Ajilipua ndani ya Uwanja wa Ndege na Kuua Watu 35 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajilipua ndani ya Uwanja wa Ndege na Kuua Watu 35

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,219
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mmoja wa majeruhi
  Mtu mmoja amejitoa mhanga kwa kujilipua na bomu ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moscow nchini Urusi na kupelekea vifo vya jumla ya watu 35 na kujeruhiwa kwa watu zaidi ya 100.

  Ilikuwa ni hali ya kutisha kwenye uwanja wa ndege mkubwa kuliko yote nchini Urusi wa Domodedovo Airport uliopo kusini mwa mji mkuu wa nchini hiyo Moscow.

  Muda mfupi baada ya mtu mmoja kujilipua ndani ya uwanja wa ndege huo kwenye sehemu ya kupokea abiria wanaowasili ilikuwa haijulikani yupi yupo hai au yupi amefariki kutokana na mazingira ya kutisha iliyojitokeza.

  Rais wa Urusi Dmitry Medvedev aliitisha kikao cha ghafla ambapo alisema kuwa tukio hilo lililotokea leo jumatatu kuwa ni la kigaidi na kuagiza ulinzi mkali kwenye viwanja vya ndege na stesheni za treni.

  "Leo saa kumi na nusu (kwa saa za Urusi), mlipuko umetokea kwenye uwanja wa ndege wa Domodedovo Airport,", ilisema taarifa ya kikosi cha upelelezi cha Urusi.

  Maafisa wa Urusi walisema kuwa mlipuko huo ulitokea kwenye eneo la kuchukulia mizigo kwenye sehemu ya kupokea abiria wanaowasili.

  Watu 35 wamefariki na wengine 130 wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambapo 20 kati yao hali zao ni mbaya sana.

  Polisi wa Urusi wameanzisha uchunguzi wa mlipuko huo ambapo taarifa za awali zimeonyesha kuwa kuna mtu alijitoa mhanga kwa kujilipua mwenyewe ndani ya uwanja huo wa ndege.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Hatari sana.
  KGB imekufa kabisa siku hizi?
   
 3. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  KGB limegeuka kundi la magaidi
   
 4. E

  E Hazard Senior Member

  #4
  Nov 24, 2014
  Joined: Nov 6, 2014
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaazi kweli kweli
   
 5. KikulachoChako

  KikulachoChako JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2014
  Joined: Jul 21, 2013
  Messages: 14,095
  Likes Received: 11,584
  Trophy Points: 280
  Warusi wana roho mbaya sana....

  Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
   
 6. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2014
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Magaidi
   
 7. Jamiix

  Jamiix JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2014
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 817
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 80
  Siku zote mlikua wapi hamku comment? mnatuchafulia tu upepo humu
   
Loading...