Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi Sofia na ulevi wa madaraka

Kwa hiyo kuvaa vimini ni marufuku kwa wakazi wa Temeke? (Wilaya ya huyo Mama). Vipi mtu akitokea Ilala akaenda Temeke kutembea naye itabidi alambwe Bakora? Sijasoma hiyo taarifa lakini hwezi kupiga marufuku uvaaji wa vimini kwa ujumla wake bali angekataza labda watu wanaokwenda kwenye maofisi ya serikali na wafanyakazi kwenye hizo ofisi za serikali wasivae vimini ingekuwa sawa. Sasa mtu wa mtaani akivaa kimini wewe anakuhusu nini?


Tiba
Kuwa mkuu wa wilaya hakumfanyi huyo mama awe juu ya sheria ,hakuna sheria inayosema ukivaa kimini ucharazwe bakora,hakuna,tuheshimu sheria na si kufanya vitu kwa hulka au utashi wa muhusika,haya mambo ya viongozi wa wilaya na mikoa kutoa maamuzi bila kuangalia sheria ndio yaliyoleta mtafaruku wa kuchinja wanyama huko Nyehunge Mwanza,wangefuatari sheria yote hayo yasingetokea,kwani hakuna palipoandikwa wanyama wachinjwe na waislamu tu,bali tulifanya mazoea ya kujifanya waislamu peke yao ndio wana haki ya kuchinja
 
Enzi zile tuna ma District Commissioner wa kweli walikuwa wanapelekwa shule kusoma masomo mbalimbali ambayo yalikuwa nyenzo zao za kazi. Siku hizi wananenda ngurudoto kwa ajili ya semina elekezi wakitoka huko hayo ndio matokeo yake.

Hajataja Kosa, hajataja ni kinyume cha kifungu gani etc
Hata kama amefanya kosa DC hana mamlaka ya kuhukumu,kwani mahakama pekee yenye jukumu hilo kikatiba
Hata kama akipatikana na hatia kuna mitigation, sio lazima kila anayevaa nguo fupi anapenda labda hakuwa na hela za kushona nguo inayifika magotini.
Hata kama alivaa nguo fupi kuvutia watu wa jinsia nyingine bado anaweza kufanya mitigation inayoweza kuonesha kuwa anafanya hivyo kwa sababu ya kutatua matatizo yake.
 
tusubiri kauli ya waziri stephen wasiraaaah!

Wasira kashindwa kutatua mgogoro wa kuchinja Ng'ombe mwanza, sidhani kama anaweza kutatua mgogogro huu.

Ule wa mwanza angeweza kuutatua bila hata kupanda ndege na kuiingiza serikali katika hasara isiyo ya lazima.
 
Tunataka nchi yenye kufuata utawala wa sheria.

Sheria hiyo ipo?

Kama ipo imeidhinishwa na bunge/ vyombo husika?
 
Hivi kimini kinatafsiriwaje!?je ni nguo fupi kuanzia wapi!!this is non sense!!nadhani kila mtu anamtazamo wake wa ufupi wa nguo..naona mama anataka kuleta balaa mitaani
 
uchi gani anaouongelea huyo bi sofia? angetoa mifano ya picha tusijeanza kuchapana bakora kumbe tafsiri ya uchi inatofautiana kati ya watu na watu.
 
hebu tujiulize, jamaa ameweka heading tu... mapovu yanatoka midomoni, kwanini asiweke habari note tukapambanua?
 
Huyo mama zimemtoka ajui kuwa hiyo ni ukandamizaji wa haki za binadamu kwani kuvaa nguo fupi ndo nini! Viongozi wetu wakilala na kuota mandoto yao bila aibu anayafanya ndo sheria!
 
Hakuna imani inayohubiri kuvaa nusu uchi

tofauti yetu na wanyama ni pamoja na kujisitiri
 
Hakuna imani inayohubiri kuvaa nusu uchi

tofauti yetu na wanyama ni pamoja na kujisitiri

Unazungumzia dini zipi wewe? Mini inakukwaza kitu gani kama siyo tamaa zako? Acha dada zetu wavae nguo wanavyotaka. Unoko nyumbani kwako.
 
mimi si dhani kama kuna haja ya kumuhukumu huyu mama,nadhani dhamira yake ni kwamba watu wawe na maadili mazuri,ila na huyu mama aelewe kwamba swala la maadili ni pana sana,si kuvaa nguo fupi tu,ila ni swala zima la ufisadi,sasa kama akitaka kumeintain naadili katika wilaya yake,aanze na ufisadi kwanza ndio aje kwenye maswala mengine.
 
Akamchape kwanza bakora katibu wa chama chake kwa kuuza meno ya tembo,mnafiki mkubwa huyu!
 
jamani namtetea huyu mama, si kweli kuwa alisema hivyo ila alichosema ni kwamba (akitoa mfano) enzi za ukoloni wanaovaa hovyo walikuwa wanakamatwa wanachapwa viboko. katika maongezi yake. nimemsikia akihojiwa na clouds FM alipopigiwa simu aeleze alimaanisha kitu gani akajibu waliomnukuu wameongeza chumvi hakusema hicho kitu. tuwe makini waandishi wa siku hizi hawana weledi wanataka kuuza magazeti.
 
Nahc vmimi co jambo zuri kwa kuangalia maadili ye2 ila pia adhabu ya bakora haifai kabisa kwa binaadam hata akiwa nakosa gani!?
 
Back
Top Bottom