Mlioko kwenye ndoa mnashindaje hili jambo?

Mlioko kwenye ndoa mnashindaje hili jambo?

Salam wanaJf

Wanandoa mnawezaje kuishi na wenzi wenu kwa muda mrefu, mwenzi ambaye amekuzwa kwao huko, mpo tofauti kitabia na makuzi, mnawezaje kuvumiliana. Nimeuliza hili jambo ili ambao bado hatujaoa tusije wachoka wake zetu tukawafukuza bure.

Ilikuwa ni siku moja nimeweka appointment na mwanadada mmoja kuwa atakuja kushinda weekend nyumbani kwangu (nimepanga), mawasiliano yalikwenda vizuri mpaka alipofika, tulikaa vizuri ila baada ya muda nikaanza kuhisi kero, maana kuna mambo alikuwa anafanya mimi sipendelei kabisa.

Nilipokuwa nakula naye nilihisi siko sawa maana mwenzangu anatafuna bila kufumba mdomo, halafu anatafuna kwa sauti( siipendi hii tabia).

Mpangilio wa vitu ndani utabadilishwa uwe kama anavyotaka yeye, hapa nikachoka kabisa, yaani utaratibu wa maisha unabadilika kabisa.

Asubuhi tumeamka nasikia mtu ana vuta makohozi kwenye koromeo cha ajabu hamalizi, kumbe huwa ni utaratibu wake kila akitaka kuswaki, nikajikaza.

Kwa kuwa alikuwa ni girlfriend nilivumilia muda ulipokwisha aliondoka.

Hivi mnaishije wanandoa bila kuchukizana na keroa kutoka kwa wenzi wenu? na sisi mabachela tujifunze kutoka kwenu?

Mimi ninahisi hii amani na furaha niliyonayo itaisha siku hiyo hiyo nitakapooa maana yataka moyo.
Tunaishi kama wazazi wako walivyoishi, hakuna formula ya kuishi wanandoa, ila cha msingi mwanamke mwachie mambo ya ndani afanye yeye hata vyombo anunue yeye, wao hupenda kuona nyumba inakaa kwa mwonekano wanaoutaka wao.
We ndo kichwa cha familia hakikisha chakula na mboga unanunua wewe,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemwambia mke wangu akuje hapa asome comment, nahisi atajifunza kitu na kujua kwamba dunia ya vijana wa .com inaelekea upande upi...tehteehh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sikushauri uwe na mpenzi, usiku kucha hukuyaona mapungufu umekuja kuyaona asubuhi kumekucha. Nakushauri jigeuze uwe mtawa
ya usiku nimepunguza mkuu, to cut the long story short
 
hapo kutafuna kwacha kwacha kumeniacha hoi kabisa yani, mi vitabia vya hovyo hunifanya nisitishe mahusiano, sasa table manners ikimshinda mtu, it's obvious na vingine vitamshinda tu

Sent using Jamii Forums mobile app
hahaa mkuu ni kweli kuna vitabia vidogo dogo vinakwaza balaa
 
POVU RUKSA WAKUU
ndio maana wazungu wanaruhuusu watoto wao wakifika miaka 16 kuwa na GF na BF,muanze kuzoeana mapema,lkn Bongo mtu una 35 unapata mwanamke ana 30 yaani lazima kusumbuana .Mwanamke kuna vitu hutakiwi kufanya kujichokonoa puani na vidole, sijui unakula huku unaongea,kutafuna vizuri (table manners ni muhimu sana kwa mtoto wa kike),kuwa mbishi,kutema tema mate njiani nk.Kama huwezi kuvumilia inabidi uwe unamwambia kila mara,yaani ukimwambia kitu mara 10 hasipobadilika huyo kimbia babu.
MTOTO WA KIKE UNATAFUNA KAMA JENERETA?,KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA KWACHA.
Mkuu uelewa wa watoto wa kizungu na wetu ni tofauti sana, tutalea wa jukuu mpaka tukome

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikajua sijui alikuwa na tabia gani kumbe vitu vya kawaida vya kurekebishana tu!!!

Ukiona kuoa ni kazi opt upande mwingine.
aisee! itabidi tukomae hivyo hivyo, tusije zalisha mabinti wa watu na kuwaacha
 
Wewe wasema kweli!

Kumpenda binadamu kama alivyo huwa ni msemo tu, binadamu kwa asili yake tu anakera, nahisi kila mtu angekuwa anamjua mwenzake kiundani ingekuwa ni tatizo
Tafuta unaetaka utapata tu hata akiwa na mapungufu mtarekebishana pole pole kila mtu ana mapungufu yake kumbuka ila uchafu na unarekebishika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom