Je, kudhibiti kipindupindu ni lazima tuzuie biashara zingine zisifanyike?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Nimesikitishwa na maono ya wataalamu wetu katika sekta ya afya kwa kuchukulia mambo kiimla-imla pasipo kuwa na consideration katika maamuzi yao ambayo kwa namna moja au nyingine uathiri maisha ya watanzania wenzao.

Ni kweli taifa linakabiliwa kwa sasa na mlipuko wa magonjwa yatokanayo na uchafu na ni aibu kubwa kwetu kushindwa kujenga vyoo vya kisasa, miundombinu mizuri ya maji taka mijini, bado tunakabiliwa na utupaji taka holela na hatuishi maisha ya kuzingatia kanuni za kiafya.

Leo hii (kwa mujibu wa agizo la waganga wakuu nchini) haruhusiwi mtu yeyote yule kufanya biashara ya kuuza mahindi, karanga, matunda,juisi, samaki n.k katika maeneo ya kibiashara hasa yenye msongamano au mwingiliano mkubwa wa watu kama vile stendi za mabasi n.k

Mimi nadhani sayansi ipo ili kutusaidia tuweze kutatua changamoto zinazotukabili na siyo kuongeza changamoto.

Haiwezekani mtu anayeuza mahindi ya kuchemsha tena kwa kutembeza kichwani na ndoo yake asiye na kipato cha kusurvive hata usiku mmoja umwambie asifanye biashara mpaka kipindupindu kitakapoisha ili hali wa buchani (mwenye kipato) yeye umempatia solution ya namna gani awalinde wateja wake kwa kuhakikisha usalama wa kitoweo chake kwa kutumia uzio wa kioo na usafi wa nyama ikiwemo kutokuning'iniza.

Tunaelewa siku zote anachokiongea daktari huwa hatukipingi lakini kwa hili naona kuna jambo haliko sawa na ninapata mashaka kidogo ninapojiuliza maswali yafuatayo;

1. Ni nani ana uhakika kama si nadharia kuwa wafanyao biashara ndogondogo za vyakula ndiyo waenezao maradhi ya milipuko kama kipindupindu?

2. Je, kama wadau wa afya mmechukua hatua zipi kuhabarisha umma (kwa njia mihadhara, matangazo,vyombo vya habari n.k) juu ya ugonjwa huu na kuenea kwake?

3. Je, ni hatua zipi za makusudi zimechukuliwa katika ngazi za mitaa au vijiji kuhakikisha hali ya usafi, ubora wa vyoo na utiririshaji holela wa maji taka katika vyanzo vya maji kipindi hiki cha mvua nyingi umezingatiwa?

Kwanini umwambie muuza miwa sitaki kukuona hapa tena mpaka ugonjwa uishe, badala ya kuja na suluhisho kuwa unatakiwa kwa sasa usiimenye miwa yako na kuitembeza ulivyokuwa ukifanya hapo mwanzo na badala yake ikatwe vipande vipande ioshe na maji moto kisha ihifadhiwe katika makontena/ndoo(transparent) na ufunike na pili uwe na karatasi maalumu iliyobandikwa juu ya makontena hayo ikielezea tahadhari juu ya ugonjwa huo hili hata mteja wako aweze kuzingatia na kuchukua hatua.

Kwanini kipindi kile cha Korona tuliweza kuwa na ndoo za maji moto na sabuni kwa ajili ya kunawa kwa kila mfanyabiashara lakini hili la kipindupindu tushindwe tu kusafisha mazingira, kuuza vyakula vyetu gengeni katika vichanja, kutumia vifaa maalumu kuokotea, kupakua au kufungia vyakula, kuhakikisha vyakula vinavyopaswa kuliwa vikiwa moto vinajotoridi stahiki na kanuni zingine za ujumla kama kunawa mikono, kusafisha vyoo na mazingira kiujumla.

Naamini bado kuna namna wanasayansi wetu mnaweza kuja na suluhisho zuri katika namna ambayo ni shirikishi na yenye faida kwa wote.
 
Back
Top Bottom