Mlokole aliyeifedhehesha weekend yangu...

Mlokole aliyeifedhehesha weekend yangu...

Pole sana my dia,kuna baadhi ya walokole huwa wana mambo ya ajabu sana,halafu wanalazimisha,halafu hayo
haya mambo ya kuonyeshewa mchumba mi siamini kabisa,utaonyeshewaje mchumba wakati una macho?

Taratibu Excellent FirstLady keshasema ana mtu halafu wewe unamwita "my dia" (dear kama sikosei)? Hivi mke wa mtu anaweza kuwa "my dear" wa mtu mwingine? Usije ukamfanya akadhani wewe ndiye yule mlokole ile umekuja kivingine!!!!
 
Jamani kama mnavyojua haya ma long distance ..Ndio nimetoka kumpokea mzee baada kuwa mbali kwa takribani miezi kadhaa,,
Mida ya saa mbili usiku naanda chakula mala simu inaita...naenda kupokea inakatika,
Ikaita tena ..Ile napokea napokelewa na salam ya bwana asifiwe
OOh nikaitikia kwa amani zote amina na wewe bwana asifiwe.
mala simu ikakatika .
mpendwa akaendelea sasa kubeep nikipiga hapokei ndipo nilipoamua kumtumia sms nikimwambia asinibeep.
Husband akasema piga.
Mlokole kapokea na sauti inatoka kila kona ya nyumba inasikika usiku
ooh nimefunga kwa muda wa week 3 nimeonyeshwa wewe ndo mke wangu mke mwema...najua hunijui sijui naitwa A.....
Naomba upokee maombi yangu...
Nikauliza simu yangu umetoa wapi..
Mlokole kanambia kaipata kwa uwezo wa roho mtakatifu.
Nikamwambia lakini mpendwa mbona nimeolewa nina familia tayari huyo roho mtakatifu aliyekuongoza amekosea
Jaribu kufunga tena.
Mlokole akasema ooh ndoa huwa zinavunjika ...
Na yeye yuko tayari kusubiri ndoa yangu ivunjike ili aje kuleta posa..
Ni mtu gani wa kusubiri ndoa ya mwenzie ivunjike eti kaokoka????

Mzee akabakia anaguna tu huku mie nikiendelea kushangaa.
Huyu mlokole mbona ananiletea balaa mwenzenu.:nono:


Hivi kina mama siku hizi mmeacha kutumia ule msemo maarufu wa "Unikome kama ulivyokoma kunyonya ziwa la mama yako?
 
Bigirita[/FONT] unachezea nguvu za roho mtakavitu?

Pole FirstLady1 (halafu hebu nipe namba ya huyu jamaa nimuunganishe na dada mmoja anatafuta mme, hope tutaweza kumbadili mawzo huyo roho mtakavitu)
RR nimekutumia PM naomba ujitahidi kuondoa hiki kikombe mbele yangu
 
Last edited by a moderator:
We tata nae bana unatibua ndoano za watu bhana!

Mwache excellent ajinoe bana!

Hahaaa! Kuna wakati unakaa mpaka mwaka mzima hujataja neno 'DEAR'! Kwenda kwa mtoto wa kike!



Taratibu Excellent FirstLady keshasema ana mtu halafu wewe unamwita "my dia" (dear kama sikosei)? Hivi mke wa mtu anaweza kuwa "my dear" wa mtu mwingine? Usije ukamfanya akadhani wewe ndiye yule mlokole ile umekuja kivingine!!!!
 
Last edited by a moderator:
Hivi kina mama siku hizi
mmeacha kutumia ule msemo maarufu wa "Unikome kama ulivyokoma
kunyonya ziwa la mama yako?

ha!ha!haa!duh!umenikumbusha mbali au "koma kampende mama ako mzazi"
 
Labda ni yule aliyedai ameambiwa na "roho mtakatifu" amwache mke wake na aoe mwingine. Hiyo ni output ya Wachungaji wengi drama, kuna yule aliyedai ukilipa US 25000/= anakuonyesha kama jina lako limeandikwa kwenye kitabu cha uzima au la! Pia kuna mchungaji hapa bongo aliyepata maono ya kufunga ndoa yake upya, may be ni huyo! Kila la heri.
 
Kwa jina la Yesu, achika! mlokole anangoja. Hizi dini zingine ni vituko tu.
 
We tata nae bana unatibua ndoano za watu bhana!

Mwache excellent ajinoe bana!

Hahaaa! Kuna wakati unakaa mpaka mwaka mzima hujataja neno 'DEAR'! Kwenda kwa mtoto wa kike!
Hahaha! umenikumbusha ngoja leo nikirudi nyumbani nikamwite "dia". Litakuwa surprise la nguvu na mimi sharti aniite "bebi" mambo ya uzee mwisho Chalinze.
 
Hahaha! umenikumbusha ngoja leo nikirudi nyumbani nikamwite "dia". Litakuwa surprise la nguvu na mimi sharti aniite "bebi" mambo ya uzee mwisho Chalinze.

umuite dia? babake leo unaachika!!!!

utasikia anakujibu, '' malaya wako ndo kakufundisha eenh! mwanume fedhuli sana wewe''... urudi kuomba ushauri eenh!
 
khaa! pole mamito kwa kisanga hicho
Huyo mtu anakufahamu fika alitaka kukutega
tu mtengoni mwake
na isitoshe anataka kuivuruga ndoa yako
cha kufanya wewe mwendee kwenye
magoti naye atakimbia, ni pepo huyo
anamsingizia roho mtakatifu bure
achana naye kabisa asikutishe
 
Back
Top Bottom