Mlimani City Dar: Nahisi kama maigizo na utapeli vimetamalaki

Ranger9

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
1,506
2,782
Hapa ukikaa unaweza kudhani watu wapo serious na maisha kumbe maigizo tu na vikao vingi hapa vimekaa kitapeli tapeli

Watu wawili ama watatu wanakaa kwenye moja ya coffee shops na mmoja anafungua laptop ama anashika notebook na pen

Ukitazama walivo serious ni kama kikao kizito cha biashara kubwa

Lakini kikao kinavoendelea unaona hakuna kinachosomwa kutoka kwenye laptop na hakuna kinachoandikwa kwenye notebook

And then mazungumzo unayosikia ni ya biashara ya Tzs 2 mil. ama ikizidi sana utasikia Tzs 7 mil.

Na broken english ya hapa na pale iliyotawaliwa na kiswahili kingi zaidi...like like nyingiiiiiii

Mji umejaa sanaa mingi sana huu, God have mercy🙌🙌
 
Wabongo kwa kuhangaika na maisha ya watu wengine utawaweza. Sasa kama wanajadili biashara ya milioni 2 au 7 yeye inamhusu nini? Nchi hii yaani dah!
Hahaha mimi binafsi sielewi kwanini watu wanafake maisha mazuri, ila wao kufanya hivyo hakunipi sababu ya kuwachukia wala kuwafuatilia maana hawanipunguzii chochote, hii tabia ya kufuatilia maisha ya watu ili ujue kama wako real au wanafake nayo inatakiwa ijumuishwe kwenye syllabus ya somo la uchawi
 
Back
Top Bottom