Mlimani TV, C2C na Capital zinapatiakana wapi?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,272
Baada ya kuanzishwa kwa matangazo ya digitali kumetokea msambaratiko mkubwa sana wa vituo vya televisheni hasa kutokana na kuwa na makampuni tofauti yanayorusha matangazo kwa njia ya digitali. Toka utaratibu huo umeanza vituo tajwa hapo juu vimepotea na sijui vimefungwa au vinarushwa kupitia ving'amuzi vya kampuni gani.

Ushauri kwa serikali: Naiomba serikali iweke utaratibu kuwa makampuni yote yanayorusha matangazo kwa njia ya digitali yahakikishe kuwa kila kampuni linaingiza vituo vyote vya ndani badala ya sasa kwamfano ukiwa na star times na ukataka kuangalia Clouds TV utapaswa kununua tena king'amuzi cha Zuku. Je tutanunua ving'amuzi vingapi? Kwa mtindo ulivyo sasa mtu anaweza akajikuta analazima kununua ving'amuzi vinne au vitano ili aweze kuona channels zote za ndani. Mimi naona tofauti za makampuni haya ingekuwa ni idadi na aina ya channels za nje. Za ndani ziwe kwenye kila king'amuzi!
 
Nenda analogia ndipo zilipo,ukizikosa kaulize TCRA
 
Tcra na masisiem wana ten pasent zao humu ndio maana hawataki watanzania mtabasamu hata siku moja...
 
Sasa hii ndio maana halisi ya UBEPARI! yaani ni mfumo unaotaka MATAJIRI (wenye mitaji) kuendelea kuwa matajiri kwa kuwanyonya MASIKINI (wasio na mitaji). Kwahiyo ni miongoni ya mikakati yakutumaliza masikini wakti wao wanatajirika zaidi. Kwahiyo utanunua mpaka decoder 5. Shida zako ndizo zitakazokufilisi ndugu yangu...
 
Back
Top Bottom