Mkuu lile halikuwa limeoshwa na nawezekana wakati wanachomea walikuwa hawajafungua mifuniko kuruhusu hewa kutoka hasa ukitilia maanani lilikuwa na mafuta na tena kama ni petrol basi walikuwa kama watu wanaolipua bomu la nyuklia. Yaani tenki hata kama ni la gari ndogo ukianza kulichomea tu bila kuliosha kwa maji na sabuni huwa linalipuka na linaweza kukurusha mbali na ukapoteza maisha. Nimesoma story yake wanasema wakati fundi anachomea juu kulikuwa na mtu nadhani alikuwa anafungua mifuniko sasa kabla hajafungua fundi chini akaanza kuchomea na hapo ndipo akalipua bomu la nyuklia!