Mlima Kilimanjaro wazua mzozo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mlima Kilimanjaro wazua mzozo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Sep 26, 2008.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  MLIMA Kilimanjaro umesababisha mzozo miongoni mwa Watanzania na Wakenya wanaoshiriki mafunzo ya utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa, mjini Milwaukee.

  Tukio hilo lilitokea juzi Septemba mwaka huu, wakati wakiwa darasani katika Chuo Kikuu cha Marquette, mjini hapa, chanzo kikiwa ni Dk. Thomas Bausch, raia wa Marekani, aliposema ni katika miaka ya karibuni amefahamu mlima huo uko Tanzania na si Kenya.

  "Wamarekani wengi ndivyo wanavyojua, nilishangaa sana," alisema Dk. Bausch na kuongeza kuwa Watanzania wanatakiwa kuutangaza Mlima Kilimanjaro ujulikane uko kwao.

  Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya Watanzania wanaohudhuria mafunzo hayo ya wiki sita kujibu kwa msisitizo, kwamba Mlima Kilimanjaro uko Tanzania, huku wakimwambia Dk. Bausch, 'karibu Tanzania upande Mlima Kilimanjaro'.

  Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela ndiye aliyeongoza 'mashambulizi' kwa upande wa Watanzania, kwa kumwambia Dk. Bausch ambaye ni mtu mzima wa makamo kuwa, yeye ni mmoja wa wabunge katika mkoa wa Kilimanjaro na ndiko mlima ulipo.

  Baadhi ya Wakenya walikuwa wakiingilia kati wakati Anne alipokuwa akimweleza Dk. Bausch kwa kusema 'hata ukiwa Kenya unauona Mlima Kilimanjaro.'

  Anne aliwataka wanyamaze na kuwaambia kwamba kwa muda mrefu wamekuwa wakieneza uongo huo.

  "Huo ni uongo wa kimataifa, Mlima Kilimanjaro uko Tanzania," alisisitiza Anne na kuongeza "Katika masuala ya msingi yanayohusu nchi yangu sitaki mchezo."

  Anne alitoa mfano kwamba, kama mtu ana nyumba yake, na jirani yake anaiona, je jirani huyo anaweza kutangaza ni yake kwa sababu anaiona akiwa kwake?. Dk. Bausch akajibu hapana.

  Mfanyakazi wa Wizara ya Afya ya Kenya, Sylivia Shitsama, alitoa doa zaidi pale alipohoji, kama hiyo nyumba ina manufaa na haitumiwi, kuna ubaya gani kwa mtu mwingine kuitumia. Kauli hiyo ilifuatiwa na mguno wa nguvu kutoka kwa Watanzania, wakiashiria kutokubaliana naye.

  Katika hatua nyingine, Dk. Bausch ambaye aliwahi kuwa mshauri wa wanafunzi katika chuo kikuu hicho kwa miaka zaidi ya 10, alisema aliwahi kuzitembelea Tanzania na Kenya. Alisifu Kenya wana chai nzuri, na Anne alimjibu kwamba siku nyingine akirudi Tanzania asikose kuulizia chai ya Njombe kwani nayo ni 'bomba'.

  Watanzania wengine wanaohudhuria mafunzo hayo, ni Naibu Spika Anne Makinda, Mbunge Injinia Mohamed Mnyaa na Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Caesar Waitara.

  Wengine ni Hakimu Mkazi Batista Mhelela kutoka mkoa wa Ruvuma, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya afya mkoani Kilimanjaro, Veronica Shao, Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi na Nyumba mkoa wa Ilala, Dar es Salaam, Lusungu Hongoli na mfanyakazi wa Bunge, Anselm Mrema.

  Source: Jacqueline Liana, Milwaukee, Winsconsin​
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ....Anne Kilango-Malecela

  Mwambie huyo Mkenya kuwa Wakenya ni WEZI....kwani huwezi kutumia kitu cha mtu bila rukhsa yake au makubaliano.....huo ni WIZI.......period!

  Tena mwambie huyo Mkenya hivi karibuni tutaanza kuwatangaza Kenya kama wezi wa kimataifa kwenye biashara.......kwani wanawatapeli watalii kuhusu Mlima Kilimanjaro......mifano hai ipo
   
 3. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
   
 4. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na inabidi ushirikiano wowote wa Afrika ya Mashariki usimamishwe kwanza hadi hapo Wakenya watakapo tangaza kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na sio Kenya.
   
