Mlipuko Tabata waua watatu

Mlipuko Tabata waua watatu

Mafundi welding wote. Jihadharini na kuchomea ma tank. Toka nakua na akili,watu wengi wamekufa wakichomelea ma tank ya petrol,diesel au gas. Jiangalieni tafadhali.

Asante kaka
 
ajali tena..hawa OSHA wako wapi...?

OSHA ndio wanaozuwia vifo?
Tunasoma ktk vitabu vya mungu kuwa hakuna ajuaye siku wala saa.
Sasa namshangaa mtu anayemtegemea osha azuwie vifo.
 
A huge explosion has been heard
around Tabata in Dar es Salaam.
We saw black smoke rising up in
the air from nearby Tabata Oilcom.
My office door felt like being ripped
off by the massive gigantic bang.
So far we cannot confirm what
happened, lets hope the security
agencies provide an update on this.
......................................Update on the Tabata Dar es Salaam
explosion an hour ago. Three welders
have lost their lives instantly while
welding a tanker. The tanker was
being welded at Ally Shum Co. Ltd ,
Tabata , Dar es Salaam.

Jana mida ya saa 12 kasoro nilikua UDSM tukasikia mlipuko wa kishindo sana mpaka tukabak tunaulizana,kumbe kuna nguvu kazi imepoteza maisha maskin
 
OSHA ndio wanaozuwia vifo?
Tunasoma ktk vitabu vya mungu kuwa hakuna ajuaye siku wala saa.
Sasa namshangaa mtu anayemtegemea osha azuwie vifo.

Mdau panda gari lisilo na break basi,maana unamtegemea mungu,sasa break kwenye magari zimewekwa za nin,japo tutakufa ila hadhari ni muhim sana,ndo maana tunaumwa tunatibiwa,OSHA wapo kwa ajil ya kusimamia usalama kazini,
 
Haya majanga sijui yataendelea mpaka lini!
Tunashindwa hata kujifunza kitu!
Ila ni faida ya serikali legelege ya jk!

Kutojifunza kwako na Kuwa na Tahadhari kuna Uhusiano gani na Serikali Ya Jk?unafikiri kwa kutumia Miguu?
 
Duuuu?mkuu ungemjibu tu kwa ustarabu nadhani angekuelewa!!Kulikuwa hakuna haja ya kumwambia akaangalie picha ya bibi yake!!!
Hili sio jibu zuri. ni kashfa. ni dharau etc. Being polite does not cost you anything. metina

Hii habari utatuthibitishia je?

Hilo jibu la picha ya bibi wengi limewauma. Lakini kwa mlolonho wa some members hapa JFni kama wanajoke wanaposema weka picha, hawana lengo zuri zaidi ya joke coz hata kama story inaeleweka na haona uhusiano woth photo, watakuja na kukuambia weka picha.
Mfano unaweza kuomba ushauri juu ya kitu flan, mtu anakuambia weka picha.
So hili jibu la picha ya wakaangalie picha za mabibi zao litawafaa sana.
 
source ni Afp au Reuters maana umebong'a ung'eng'e mtupu haya hebu andika kwa kiswahili na useme tabata ipi
 
Hilo jibu la picha ya bibi wengi limewauma. Lakini kwa mlolonho wa some members hapa JFni kama wanajoke wanaposema weka picha, hawana lengo zuri zaidi ya joke coz hata kama story inaeleweka na haona uhusiano woth photo, watakuja na kukuambia weka picha.
Mfano unaweza kuomba ushauri juu ya kitu flan, mtu anakuambia weka picha.
So hili jibu la picha ya wakaangalie picha za mabibi zao litawafaa sana.
acha kupanic wewe!!sasa kwa akili yako unadhani ukimwambia aangalie picha ya bibi yake ndio utakuwa umetatua tatizo???punguza stress maisha yenyewe ni mafupi!!
 
A huge explosion has been heard
around Tabata in Dar es Salaam.
We saw black smoke rising up in
the air from nearby Tabata Oilcom.
My office door felt like being ripped
off by the massive gigantic bang.
So far we cannot confirm what
happened, lets hope the security
agencies provide an update on this.
......................................Update on the Tabata Dar es Salaam
explosion an hour ago. Three welders
have lost their lives instantly while
welding a tanker. The tanker was
being welded at Ally Shum Co. Ltd ,
Tabata , Dar es Salaam.
Asante mkuu Bujibuji kwa taarifa. Kuna mchokozi mmoja eti anauliza kiinglish hiki ni chako au eti umekata AFP?? Nimecheka sana. Unyenye wengi wanajua ila kwa ajili ya wengi basi Kiswahili kinatumika.
 
Elimu ya usalama kazini bado sana TZ. Osha wamekaa tu maofisini
Mkuu hiyo kazi yenyewe ni ya hatari sana kwa sababu hilo tanker whether lilikuwa au halikuwa na mafuta bado ilikuwa ni hatari tu.
Poleni sana waathirika.
 
A huge explosion has been heard
around Tabata in Dar es Salaam.
We saw black smoke rising up in
the air from nearby Tabata Oilcom.
My office door felt like being ripped
off by the massive gigantic bang.
So far we cannot confirm what
happened, lets hope the security
agencies provide an update on this.
......................................Update on the Tabata Dar es Salaam
explosion an hour ago. Three welders
have lost their lives instantly while
welding a tanker. The tanker was
being welded at Ally Shum Co. Ltd ,
Tabata , Dar es Salaam.

This is the story:

Lori la mafuta lalipuka Dar, wawili wajeruhiwa




mlipuko.jpg
Mafundi wa Kampuni ya Oilcom wakiangalia mabaki ya lori la kampuni hiyo lililochanika baada ya kulipuka kwa tanki lake wakati likichomewa katika eneo la Tabata Relini, jijini Dar es Salaam jana.

Dar es Salaam. Taharuki ya aina yake ilitokea jana eneo la Tabata Relini kwenye yadi ya malori ya Kampuni ya Oilcom baada ya kutokea kishindo kikubwa kilichotokana na kupasuka kwa tanki la mafuta.

Tukio hilo lililotokea saa 11 jioni, lilizua hofu miongoni mwa wakazi na wafanyakazi wa eneo hilo, na lilitokana na hitilafu ya kiufundi wakati wa kulitengeneza tanki hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo lililojeruhi watu watatu waliliambia Mwananchi kuwa mlipuko huo ulitokea wakati fundi akichomea sehemu ya tanki katika karakana ya magari ya kampuni hiyo.

"Kuna fundi alikuwa juu ya lori akipima mifuniko na chini alikuwepo dereva wa lori hilo na fundi mwingine wa kuchomea vyuma akichomea, wote walikuwa wakiendelea na kazi.

"Dereva wa lori hilo alikuwa akimuelekeza fundi sehemu ya kuchomea na ghafla ukatokea mlipuko mkubwa," alisema Omari Wenge, fundi katika karakana hiyo.

Alisema mlipuko huo ulimtupa chini fundi aliyekuwa juu ya tanki na kulikosababisha aumie usoni na sehemu za kifuani.

Shuhuda huyo alisema dereva na fundi wa kuchomea, waliumizwa sehemu mbalimbali za mwili kwa kupigwa na vipande vya mabati ya tanki na kichwa cha gari hilo.

Majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Camillus Wambura alisema kuwa hakuwa amepata taarifa zozote za ajali hiyo hivyo angetujulisha pindi angezipata.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia baadhi ya wafanyakazi wa karakana hiyo wakipewa huduma ya kwanza baada ya kuzimia kwa mshtuko huku wengine wakiweweseka kwa hofu.

Kichwa cha lori hilo kilichakazwa na mlipuko huo ambao moja ya mabati yanayoligawa tanki hilo yalitupwa upande wa pili wa Barabara ya Mandela.

Sehemu ya juu ya mbele ya lori hilo, ilitupwa juu ya paa la moja ya majengo ya karakana hiyo huku chini zikiwa zimetapakaa nyaraka na mabaki mengine ya sehemu ya mbele ya lori hilo.

Naye mmoja wa mashuhuda, Boniface Msisi aliyekuwemo ndani ya karakana hiyo, alisema hali ndani ya eneo hilo ilibadilika ghafla huku kila mfanyakazi akitafuta mlango wa kutokea.


"Mmoja wa mamalishe wanaotoa huduma ya chakula katika eneo hilo, alizimia mara baada ya kusikia kishindo hicho...kila unayemuona hapa ndio kwanza anarudi katika hali yake," alisema Msisi huku akionyesha sehemu ya tanki iliyokuwa ikichomewa.

Alisema kuwa lori hilo lilikuwa limetoka safari hivyo walikuwa wakilifanyia matengenezo ya kawaida.

Juhudi za kuupata uongozi wa karakana kuzungumzia ajali hiyo uligonga mwamba kutokana na viongozi hao kuwa katika harakati za kuokoa maisha ya majeruhi.

Source: Mwananchi 03/04/2014
 
Mkuu hiyo kazi yenyewe ni ya hatari sana kwa sababu hilo tanker whether lilikuwa au halikuwa na mafuta bado ilikuwa ni hatari tu.
Poleni sana waathirika.

Kwa kawaida tenki la mafuta huwa linatakiwa lioshwe vizuri kabla ya kuanza kuchomea na lisiwe limefungwa kwa mifuniko. Hii ni kwa matanki yote yale ya kubebea mafuta kwa ajili ya kuyasafirisha na yale yanayokuwa kwenye gari kwa ajili ya kupeleka mafuta kwenye injini.
 
Umeendelea hivyo,
Hongera,
............ Poleni kwa majanga hayo.
 
Kwa kawaida tenki la mafuta huwa linatakiwa lioshwe vizuri kabla ya kuanza kuchomea na lisiwe limefungwa kwa mifuniko. Hii ni kwa matanki yote yale ya kubebea mafuta kwa ajili ya kuyasafirisha na yale yanayokuwa kwenye gari kwa ajili ya kupeleka mafuta kwenye injini.
Asante kwa ufafanuzi mkuu, hivyo yawezekana utaratibu huo haukufuatwa?
 
Back
Top Bottom