA MWAMINIFU KWA KIDOGO HUWEZI KUWA MWAMINIFU KWA KIKUBWA PIA....si ajabu alishindwa kutii kiapo chako na nadhiri yake kwa Mungu aliyoapa akiwa padri..leo nitashangaa akiwa mwaminifu kwa binadamu mwenzake kama kashindwa kumweshimu Mungu.
3.Lakini ni siku chache sana zimepita babu aliwatuhumu baadhi ya viongozi wa Chadema Kigamboni kuwa ni mapandikizi ya CCM kwa chama chake...nikashangaa sana, babu anawatuhumu wenzake ambao hawana hata kadi za CCM kama yeye kuwa ni mapandikizi ya CCM huku yeye ambaye kwa tafsiri hii ni pandikizi namba moja akijifanya ni msafi sana..nilichofanya ni kumkumbusha kuwa yeye ndio "pandikizi" namba moja kwahiyo aanze kujifukuza yeye.
Endeleeni kumtetea nianike mtiririko wa kulipia kwake kadi yake ya CCM.