Mlimuona Mwakyembe jana? Ana kipaji cha ajabu...

Tungeweka juhudi katika usanii tukaachana na Michezo mingine maana hatuna vipaji upande huo ukweli tumesheheni vipaji kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi mkulu
 
Tanzania yetu imebarikiwa wanasiasa wenye vipaji vya ajabu...

Kikwete anatajwa vipaji vingi tu ikiwemo kushawishi watu wamuunge mkono
akiwahiidi hiki na asiwape....Sitta sasa tunagundua alikuwa na kipaji cha kutumia wanasiasa
wote tu..wa upinzani na wa chama chake kufikia malengo yake..

Jana watu tulimuona Mwakyembe..akionesha kipaji kingine kabisa....
kipaji cha 'kugusa watu' kupitia msiba.....

Jana watu walimuona Mwakyembe akilia na kuliza watu......akimsifia Sitta
na kusema yeye Mwakyembe nae ni 'mwanafunzi' wa Sitta....
ilkuwa kama kumuona mwanafunzi akimlilia mwalimu wake aliemkubali kuliko wote

cha ajabu Mwakyembe huyu huyu 'anampinga kabidsa Sitta' kwa matendo

Sitta anasifiwa kwa bunge lenye meno,Mwakyembe anashiriki kuliondoa bunge la sasa meno

Siita anasifika kuheshimu wapinzani na kuwapa nafasi,Mwakyembe anashiriki kuwakandamiza

Sitta alisifika kwa uhuru wa vyombo vya habari hasa bunge live
Mwakyembe anashiriki kuua yote hayo

Sitta alisifika kwakupenda sheria na kanuni ziheshimiwe,Mwakyembe yuko tayari kuzipinda
au hufurahia zikikiukwa mradi tu serikali ipate inachotaka....

Mwakyembe kaenda mbali zaidi kunukuliwa akisema 'taifa sasa halihitaji katiba mpya'
huku Sitta akiwa ndo mwenyekiti wa bunge la katiba iliyobaki kupigiwa kura tu.....

Siita atakumbukwa pia kwa kutokuwa mtu wa kujipendekeza kwa Rais au serikali bali misimamo
ndo ilikuwa inampa nguvu, Mwakyembe amewahi kunukuliwa akimsifia Magufuli katika namna unayoweza kuiita ni kujipendekeza........

Wakati jana Mwakyembe anamlilia kwa nguvu Sitta nilibaki najiuliza....Mwakyembe huyu
hiki kilio ni cha moyoni au 'anatuonesha' tu kipaji chake kingine?

Nchi hii wanasiasa wana vipaji vingi sana....kama kipaji cha kinyonga kubadili rangi kila mara...
Train ya Mwakyembe the prof of Tanganyika.
 
Kwa nafasi aliyonayo ya Waziri wa sheria na katiba angeweza kuleta mabadiliko makubwa sana. Lakini nashangaa anashindwa kumshauri Bwana Yule impasavyo kuenenda kwa mujibu wa sheria. Sheria zinanyongwa yeye anachekelea tu. Kweli mnafiki ni mtu hatari sana.
 
hata mimi niliona kipaji cha mbowe na lissu ni hatari sana, 8years walivokuwa wakiimba ule mwimbo juu ya lowassa na mwimbo wanaoimba sasa kweli tz inavipaji vya ajabu...hongera kwa wanasiasa wa tanzania wakiongozwa na mzee wa kubadili gia angani mbowe
kabisaaaaaa siasa za Tz ni majitaka.
 
That was stupid. Angekuwa na uchungu asingeliingizia hilintaifa hasara ya trillions

Crocodile tears
 
Wanasiasa Ni Ajabu Jingine Tanzania Pia Ndiyo Wanaoongoza Kwa Fitna,Undumilakuwili,Kujipendekeza,Na Mambo Yanayofanana Na Niliyoyataja
Huwezi Kuamini Hata Speaker Ndugai Anasema Aliitamani Safari Ya Mwisho Ya Samwel Sitta

Hivi Hospital Kuu Ya Watu Wenye Matatizo Fulani Ipo Milembe Dodoma Kwanini Wasiandae Workshop Bungeni Wakawapa Vyeti Tuwajue Hadharani
 
Ms
Tanzania yetu imebarikiwa wanasiasa wenye vipaji vya ajabu...

Kikwete anatajwa vipaji vingi tu ikiwemo kushawishi watu wamuunge mkono
akiwahiidi hiki na asiwape....Sitta sasa tunagundua alikuwa na kipaji cha kutumia wanasiasa
wote tu..wa upinzani na wa chama chake kufikia malengo yake..

Jana watu tulimuona Mwakyembe..akionesha kipaji kingine kabisa....
kipaji cha 'kugusa watu' kupitia msiba.....

Jana watu walimuona Mwakyembe akilia na kuliza watu......akimsifia Sitta
na kusema yeye Mwakyembe nae ni 'mwanafunzi' wa Sitta....
ilkuwa kama kumuona mwanafunzi akimlilia mwalimu wake aliemkubali kuliko wote

cha ajabu Mwakyembe huyu huyu 'anampinga kabidsa Sitta' kwa matendo

Sitta anasifiwa kwa bunge lenye meno,Mwakyembe anashiriki kuliondoa bunge la sasa meno

Siita anasifika kuheshimu wapinzani na kuwapa nafasi,Mwakyembe anashiriki kuwakandamiza

Sitta alisifika kwa uhuru wa vyombo vya habari hasa bunge live
Mwakyembe anashiriki kuua yote hayo

Sitta alisifika kwakupenda sheria na kanuni ziheshimiwe,Mwakyembe yuko tayari kuzipinda
au hufurahia zikikiukwa mradi tu serikali ipate inachotaka....

Mwakyembe kaenda mbali zaidi kunukuliwa akisema 'taifa sasa halihitaji katiba mpya'
huku Sitta akiwa ndo mwenyekiti wa bunge la katiba iliyobaki kupigiwa kura tu.....

Siita atakumbukwa pia kwa kutokuwa mtu wa kujipendekeza kwa Rais au serikali bali misimamo
ndo ilikuwa inampa nguvu, Mwakyembe amewahi kunukuliwa akimsifia Magufuli katika namna unayoweza kuiita ni kujipendekeza........

Wakati jana Mwakyembe anamlilia kwa nguvu Sitta nilibaki najiuliza....Mwakyembe huyu
hiki kilio ni cha moyoni au 'anatuonesha' tu kipaji chake kingine?

Nchi hii wanasiasa wana vipaji vingi sana....kama kipaji cha kinyonga kubadili rangi kila mara...
Hisia za msiba au kufa mtu ni tofauti na mambo ya kazi ,ya kwenye msiba tuache yawe ya msibani.
 
Back
Top Bottom