Mlipuko wa kipindupindu ni aibu kubwa, serikali fundisheni watu kunawa mikono

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,261
Serikali amrisheni sehemu zote zinazouza vyakula ziwe na masinki au ndoo za maji za kunawa mikono(sio kunawa kwa vikombe na majagi katika bakuli)na zisitumbukizwe majagi au bakuli za kunawia.

Pia wapeni elimu raia wakati muhimu zaidi wa kunawa mikono na sabuni ni kabla ya kula na sio baada, raia wengi wateja wa vyakula na wahudumu wengi wanaelewa kinyume.

Ni aibu katika karne hii watu hawajui umuhimu na jinsi bora ya kunawa mikono.
 
Kwamba unaamini chanzo cha kipindupindu ni watu kutokunawa mikono sio?
Ukitoka chooni ambako kumetumiwa na watu wa kipindupindu na usinawe mikono kwa sabuni kabla ya kula au kukatakata kachumbari utapata kipindupindu au kusababishia wengine kipindupindu.
 
Back
Top Bottom