A
Anonymous
Guest
Sisi Wananchi wa Mbezi Msumi Shina Namba 7 kuna Mjumbe anaitwa Michael Meshack Mnyeke, asilimia kubwa ya Wananchi wa huku hatumtaki kutokana na tabia yake ya kuonea watu na kutumia madaraka yake vibaya.
Alhamisi iliyopita tulifanya kikao cha Wananchi pamoja viongozi wa Mtaa pamoja na CCM ambao ndio wamempa nafasi hiyo, tumewasilisha malalamiko yetu na wakasema watayafanyia kazi lakini mpaka leo Machi 12, 2024 hakuna kilichojibiwa.
Baadhi ya manyanyaso ambayo amekuwa akituhumiwa ni kuingia ndani ya nyumba za watu bila utaratibu, anatamba hakuna wa kumfanya kitu chochote kwa kuwa yeye ndio Serikali, amekuwa akichukua mali za watu kwa nguvu, mfano hivi karibuni alimpora mtu pikipiki kwa kutumia cheo chake.
Malalamiko haya nyafikisha hapa kwa kuwa kama hatua hazitachukuliwa tumekubaliana kuwa tunaweza kurudisha kadi za Uanachama kwa kuwa CCM wakiendelea kumuacha inamanisha wanaridhia tuendelee kunyanyasika.
====== ==
JamiiForums ilipozungumza na Balozi wa Mbezi Msumi, Ismail Mbinda amesema “Kweli nimepata malalamiko ya Mjumbe huyo na Wananchi wameyawasilisha katika Ofisi ya CCM Mbezi Msumi ambayo ndio imemdhamini, wao huko ndio watatoa majibu na kujua hatua za kuchukua.”