Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 775
- 1,332
Watu wanne walijeruhiwa nchini China wakati mwanamme mmoja alirusha bomu la kutengenezewa nyumbani, lilikuwa limewekwa ndani ya chupa ya bombe katika uwanja mkuu wa ndege mjini Shanghai.
Mshambuliaji huyo kisha alichukua kisu na kukata shingo lake. Kwa sasa yuko katika hali mahututi hospitalini.
Bado haijabainika kilichosababisha afanye shambulizi hilo lililotokea karibu na kituo cha ukaguzi.
Safari kadha za ndege zilicheleweshwa lakini sasa shughuli zimerejea hali ya kawaida.
Chanzo: BBC