GuDume
JF-Expert Member
- Jan 18, 2015
- 6,700
- 14,647
Hili wazo niliwahi kulifikiria mara kadhaa.... na ndugu yangu Consigliere naye ameweza kulizungumzia sehemu flan kuhusiana na vituko na vitimbi vya mlimani city.
1. mlimani city ni sehemu pekee ambayo asilimia 90 ya wanaokuwepo pale wakiwa mle ndani ya eneo ni watu wa kishua sana. wamesoma shule za gharama au za nje ya nchi. wanakaa maeneo flan ya hadhi ya juu na hata maisha yao pia ni ya hali ya juu sana. ni kweli kuwa inawezekana kabisa ukapanda na wadada watatu kwenye daladala na ukawasikia wakibishana na konda yeye akitaka wamwongezee tsh 50 zake tatu katika nauli waliyomlipa wakamkatalia kabisa na kumchamba kuwa aishie zake kama hataki awashushe mbona mchana huwa wanalipa 400 badala ya 450? tena watamzogoa sana kuwa hana haya hata kama imeandikwa kwenye tiketi 450 wao ndo wanayo hiyo hiyo kama hataki awashushe. ila hawa wakifika mle ndani mlimani city wote watakwambia wakati wa kuondoka kuwa wanamsubiria dereva taxi/bajaji aliyewaleta aje kuwachukua.
2.mle ndani wadau wengi wakikutana utasikia tu umerudi lini toka usa au uk? utasikia nimekuja mara moja nlikuwa dubai ndo nimeingia jana usiku. au hapa nimekuja niangalie vitu viwili vitatu natake kesho niende canada. yaani ni watu wa mihanjo tu na uzungu zungu mwiiiiingi sana.lakini ndo maisha waliyoyachagua.
3.mlimani city kiswahili huwa hakipendezi kabisa... pale utasikia tu "yes yes mzungu kala mafenesi... ni lugha ya malkia ndo inapendeza sana. hili sijalijua linasababishwa na nini... utasikia tu hi, whatsapp. hakuna ughonile,mwangaluka,kamwene n.k lugha inachange into english medium of communication.
4. ni mlimani city pekee ambako watu huja kuzungumzia madeal makubwa makubwa huku wakitembea. usishangae kusikia mtu anazungumza kwa simu huku anatembea " sasa ile milion 80 nimeshakutumia. nimebakiza kwenye account million 200. ukinitumia mzigo nakurushia nyingine iliyobaki" au ukasikia mtu anadai "we fala hiyo mil 10 yangu unanipa lini? nataka weekend hii nikale bata ile mbaya" si ajabu ukakuta mwingine ana bargain kwenye simu " tsh mil 40 haitoshi nipatie 45 kama upo serious" ukigeuka huku unamkuta dr naye anakwambia "fanya mil 90 itapendeza zaidi" yeaah pale wanakuwepo madaktari, maprofesa,wafanya biashara wakubwa wakubwa sana.
5. vyakula wanavyozungumzia watu wa pale kuwa huwa wanakula navyo ni vya kipekee kabisa... utasikia "mi ugali siwezi kula..ni kama mdogo wangu yeye anapenda sana pizza,burger,chicken n.k ugali wali hali kabisa. sisi home ndo tulivyo...."
6. kila utakayekutana naye mlimani city utamwona mkononi anazungusha zungusha funguo.... yeaaah. maana yake amekuja na gari. si jambo baya. lakini ni utamaduni uliozoeleka sana .wakikaa watu mezani utakuta wametandaza funguo za gari na mpka kuna jamaa yangu mmoja aliondoka kwa bahati mbaya na funguo ya gari ya mwenzie ila cha kushangaza wote wawili walifika makwao kwa magari yao wakaja kukumbuka later kuwa zile funguo siyo za kufungulia mageti yao. ila kwa gari ziliwafaa...? sijui badaye waliposema watafutane kurudishiana walikuwa wote wanatumia boda boda maana wangeendeshaje magari wakati walibadilishana funguo?