Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,370
- 39,186
Mimi naogopa watu wanapotambulisha kiongozi au mtu yeyote yule na kutanguliza au kumalizia kwa jina la kabila lake, kwani bado sijaelewa ni kwanini "Mmasai, Mmeru, Mkwere" itumike kumtambulisha mtu anayejulikana tayari kuwa ni mtu wa kabila fulani. Kutumia vielelevyo hivyo vya kikabila inahitaji kuonesha nini? Kwani Mnyakyusa Mwakyembe, na Mhaya Karamagi, na hata Mngoni Nchimbi au yule Mpare Mgonja n.k makabila yao yanahusiana vipi na ufisadi au uadilifu?
Kama ni muhimu kujua kabila la kiongozi ili tuweze kupima ufisadi na uadilifu haiwezekani kuwa tuna sentiments za kikabila au ukuu wa kikabila na kuona makabila mengine duni!? Lakini yawezekana kuna sababu za kutumia vitambulisho vya kikabila wanapozungumziwa baadhi ya viongozi (maana si wote) naomba mnidokeze na mimi nianze kutumia maana mara zote huwa natetemeka sana ninapoona hili; labda ndio uzee wenyewe huu. Au ndiyo nimepoteza sense yangu ya mizaha na utani wa jadi?