Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 218
Bravo Lunyungu
Hii ni njia moja nzuri ya kuonesha kuwa haturidhishwi na huyu mtu. Ni lazima tuchukue hatua i think it is wise if we get the message sent. Lazima tuoneshe uzalendo kwa taifa letu. Wanaomtetea RA wana lao
No no no hapo bado hauja tushawishi tuache kutumia mtandao wa Voda kisa ni wa RA tena kwa hiyo mada yako isiyokuwa na ushahidi wowote. Please kama una ushahidi wa uhakika uweke hapa kila mtu aone. La sivyo hadi house girl wangu naenda kumnunulia line ya VODA. siwezi kushawishika kwa hayo maneno yako tu.
Kususia huduma za Voda and any Rostam Az related product is not a soln on ufisadi and so. If the price of using Voda is extremely higher compared wit TiGO, Celtel, Zantel and other Netwk providers kwa namna ya kifisadi, then u can convice me kuihama Voda. Mi natumia TiGO, Celtel, Voda & Zantel.
It's free market but we have to be very careful especially when it comes the issue of being against smthg coz of smthg!! Kama huduma inatolewa na fisadi lakini imezingatia taratibu za kisheria na wananchi wameridhika nayo, then binafsi siioni kama kuna haja ya kutaka kuisusia eti kwa sababu tu kuendelea kuitumia unamwongezea mafungu the owner. We gain on both sides the user (consumer) and the provider na ndo maana kuna terms of use!
jamaaa umekosa hoja ukisusia voda what next pato la taifa litashuka halafu Rostam siyo yeye ndiye mwenye hisa soln ni kumfikisha ktk vyombo vya dola ili sheria ichukuwe mkondo wake halafu kama ukiwa umezaliwa mjini unafahamu kama mengi aliwahi kuwazulumu wanzungu kutoka marekani pamoja na wafanyakazi wake katika kiwanda cha dawa za meno akasababisha hadi wazungu wapewe masaa 24 kuondoka nchini huyu...Kenya waligomea hata vyakula kwenye supermarket when they felt kwamba pesa zao zilienda kwa Kibaki na zikatumika kuwanyima haki yao .Tanzania Rostam Aziz kila kukicha ana wezi mpya lakini iko kimya na support anapewa .Sisis tuna lalamika lakini bado tunatumia huduma za simu za Vodacoma ambazo yeye ni mmoja wa share holders .Kama tuna uchungu kweli na huyu ambaye analindwa na CCM na serikali yake , tuhamie sote kwenye tigo ama zantel ama Celtel .Hii itakuwa njia nyingine ya sisi kuonyesha kwamba tumechoka kuibiwa na kuzidi kukamuliwa kila mara .Mimi nimesha hama na huhu unakaribia mwaka tangia nimejua kwamba Rostam anatumaliza bado na vodacom yumo .Mie natumia Zantel sasa na Celtel .Je wewe unangoja nini ?Tuambiane tuachana nao hawa .Wanatuona wajinga katika maamuzi yao je waendelee kutuona wajinga hata katika pesa zetu wenyewe za kutumia katika simu ?
Bravo Lunyungu
Hii ni njia moja nzuri ya kuonesha kuwa haturidhishwi na huyu mtu. Ni lazima tuchukue hatua i think it is wise if we get the message sent. Lazima tuoneshe uzalendo kwa taifa letu. Wanaomtetea RA wana lao
wakati ule unaniandikia sms kwamba unauza computer ulikuwa hutumii voda ? ulikuwa ni mtandao gani ule tena ? ulivyojifanya unafanya kazi kongo kampuni ya mtn lakini uko kigoma kwa muda
hebu nikumbushe
Inaweza Kuwa Kweli Alivipata Kwa Ufisadi.lakini Kashfa Zote Za Ufisadi Zimetoka Mwaka 2004/2005 Wakati Yayari Vodacom Ilikuwepo.sasa Hapo Ilianzishwaje Na Hizo Pesa????au Inakuwa Hadithi Ya Mwana Kondoo Ya Kuwa Kama Siyo Wewe Basi Ni Babu Yako Na Lazima Ni Kule?
Kuna maswali kadhaa,
-Je shares za Caspian T LTD(zilinunuliwa kwa hela za kifisadi)
-Ilikuwaje Shares za Caspian kuongezeka wakati za Planetel zikapungua na Shivacom kuondolewa?
-Hizi kampuni nyingine zina nafuu? najua Celtel wamenunuliwa na Zein/Zain, Tigo from my understanding wako owned na Mic T LTD na Ultimate Security(ambayo inamilikiwa na muungwana mmoja ambaye naye ametajwa kwenye some of the dubious deals)
Superb! I like you, always sounding like a concerned TISS associate!
Asha
Ilianza mwaka 2000 ambapo tayari huyu Bwana alikuwa tayari ameshafilisi viwanda vyetu vya ngozi, tayari alishategeneza himaya yake ya kisiasa ndani ya CCM na kuitumia kuhakikisha kampuni yake ya Caspian inapata kandarasi serikali. Na kampuni hii ndio yenye mahisa humo vodacom. Lakini alikuwa pia na makampuni mengine pembeni yaliyokwiba fedha za mfuko wa Japan. Na pia lile kampuni lake lingine lililojibebea fedha za import support. Halafu akaendeleza mtaji wake miaka ya 2002-2006 kwa kutumia mafedha mengine ya BOT. Huyu ndiye Kagoda ninayemfahamu! Sasa ni bilionere, hata mkimchanganya vodacom, mkono wake upo kila mahali. Upo TICS, msuse kuingiza makontena. Upo habari corporation, msuse kusoma rai na mtanzania. Upo Mwananchi, nako pia msuse. Lakini upo pia ndani ya CCM, hisa zake huko ni nyingi zaidi. Mkitaka kumkomoa basi mjitoe kwenye Chama Cha Mafisadi(CCM),atabaki tu na vile vitega uchumi vyake vilivyopo Oman, Iran, Maritius etc. Hivi ile tenda ya kujenga kiwanja cha ndege alishakamilisha?
Asha