 5. Tonga

  Tonga Senior Member

  #5
  Sep 26, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa wapuuzi nimeshawashushua mara nyingi ni wezi sana wa rasilimali na hawana hata aibu kwa hilo. Siku moja niliona kalenda kwenye stationery moja ina picha ya mlima kilimanjaro nchini Kenya, I was so pissed nikaangalia anwani ya publisher nikatuma email kuelezea kwamba sio sahihi na sio haki kwa wao kutangaza kitu bila kuwa na uhakika! baada ya mwezi wakanijibu kuwa wanalifanyia jambo hilo uchunguzi na sijawahi kuwasikia mpaka leo; it was beyond my ability I wish I was able to do more follow up.Inauma sana jinsi watz tulivyo passive hata na mambo makubwa kama haya, hiki ni kitega uchumi chetu, je wizara ya Maliasili na utalii imechukua jukumu gani katika kurekebisha hili? tusipoamka hao matapeli wakenya wanaendelea kuclaim hata mbuga zetu na kila tulicho nacho kwa simple fact kuwa " kama hatuvitumii ni vyao" au wanaziona wakiwa Kenya" how stupid is this?
  Na mkenya mwingine kwa kujitetea zaidi kuhusu mlima Kilimanjaro akasema mkoa mzima wa Kilimanjaro na Arusha ni sehemu ya Kenya waingereza waligawa mpaka vibaya; nikataka kumtemea mate usoni, na kumhakikishia mimi si mkenya hata kidogo and I Thank my almighty God for that.
  They trully piss me off.
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ukiwa Tanzania unaiona Kenya.
  Je Kenya Iko Tanzania?
  Nasikia harufu kali ya Unyang'au kutoka Tanzania Tourist Board.
   
 7. P

  Paullih Member

  #7
  Sep 26, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kuwalalamikia tu Wakenya wanapojitangazia kuwa mlima Kilimanjaro uko kenya kunatuathiri nini? kwani jirani yako akisema nyuma yako ni yake anapata faida gani wakati hata funguo za nyumba hana?

  let them say sana tu, as long as watalii wakija hawaupandi mlima kilimanjaro Kenya. Wanakuja Tanzania, wanalipa maushuru then wanakwea. what do kenyans get? Kitu pekee wanachokipata ni wao kuwa entry point ya kufika na kupanda Kilimanjaro! may be na exit point.

  sasa ili na sisi tufaidike, Tutangaze kwa bidii mlima wetu ili tupate advantege zote tatu! entry point, ushuru wa kupanda na exit point.

  tukibaki kulalamika kuwa Wakenya wanajitangazia haisaidii sana! bodi ya Utalii pamoja na Wizara ya maliasili hata na taasisi binafsi za tanzania zina wajibu mkubwa wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii ambavyo vimetapakaa nchi nzima.
   
 8. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Wakenya wanatumia vizuri fursa ya ujirani, tusiwalaumu bure sisi ndio tuliozubaa. Wao wanahimiza watalii waende Kenya kwa safari ili wawawezeshe kupanda mlima Kilimanjaro. Na kweli watalii wakienda Kenya wanafanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro japo haupo Kenya, ni rahisi tu wanawapakia kwenye mabasi wanapita Namanga to Arusha then Moshi halafu wanawaunganisha na wakala wengine, wanapanda mlima. Watalii wanapovuka Namanga kwenda Tanzania kupanda mlima wanaona kabisa wakiingia nchi nyingine, wanapogongesha passport zao pale. Kumbe wameshaeneza kuwa licha ya mlima kuwa Tz, njia convenient ya kuufikia ni kutokea Nairobi, na hapo wanavuna hela nyingi sana kwa watalii kulala kwenye hoteli zao na kununua vitu mbalimbali. Nasi pia tunapaswa kuweka vivutio vitakavyomfanya mtalii aione convenience ya kuja moja kwa moja Tanzania bila kupitia Kenya. Lawama na kelele hazitasaidia, watalii ni watu huru wanaopenda kupata thamani bora zaidi ya fedha zao, wakiona safari inakuwa nzuri zaidi kupitia Kenya wataendelea kufanya hivyo.
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Jamani raisi wetu anaweza kuamua kuwapa huo mlima wakenya manake kama ana toa mbuga za wanyama , na sehemu zingine nyingi kwanini ashindwe mlima kilimanjaro
   
 10. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kenya sio wa kulaumiwa, sisi ndio tuliowapa go ahead, kwani muda mrefu tu bodi ya utalii ilitowa ruhusa kwa baadhi ya makampuni kenya kuleta watalii kwa kupitia wapi kule!!!!!! halafu wala hakuna uhamiaji tunakuza ushirikiano na ujirani mwema, lakini funga gate farasi amepita, haya matatizo sio ya leo ni mida sana zaidi ya miaka 10 kwenye late seventy early eighty ndio ilikuwa njia
   
Loading...