Mkwamo wa Bunge kikanuni bila kambi Rasmi ya Upinzani

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
84
1,562
Na Bashir Yakub, WAKILI

Kanuni ya 135(11) ya Kanuni za Kudumu za Bunge za June 2020, inasema kuwa " Wenyeviti wa Kamati ya Hesabu za serikali(PAC), na Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) wanatakiwa kutoka Kambi Rasmi ya Walio wachache Bungeni".

Kwanza kwa Kanuni hizi mpya hakuna kitu kinaitwa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, bali imebadilishwa na kuitwa Kambi rasmi ya walio wachache Bungeni.

Kanuni niliyotaja hapo juu inatafsiri kuwa hapawezi kuwa na kamati PAC na LAAC bila kambi rasmi ya walio wachache bungeni.

Na ili iwepo Kambi rasmi ya walio wachache bungeni ni lazima wabunge wa upinzani wafikie 12.5% ya wabunge wote kwa mujibu wa kanuni ya 21.

Mkwamo wa bunge la sasa ni kuwa wabunge wote wa upinzani hawafiki 12.5% ili waweze kuunda hiyo kambi rasmi.

Na kama hawawezi kuunda hiyo kambi maana yake kamati ya PAC na LAAC haziwezi kuwepo kwakuwa haziwezi kupata mwenyekiti aliyetakiwa atoke katika hiyo kambi.

Na bahati mbaya Kanuni hazisemi nini kifanyike iwapo Kambi rasmi haipo, au ikiwa upinzani haujafikia 12.5%.

Je inawezekana Bunge kuendeshwa bila Kamati muhimu na za lazima kama PAC ya hesabu za serikali na LAAC ya hesabu za serikali za mitaa?

Jibu ni hapana haiwezekani. Jambo moja kati ya matatu litatokea.

Moja, hiyo idadi ya 12.5% ilazimishwe ipatikane ili Kambi Rasmi ya Waliowachache Bungeni iwepo ili Wenyeviti wa PAC na LAAC wapatikane.

Mbili, itumike kanuni ya 174 ambayo inatoa uhuru kwa mbunge yeyote, waziri, au mwanasheria mkuu wa serikali kuleta Hoja ya kuomba Kanuni yoyote katika Kanuni za Kudumu KUTENGULIWA kwasababu na malengo maalum.

Maana yake mleta hoja ataomba Kanuni ya 135(11) inayolazimisha wenyeviti wa PAC na LAAC kutoka kambi rasmi ITENGULIWE, na baada ya hapo mwongozo mpya utatolewa.

Tatu, itumike Kanuni ya 2(2) inayomtaka Spika kutumia Sheria nyingine, Maamuzi ya mabunge yaliyopita, mila na desturi za mabunge, ikiwa kuna jambo au shughuli imejitokeza lakini haijaelezwa kwenye kanuni.

Nauona mkwamo huu ukimalizwa na moja kati ya haya matatu.

Wasalaam.
 
Bashir Yakub hivi tatizo liko wapi, kama wameweza kuiba kura "kifala" namna hii, bila chembe ya aibu, si waendeshe bunge at their own leisure, kwani nani atawauliza? Kama wamefanya ubatili huu wa kura bila kuulizwa, na hili waendelee wanavyotaka.... simple! lawlessness country!
Point tupu. kwani watashindwa kubadili hizo kanuni?
 
Na ndio maana Ndugai aliahirisha bunge ili wabunge wakafanye shopping, kupiga selfie viunga vya bunge na wengine kuanzisha connection mpya huku nyie mawakili maslahi mkiangalia namna ya kutengua kanuni kisheria ili mlazimishe bunge lisonge 'kizombiezombie'.

Jiwe ni nuksi na laana ya Taifa.
 
Na ndio maana Ndugai aliahirisha bunge ili wabunge wakafanye shopping, kupiga selfie viunga vya bunge na wengine kuanzisha connection mpya huku nyie mawakili maslahi mkiangalia namna ya kutengua kanuni kisheria ili mlazimishe bunge lisonge 'kizombiezombie'.

Jiwe ni nuksi na laana ya Taifa.
Ndicho kinachotafutwa
 
Nilitegemea kukusikia ukitoa mawazo yako na mchango wa elimu yako ya sheria kuwezesha wananchi wote waliodhulumiwa haki ya kuwakilishwa na viongozi waliowachagua kihalali wanafungua kesi katika mahakama zote nchini kudai haki zao, ili kusaidia wabunge halali warudi bungeni! Lakini inashangaza unasaidia waliodhulumu wazidi kuhalalisha dhuluma zao! Mwenyezi Mungu akulipe sawasawa na matendo yako!
 
Siasa ni sayansi, MAENDELEO ni sayansi.

Hakuna tena mtu wa kupiga a kelele na CCM baada ya kutoheshimu sanduku la Kura. Ccm waliopata Kura 12 milioni, watanzania wapi 60 million. That means watanzania 48 milioni wamekaa wanawatazama walio 12 milioni kufanya kazi kutimiza ilani yao ya uchaguzi. Hakuna maswali wala majibu.

Wenzenu wamekaa sasa jengeni barabara wao watapita huu yake,nunueni ndege wao watapita fedha wanazipanda.jengeni hospital wao watatibiwa.mkishindwa mtakuwa mmejidhitaki wenyewe kea wenzenu 12 milioni
 
Mjinga ni mjinga tu kanuni ni vitu vya kutengeneza sio sheria ya bunge. Vinaweza kubadilika anytime. Wakili anakubuluza alafu unatukana na kushabikia upuuzi.
Kwanini mtengeneza vitu halafu,mvibadilishe mkiona haviendi Kwa manufaa yenu??

This happen only in Sub Sahara Countries, Shit hole countries..

Hivi ulivyojibu tu inaonyesha malezi uliyopata kutoka kwa wazazi wako,umelelewa Kwa viboko

wazazi wamefikisha ujumbe kwako kutumia vitisho,na unaviendeleza Kwa Wengine

unaamini kuwa ujumbe haumfiki mlegwa mpaka Kwa fujo,vitisho na Matusi

Sasa Matusi ya nini Kaka,UJUMBE utanifika bila ya kutumia matusi
 
Back
Top Bottom